Kibiti imetulia, hongera IGP

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
MWANZONI mwa mwezi uliopita, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema atashughulikia matukio ya mauaji ya raia yaliyokuwa yakiendelea kutokea mkoani Pwani.

IGP Sirro alitoa kauli hiyo Julai 5, 2017, wakati wa makabidhiano ya magari manne ya polisi yaliyotolewa kwa njia ya msaada na kampuni moja ya binafsi nchini.

Katika kauli yake alieleza namna isivyokuwa kawaida yake “kusemasema” na akasisitiza kwamba muda si mrefu angetoa majibu kuhusu ukomeshaji wa matuko ya mauaji ya raia wasio na hatia mkoani Pwani.

IGP Sirro alisisitiza kwamba Watanzania, katika maisha yao ya kawaida, hawajazoea mambo ya fujo na kwa hiyo, kwa kauli yake alitamka; “..wale waliotumwa kwa ubaya ubaya sisi tunawajibu vibaya vibaya.”

Kauli hiyo ilipokewa kwa hisia tofauti na Watanzania, wengine wakiamini ni kauli thabiti dhidi ya wanaotishia kuvuruga amani ya Tanzania lakini wapo waliodhani kauli hiyo ingeweza kuchochea zaidi vitendo vya mauaji katika maeneo hayo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani Pwani.

Ni takriban mwezi mmoja sasa umepita tangu ahadi hiyo ya IGP Sirro itolewe. Kwa ‘jicho’ huru la tathmini kuhusu hali ilivyokuwa awali na sasa, ni dhahiri kwamba kazi kubwa imekwifanyika na huenda kinachoendelea sasa ni kukamilisha sehemu tu ndogo ya kazi iliyosalia. Tena, tunaamini kwamba, kazi hiyo imefanyika kwa mafanikio makubwa.

Matukio ya mauaji ya kupangwa yamepungua kama si kutoweka kabisa katika maeneo hayo. Kwa hiyo, kwa upande wetu tunatoa pongezi kwa IGP Sirro na askari wote wa Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi vilivyoshiriki kuhakikisha raia wa maeneo hayo wanaishi kwa amani kama ilivyo raia wenzao wa Tanzania katika maeneo mengine ya nchi.

Lakini mbali na kumpongeza IGP Sirro na askari wengine wote walioshiriki kukomesha matukio hayo yaliyokuwa yakichafua taswira ya Tanzania katika majukwaa ya kimataifa, tunatoa pongezi pia kwa wananchi waliojitoa kusaidiana na vyombo vya dola kukomesha kadhia hiyo.

Tunasisitiza kwamba, popote pale, ni haki na wajibu wa raia mwema yeyote kushirikiana na vyombo vya dola kukomesha mambo yanayokwenda kinyume cha maisha halisi ya Watanzania, maisha ya kudumisha amani na utulivu.

Ni matumaini yetu kwamba, ushirikiano baina ya vyombo vya dola na raia wema utaendelea kudumishwa na pande zote hizo mbili kwa masilahi mapana ya taifa hili. Hongera IGP Simon Sirro.


Raia mwema
 
Jumla waliouwa ni wangapi hadi sasa?
Wauaji siyo magofu yaliyosimama ambayo unaweza ukayahesabu. Hawa ni watu wenye malengo maalum na wanaanzia kwa wauaji wenyewe hadi wafadhiri wao. Mauaji yamekoma lakini lazima tunakwenda mbali zaidi kuchunguza kama wapo wengine sehemu yoyote duniani. Lazima tujue mambo mengi kwa ujumla wake kama vile iwapo yalilenga eneo hilo tu la nchi, iwapo yalihusiana na siasa au biashara haramu, iwapo yanatokea ndani pekee na hayana uhusiano na nchi za nje,..... hivyo hatuwezi kupata jibu lako kwa wakati wowote ule!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kupata wachangiaji mkuu....labda ungeandika Kibiti kumeanza tena watu kuuawa!
 
Back
Top Bottom