Shida na raha
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 3,773
- 3,474
Au ndo yule aliemuimba mr ebo? " kamongo umemfanya nini perege ana.........."
Ha,haaaa....tena akiwa na dida patanoga zaid mana litakua ni colabo zuri sana la michamboTZApewe kipindi cha B.chau,kina mfaa sana
Asante kwa kutaka kujua Perege ni samaki wa aina gani, Perege ni Samaki ambaye yuko kwenye kundi la samaki aina ya Sato, (Tilapia) wao wana ukubwa wa kati na wanaweza kukua hadi kufikia kilo moja na nusu ukilinganisha na Sato wekundu, Sio rahisi akuwe kuvuka kiwango hicho.Tuelezee wewe basi perege ni samaki wa aina gani
Hamna samaki anayeitwa kambare labda kambaleSamaki anayependa kuishi kwenye tope ni kambare sio perege
Asante kwa shuleAsante kwa kutaka kujua Perege ni samaki wa aina gani, Perege ni Samaki ambaye yuko kwenye kundi la samaki aina ya Sato, (Tilapia) wao wana ukubwa wa kati na wanaweza kukua hadi kufikia kilo moja na nusu ukilinganisha na Sato wekundu, Sio rahisi akuwe kuvuka kiwango hicho.
Hawezi hata kidogo kuishi kwenye matope kwani hutegemea zaidi hewa ya oksijen.Utafiti umefanyika katika nchi nyingi na kuonelea kuwa samaki aina ya perege/ngege/sato [tilapia] anafaa kufugwa katika mabwawakulinganisha na aina nyingine. Samaki wa aina hii wana sifa nzuri sana kwani; huishi kwenye maji yenye joto la kadri katika nchi nyingi, wanaweza kuzaana kwa wingi katika mabwawa, hula majani na chakula kingine chochote kinachopatikana kwa urahisi shambani au nyumbani, hukua kwa haraka, uvumilia sana changamoto za bwawa hii ikiwa ni mabadiliko ya joto, hewa ya oksijeni, na pH, pia nyama ya samaki hawa ni tamu na yenye ladha nzuri.
Kuna aina nyingi za sato(tilapia) kama vile Sato mwekundu, Sato wa Msumbiji, Sato mweupe na Sato wa Mwanza.
Sato hawa hula mimea na majani, huhitaji chakula kingi na huzaana sana, wana doa moja kubwa kwenye pezi la mgongoni. Sato hawa hula vijimea vya plankiton, hukua kwa haraka na wana mistari kwenye mikia. Aina nyingine za samaki zimechanganyikana na kuwa machotara hivyo siyo rahisi kuwatambua.
Nadhani utakuwa umelewa kidogo kuhusu Perege, kwa wale wanaotoka Musoma Vijijini, Ukerewe, Mwanza na Bunda kwao sio Tatizo kumfaham Perege, lakini pia wale wanao toka maeneo ya Bwawa la nyumba ya Mungu, ziwa Mdoli nk.
Asante.
Ephrahim Kibonde wa cloud sio lazima uelezee kila kitu wewe, mnakuwa watatu kwenye kipindi acha wanzako au mwenzako anayekuwa na uelewa fulani muwapo studio aelezee, na rudia tena siyo lazima wewe. Mara nyingi nimekuwa nikiona comment humu ndani watu wakikuelezea ktk mtazamo hasi. Lakini wengi wamekuwa wakisisitiza kuwa upuuzwe, binafsi nimeona siwezi kukupuuza kwani umeendelea kupotosha katka mambo mengi sana uwapo studio na mengi ni mambo madogo lakini yenye madhara makubwa kwa kizazi kijacho.
Mfano jana wakati unaongelea tukio la yule jamaa wa Mbeya ambaye alifariki kutokana na kumeza samaki aina perege. Tukio lilikuwa sahihi make lilithibitishwa na RPC wa mkoa husika.
Hoja yangu ni pale ulipokuwa unajaribu kuongelea ama kumwelezea perege na ukadai unamfaham vizuri perege ni Samaki ambaye anweza ishi hata kwenye tope, ama anafuata Tope pindi maji yakikauka. Kibonde sio kweli watafute watalaam wa mammbo ya viumbe wa majini, kwa maana ya ziwani na bahari watakusaidia kufahamu vizuri zaidi. Pia jenga utamaduni wa kusoma ili uwe na uelewa ma mambo zaidi.

Hamna samaki anayeitwa kambare labda kambale