Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Kibanda: Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Status
Not open for further replies.

kanda2

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2007
Posts
1,319
Reaction score
76
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima bwana Kibanda ameandika makala kwenye gazeti la Tanzania Daima kumshutumu Zitto Kabwe kugombea uenyekiti Chadema.Kibanda anafanya kazi chini ya gazeti la Mbowe,swali Mwalimu Nyerere alipewa Uenyekiti wa Tanu akiwa chini ya miaka 30,

Chadema ni Chama cha demokrasia kwanini Kibanda aogope Chadema watimize kauli yao ya Demokrasia kwa Vitendo? kama Kigezo ni Umri Marekani wangempa John MC CAIN kwa vile ni mtu mzima ana mvi kichwa chote. Tanzania Daima la leo lina habari mbili zote za Zitto Kabwe.

Naliona anguko la Zitto Kabwe!

Absalom Kibanda

NAOMBA nianze makala yangu hii kwa kuwaomba radhi sana wasomaji wa safu hii, ambao wiki iliyopita niliahidi kuendelea na hoja yangu kuhusu tatizo la ushabiki wa kisiasa, ambalo limekuwa likiliandama taifa hili kwa miaka mingi sasa.

Nimelazimika kuomba radhi kutokana na ukweli kwamba, nimejikuta
nikipaswa kuachana na mada hiyo ya ushabiki wa kisiasa , baada ya kuibuka kwa moja ya mambo mazito katika siasa za ushindani na hususan katika medani ya ujenzi wa demokrasia madhubuti ndani ya vyama vya siasa vya upinzani.


Kikubwa kilichosababisha nifikie uamuzi huo, ni tukio kubwa na la kihistoria lililojitokeza wiki hii, ambalo mwanzo wake uko ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho hakuna shaka kwamba, afya yake ya kisiasa ya jana, leo na kesho ina mchango mkubwa katika maendeleo ya kisiasa katika taifa letu.

Tukio hili ambalo baadhi ya watu wanaweza wakaliona kuwa ni dogo na pengine lisilo na maana kubwa, ni lile la uamuzi wa mwanasiasa mchanga na kipenzi cha watu, Zitto Zubeir Kabwe, kuamua kujitoa mhanga na kugombea nafasi ya uenyekiti wa taifa wa CHADEMA.

Niseme bayana kwamba, uamuzi huo wa Zitto, mwanasiasa kijana aliyejizolea umaarufu mkubwa tangu alipoingia katika siasa za kitaifa ndani ya Bunge mwaka 2005, unaonekana waziwazi kuitikisa CHADEMA, na kwa kiwango kikubwa kugusa hisia za viongozi na wanachama wake na wale walio nje ya chama hicho.

Kikubwa kinachoonekana kuzusha maswali vichwani mwa watu wengi, nikiwamo mimi mwenyewe, ni uamuzi wa kijana huyo kuamua kugombea nafasi hiyo pasipo kujali iwapo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe anayemaliza muda wake atachukua fomu au la.

Ingawa watu wanaofahamu ujasiri wa Zitto katika kuchukua maamuzi mazito tangu akiwa shuleni na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaweza wakawa hawajashtushwa na uamuzi wa kijana huyo, ni wazi kwamba, hatua yake ya safari hii itakuwa imewafanya waanze kujiuliza mara mbili mbili kulikoni!


Katika hili la uenyekiti wa taifa wa CHADEMA, naweza kusema waziwazi kwamba, hata kwangu mimi ambaye mara kadhaa nimepata fursa ya kushiriki katika mawazo na maamuzi kadha wa kadha ya Zitto, nimejikuta nikishtushwa na namna alivyofikia uamuzi huu na kuutekeleza.

Ingawa nilikuwa nikijua japo kwa sehemu ndogo kuwa, Zitto alikuwa akipita katika tanuri gumu la kimaamuzi juu ya ama kugombea uenyekiti wa CHADEMA au kutogombea, bado sikuweza kujiaminisha kwamba, kijana huyu niliyemuunga mkono wakati wote alipokuwa akisimamia baadhi ya mambo makubwa ya kisiasa, angefikia hitimisho la kuwashtua watu wengi kwa uamuzi wake huu.

