Kiboko ya vigogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiboko ya vigogo

Discussion in 'Sports' started by dazu, Apr 11, 2011.

 1. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wanajamvi wenzangu ambao ni wakongwe kidogo na wafuatiliaji wa soka, bila shaka tutakua tunakumbuka kwamba kulikua na timu ilikua inajulikana zaidi kama kiboko ya vigogo. Nayo ni Reli ya Morogoro. Kikosi chao cha miaka hiyo huwa kinanivutia hata leo, kwa jinsi kilivyokua kinatoa wakati mgumu kwa timu kongwe kama simba na yanga. Kikosi hiki golini alikua anasimama Athumani Msumari, Full beki 2 Mohamed Mtono, 3 Abdalla Mkali, 4 ni Ramadhani Kilambo, Sentahafu Gasper Lupindo, namba 6 ni Christopher Maiko, winga namba 7 ni Nassib Abbas namba 8 Yusuph Macho wakati mwingine hucheza Bonifas Njohole, Sentafowadi yupo Duncan Butinini, namba 10 David Mihambo halafu winga ya kushoto hucheza Mbui Yondan au Peter Mjata. Kikosi hiki ambacho kilikua chini ya Simkoko, Kilikua ni hatari mno hasa kinapokutana na yanga au simba.
   
 2. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Umemsahau Dr Madundo Mtambo.
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280

  Alikuwa mkali sana,siku hizi ni Prof.
   
 4. dazu

  dazu JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 365
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wachezaji zamani walikua wanazingatia shule, sasa hivi akisajiliwa ligi kuu na shule basi.
   
 5. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Kweii kabisa,lakini pia zamani ilikuwa ni kucheza kwa kujifurahisha,heshima na sifa.Siku hizi ni pesa mbele na akishanunua ki corola ndo unamkoma kabisa...,totoz na kinywaji kwenda mbele.
   
 6. M

  Masuke JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  David Mihambo yuko wapi siku hizi, kuna kipindi alichezea Simba na kulikuwa na mechi kati ya Simba na Gor-mahia alinikomeshea sana wale wakenya.
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mbui Yondani naye yuko wapi alikuwa balaa jamaa?
   
 8. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Imebaki historia tu,bado simba na yanga wababe ktk soka la tanzania,
   
Loading...