KIBITI: Watu watatu wameuawa akiwemo Afisa wa Upelelezi (OCCID)

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,

Mkuu wa Wilaya Gullamuhusein Kifu amethibitisha kuwa watu watatu akiwemo ofisa upelelezi, Peter Kubezya wameuawa kwa kupigwa risasi katika Kijiji cha Jaribu.

Taarifa zaidi zitakujia kupitia uzi huu....

=========

Kibiti. Watu watatu akiwamo OCCID wa Wilaya ya Kibiti, Peter Kubezya wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na watu wadhaniwa kuwa ni majambazi katika Kijiji cha Jaribu wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gullamuhusein Kifu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema watu sita wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto walikivamia kituo change Wiley's cha kukusanyia ushuru kilichopo kijijini hapo.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia leo Jumatano ambapo watu hao wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki walivamia kuzuizi cha maliasili kilichopo kijijini hapo na kukichoma moto kabla ya majibizano ya risasi na polisi wakiokuwa doria kwenye eneo hilo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Misheni ya Mchukwi, Zakaria Lukeba amethibisha kufikishwa kwa mwili Kubezya ukiwa na jeraha la risasi tumboni pamoja na maiti mbili ambazo hazijajulikana majina.
 
Wame uawa na Nani au hata kama taarifa itatujia baadae ni vizuri pia ungedokeza wamepigwa risasi na nani, majambazi au aina ya wale wajahidina wa kimanzichana, au wananchi wenye asira kali, au Askari wa kule selou?
 
Habari wanaJF,

Mkuu wa Wilaya Gullamuhusein Kifu amethibitisha kuwa watu watatu akiwemo ofisa upelelezi, Peter Kubezya wameuawa kwa kupigwa risasi katika Kijiji cha Jaribu.

Taarifa zaidi zitakujia kupitia uzi huu....
Chanzo cha mauaji ni nini?
 
Back
Top Bottom