Watu wanaojua masuala ya CHADEMA ni mashahidi wazuri kwamba, uamuzi huu wa Zitto kuchukua fomu kupambana na Mbowe ambaye yeye mwenyewe (Zitto), mara zote amekuwa akimtambulisha kuwa ni 'mentor' wake wa kisiasa ndani ya chama hicho cha upinzani, tena kwa staili ya kumshtukiza, umesababisha mtafaruku mkubwa wa mawazo.

Ni wazi kwamba, uamuzi huu wa Zitto kuchukua fomu, kwa kiwango kikubwa umekuwa ni wa faraja kubwa kwa wana CCM, ambao siku zote wamekuwa wakitaka kuiona CHADEMA ikisambaratika na kukipa fursa chama hicho tawala kupumua.

Watu tunaolifahamu hilo kwa ndani, tunatambua vyema kwamba, kwa CCM na kwa maofisa usalama wa taifa waliolelewa katika mfumo wa siasa za chama kimoja, kuanguka au kuporomoka kwa uimara wa CHADEMA wa leo hii, ni jambo la kuliwekea mikakati na kwa kiwango kikubwa kulishangilia.

Kwa wana CCM na wapambe wao hao wa ‘kiusalama', hatua yoyote ya kuwang'oa kutoka katika madaraka ya CHADEMA au ya kuwadhibiti watu wa aina ya Mbowe, Dk. Willbrod Slaa, John Mnyika na wanasiasa wengine madhubuti wengi tu wa ndani ya chama hicho cha upinzani, ni ya kushangiliwa na kuungwa mkono.

Ni wazi kwamba CHADEMA chini ya uenyekiti wa Mbowe na ukatibu mkuu wa Dk. Slaa, pamoja na kuwapo kwa kasoro zake nyingi za kiutendaji, kiutawala, kimfumo, kisera na pengine hata kiitikadi, imepiga hatua kubwa katika medani ya ushindani wa kisiasa ndani ya nchi hii.

Watu wanaofuatilia historia ya CHADEMA ya siku na miaka ya hivi karibuni, ni mashahidi wazuri kwamba, chama hicho kimeweza kujijengea misingi bora na imara kisiasa, kiasi cha watu wengi kukijengea imani na matumaini makubwa kwamba, kinaweza kikafanya mambo makubwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Dalili hizi za CHADEMA kujijengea uhalali ambao umejidhihirisha wakati wa chaguzi mbalimbali ndogo zilizofanyika katika miaka ya hivi karibuni, kama zile za Tunduru, Kiteto, Tarime, Mbeya Vijijini, Busanda na Biharamulo, zimekuwa zikikifanya CCM na majemedari wake wa mikakati kujipanga na kukesha wakikiwinda, usiku na mchana.


Mawindo hayo dhidi ya CHADEMA yamekuwa yakijionyesha waziwazi kupitia katika vyombo vya habari, ambako kila mara taarifa za kupikwa na kufinyangwa dhidi ya chama hicho na viongozi wake, kama
akina Mbowe, zimekuwa zikiandikwa mfululizo na kupewa uzito mkubwa.


Kwa ustadi mkubwa wa kufinyanga uongo, mawakala wa CCM wamefanya kila linalowezekana kumchimba Mbowe wakitumia falsafa ya Kibiblia isemayo; ‘Mpige mchungaji, kondoo watawanyike' ili kufanikisha malengo yao haya ambayo matokeo yake hayatamgharibu mwenyekiti huyo pekee yake, au chama anachokiongoza, bali mafanikio yote tuliyopata kidemokrasia kama taifa.

Ni kwa sababu hiyo basi, Mbowe amepewa sifa mbaya kila wakati, akihusishwa na ukabila, ufisadi, udikteta, ubinafsi na kila aina ya sifa mbaya, lengo likiwa ni lile lile la kukivuruga chama hicho na kudumaza nguvu ya kiushindani ya vyama vya upinzani.


Mbinu hiyo haramu ya kutumia vyombo vya habari kumchafua Mbowe iliposhindikana, hata wakati ule ikafikia hatua ya kutumia hoja za aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Chacha Wangwe, mawakala hao wa CCM wakaja na mbinu nyingine mbadala.


Mbinu hii haikuwa nyingine bali ile ya kujaribu kuwagombanisha na kuwachonganisha viongozi wa kitaifa wa chama hicho kwa mbinu na staili tofauti.

