Kibanzi cha jichoni kwako nani akutoe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kibanzi cha jichoni kwako nani akutoe?

Discussion in 'International Forum' started by nyihirani, Apr 1, 2011.

 1. n

  nyihirani New Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tumekuwa tukijadili hasa nani kafanya nini na wapi,haitusaidii hilo badala yake tufanye kazi na tuwe na upendo misimamo ya vyama vyetu tusiingize ktk familia zetu tutazibomoa tishindwe kuzijenga.
  hakuna nchi wala mtu aliye wahi kufanikiwa kwa kukaa na kulalamika hata siku moja,watanzania wenzangu mambo mengine yanatupunguzia siku za kuishi.
  unajisikiaje mtu uliyemaliza nae masomo anavyopiga hatua mbele ya kimafanikio na wewe ukiwa kijiweni ukisubiri mtu anunue sigara au muhindi ugongee mwisho wa siku tunakimbilia kusema fulani mwizi haibadili maana ya yule ni tajiri na wewe ni maskini.
  inatuonyesha ni jinsi gani tulivyo wachovu wa kufikiri hivi muda tunatumia kutafuta vitu kama hivyo ni vipi kwa wale walio soma science wengetumia muda huo kuangalia vitu vya kutusaidia kuliko kutuumiza.
  leo india miaka 10 iliyopita ilikuwa ni nchi ya 2 kwa umaskini duniani lakini leo sisi leo bado tupo ndani ya 5 bora ya nchi maskini na india huwezi tena kusema.
  vijana tufanye kazi tuache utegemezi 40 mil ya watu wanao fanya kazi ni 1/4 ya hao na wengine tumekuwa tegemezi unadhani kweli tutalisaidia taifa letu au tunaliangamiza taifa letu?
  MUNGU ALIHAIDI PEPO LAKINI PEPO HAIKUFUATI BILA KUITUMIKIA .
  MAISHA MAZURI HAYAJI BILA YA KUFANYA KAZI.
  WABUNGE MSILALAMIKE KAMA WANAWANCHI BALI LAZIMA MUWE MFANO,leo munasimama majukwaani mkihubiri juu ya ufisadi na wizi na huku mkisema maisha magumu kwa wananchi bila hata ya aibu juzi munapewa 90mil ya magari na mkiomba pia muongezewe posho ya kamati zenu.
  mwl anayelipwa 150,000/= atafanya kazi yake kwa miaka mingapi kufikia 90mil uliyopewa/kukopeshwa.?
  kumbe hata viongozi wetu wengi wa siasa ni wanafki kwetu,yani wanahuruma ya mamba.
  vijana wenzangu hizo ni changamoto mie sina mkondo wowote wa kisiasa kama wengi wenu humu.
  small minds discuss people
  average minds discuss event
  great minds discuss idea
   
Loading...