Wakati fulani mwaka jana, Zitto alipofanya mahojiano na gazeti hili na kuulizwa kuhusu kusambazwa kwa habari za viongozi wa CHADEMA kugombanishwa, alikiri kulifahamu hili.

Wakati huo (Desemba mwaka 2007), vyombo kadhaa vya habari vilianza kuandika habari za kumpamba Zitto, zikimsifu kwa kuwa mwanasiasa kijana machachari na ambaye uwezo wake wa kiuongozi ulikuwa ukikizidi chama hicho na pengine viongozi wengine wa chama hicho.

Taarifa hizi za vyombo vya habari zilinikutanisha na Zitto na tukazijadili naye kwa muda mrefu kabla ya wote wawili kukubaliana kwamba, zilikuwa na lengo la kukihujumu CHADEMA na kuua dhana nzima ya upinzani hapa nchini.

Tulipofikia hatua ya kukubaliana naye, alifanya mahojiano na gazeti hili na akatoa tamko zito ambalo kwa kiwango kikubwa lilisababisha mawakala wa CCM kuachana na ajenda hiyo. Kwa maneno yake mwenyewe wakati huo akirejea taarifa za vyombo mbalimbali vya habari alisema: '‘Tumegundua kuwapo kwa juhudi za makusudi za kutaka kutugombanisha CHADEMA. Hiki ni chama makini, kimezibaini njama hizo na kwa hakika hakiwezi kusambaratishwa.

"...CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu mimi… mimi si maarufu kuliko chama. CHADEMA ni taasisi, ni chama ambacho kina misingi ya uanzishwaji wake.

"…(Wanasema) eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi, si kweli. Niligombea ubunge nikitokea shule, sikuwa najulikana. Nilikuta ‘grassroots network' ya chama, (chama) hakikujengwa na mimi.

"CHADEMA ilijengwa na uongozi uliokuwepo, nilikuta uongozi 'intact' (imara). Katika kila kijiji kulikuwa na uongozi na hata katika vitongoji vyote. Wakati naingia kugombea ubunge kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wenye kadi wanaofikia 10,800 katika jimbo zima. Hawa sikuwatafuta mimi, niliwakuta na ndio waliofanikisha ushindi wangu.

"...Katika mazingira kama haya utasemaje kuwa mimi ni maarufu kuliko chama wakati chama ndicho kimenipa umaarufu?

"...CHADEMA ni chama ambacho wenyeviti wake wastaafu wanaendelea kuenziwa na kuhudhuria vikao vyote vya chama… ‘institutional memory' ipo kuliko katika vyama vingine vya upinzani.

"...Alipohama (Dk. Aman Walid) Kabourou, wengi walidhani ndiyo mwisho wa CHADEMA Kigoma, lakini leo hii CHADEMA ni moto Kigoma kuliko ilivyokuwa awali."


Ni jambo la ajabu kwamba, karibu miaka miwili tangu Zitto mwenyewe akiri kutambua kuwapo kwa njama hizo za kumkosanisha na viongozi wenzake na pengine kukihujumu chama chao, anaonekana akiingia katika mtego ambao miaka kadhaa iliyopita ulipata kukinasa chama kingine cha NCCR Mageuzi kiasi cha kukifanya leo hii kushindwa kufurukuta hata kufananishwa na baadhi ya watu kuwa ni sawa na shirika lisilo la kiserikali (NGO).

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba, leo inapofikia hatua ya mwanasiasa kijana aliyekuwa akionekana kuwa moja ya mazao ya kuigwa ndani ya kambi ya upinzani tangu kukwama kwa akina James Mbatia, Mabere Marando, Augustine Mrema na wenzao wengine wengi, akifuata mkondo ule ule, basi ni wazi Watanzania wanaweza wakajikuta wakilazimika kukata tamaa zaidi na zaidi.

Ingawa ni kweli kwamba pengine nyuma ya Zitto wako watu wengi ndani ya CHADEMA na nje, waliojitoa mhanga kumuunga mkono katika mapambano haya, mwanasiasa huyo anapaswa kutambua wazi kwamba, uamuzi wake huu wa sasa, unamuandalia anguko ambalo si mimi wala mwingine yeyote atamwepusha nalo.


Ni wazi kwamba katika umri wa miaka 33 aliyonayo Zitto na tena akiwa na akili zinazochemka na afya njema, mwanasiasa huyo mchanga anayo fursa kubwa mbele ya safari ya kuwa mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA na Mungu akipenda kupanda zaidi ya hapo alipo leo.

Anapaswa kujifunza kuwa na subira waliyonayo vijana wengi ndani ya CCM na serikalini, ambao pamoja na kuwa na fursa nyingi za harakaharaka, wameamua kuwa watulivu na wenye subira, wakiwa na uhakika kuwa, wakati wao utafika.

Wakati atakapokuwa akiyatafakari hayo, Zitto anapaswa kuyarejea maneno aliyoyatoa Rais Jakaya Kikwete siku alipoteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM pale Dodoma, Mei mwaka 2005, alipokiri yeye mwenyewe kwamba lilikuwa jambo jema kwake kuukosa urais mwaka 1995.

Naliona anguko la kihistoria la Zitto.
 
Last edited:
Umri hata siku moja hutakuwa mizani ya kuangalia kama mtu anauwezo wa kuongoza ama la. Hii article ni kama propaganda fulani na pengine Kabwe akisoma inaweza kumpa nguvu zaidi katika nia yake ya kugombea uenyekiti wa chama chake. Si haja kwa kweli ya kutoa mifano ya viongozi ambao hili swala la umri lilitolewa kama kisingizio cha kuwafanya "eti hawapo tayari kuongoza", hivi karibuni tu, Obama wa Marekani, Joseph Kabila wa Democatic Republic of Congo na wengine wengi. Wote hawa wanafanya kazi ya uongozi vema kabisa ....

Cha msingi tu ni yeye (Kabwe) kuwa na stratejia ya kupambana na wapinzani wake kwenye hicho kiti na kufanya kampeni maradufu, kama wananchi wa constituency ya Kigoma North walivyompa kura na kumchagua kuwa Mbunge, ndivyo atakavyoweza kuchaguliwa na wanaCHADEMA kuwa mwenyekiti. Godspeed!
 
Last edited by a moderator:
Kibanda kwenye makala hii umekuwa upande mmoja wa Mbowe,unasema kuwa Zitto ni kijana na unakubali amesimamia mambo makubwa ya kisiasa nchini, pia amekuwa naibu Katibu mkuu kwanini ashindwe kusimamia kazi ya uenyekiti wakati Mtendaji mkuu wa chama ni katibu mkuu? Zitto awe na subira kwani hujui kuwa muda uliopo ndio wako na muda ujao si wako? una maana vijana ni taifa la Kesho? JK amekuwa naibu Katibu mkuu wa CCM akiwa na miaka 25.

amekuwa naibu waziri kwenye wizara nzito ya nishati akiwa na miaka 33.kama ZITTO ana SHINE bungeni kwanini ashindwe uenyekiti wa Chadema?
 
Pointless, baseless and meaningless points from pressman Kibanda; kamwe umri sio kitu kinachotazamwa kwa mtu ku-deliver kwa kile alichochaguliwa!

Mbona akina JK na wenzake wana umri mkubwa sana (zaidi ya miaka 60 sasa) wamefanya nini kwa watz zaidi ya kumuita mzee mwenzao Spika Sitta dodoma na kumdhibiti?Chenge ana umri gani? akina Dr Rashid Je wanafanya madudu kwa sababu wana umri mdogo au?

Kibanda,here we go kaka,tz tunataka kiongozi bora bila kujali ana umri gani; Nyerere alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TZ akiwa na miaka 39 na bado anabaki kuwa ndiye Rais Bora kupata kutokea TZ

Zitto kama ukiamua kutumia haki yako ya kidemokrasia wewe gombea wala usijali maneno ya kutumwa ya Kibanda hasa anaposema kuwa "Zitto kaamua kugombea bila kuuliza kama Mbowe atatetea kiti chake" hapo kwa kweli nilicheka sana, hamna kwenye katiba ya CHADEMA inaposema unapotaka kugombea ngazi husika basi lzm umuulize incumbent kama kaamua kutetea kiti chake! Na akisema Yes basi ufikiri cha kufanya au uache kumpinga kwenye sanduku la kura? Hapo sijaelewa Kibanda alikuwa na maana gani!

Tuache demokrasia itawale!
 
Dr Kitila Mkumbo

Mbona sijaona popote kama unachukua fomu; kulikoni MPIGANJI wetu?
 
Aarghhh!!!! Nilidhani ni CUF na CCM peke yao!

Watu wana uchu saana na madaraka. Umri si tatizo bali ni uwezo. Hatuhitaji reference ya nani ni nani, ndio maana mashirika na title kubwa kwenye nchi yetu hadi ukuu wa Mikoa unashikiliwa na wazee. No way. Kipimo cha ukomavu si umri. Zitto anaweza tumuache.

Kwa dhana anayoileta Kibanda ni kwamba vijana hawawezi, na pia ukikuta chama au taasisi imeanzisha hata baada ya kujiunga nayo basi hufai kuiendesha kwa sababu inawenyewe. Mie nadhani tunahitaji uchambuzi ambao ni substance umejaa facts, na si mentor, age etc.
 
Kibanda ametoa maoni yake binafsi, ni mbaya kwa mwandishi wa habari kuwa biased kiasi hiki. Tueche demokrasia ichukue mkondo wake.
 
Tutayasikia mengi. Lakini kila kitu kina sababu zake. Watu wanajaribu kuchimba suluhisho hapo ni kwa Zitto na Mbowe kufunga midomo yao kwenye vyombo vya habari ili mafisadi wasiwemanipulate na waache demokrasia ichukue mkondo wake.
 
*MWENYEWE AMKARIBISHA ULINGONI WAPAMBANE

Na Boniface Meena

NAIBU katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema ana sababu za msingi za kuamua kuuwania uenyekiti wa chama hicho, huku mwenyekiti wake Freeman Mbowe akimkaribisha katika kinyang'anyiro hicho.

Zitto, ambaye yuko nchini Ujerumani kikazi, aliiambia Mwananchi jana kwamba, ameamua kuingia katika kinyang’anyiro cha uenyekiti kupambana na Mbowe kwa lengo la kuandaa chama kuchukua dola.

Lakini Mbowe, ambaye uongozi wake umeifanya Chadema kuwa tishio kwa chama tawala na upinzani, alisema anamkaribisha mwanasiasa huyo kijana katika kuwania nafasi hiyo, akisema uamuzi huo ni haki ya kila mwanachama wa chama hicho kugombea nafasi yoyote kama ana sifa.

"Sina mengi ya kusema; kama alivyosema Dk Slaa (Willibrod) kila mwanachama anaruhusiwa kugombea nafasi yoyote, hivyo sina tatizo na Zitto kuwania nafasi hiyo," alisema Mbowe.

Zitto, ambaye ameibukia kuwa mwanasiasa maarufu mwenye uwezo wa kujenga hoja, alisema anatambua kazi nzuri ambayo Mbowe ameifanya katika chama, lakini akaongeza kuwa, uamuzi wa kupambana naye unalenga kukiandaa chama kuchukua dola katika chaguzi zijazo.

"Ninajua kazi ambayo Mwenyekiti Mbowe kaifanya kwenye chama. Ni kazi kubwa sana na hata mimi kuwepo kwangu katika siasa, Mbowe amechangia sana, alisema Zitto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32.

"(Mbowe) Ni kiongozi ninayemheshimu na kwa kweli anakipenda sana chama na amejitolea sana kwa ajili ya chama."

Hata hivyo, Zitto, ambaye aliwahi kukaririwa akisema nia yake siku moja ni kushika nafasi ya juu ya uongozi katika nchi akimaanisha urais, alisema ni lazima chama kionekane sasa kipo tayari kuchukua dola.

"Mbowe ni kiongozi mzuri sana wa chama ambacho kipo katika siasa za upinzani. Watanzania sasa ni lazima wapewe sera mbadala za kuonyesha kuwa tunaweza kutawala. Jambo la msingi kuliko vyote ni kuona chama kinabaki kimoja na imara. Hili ndilo lengo langu," alisema.

Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini ambaye alijiunga na Chadema akiwa na umri wa miaka 16, alisema ingawa katika uongozi wa Mbowe amekuwa na mafanikio, chama hicho kimekuwa katika hali ya kufukuza wanachama.

"Tumefukuza sana wanachama. Haiwezekani tukajenga chama cha kufukuzana tu. Ni lazima tukubali kutokubaliana," alisema.

"Kugombea kwangu ni wito wa kurejesha umoja katika chama wakati tunajiandaa kuchukua dola. Uchaguzi Mkuu wa 2010 utakuwa wa kihistoria kwa kuwa kwa uzoefu wangu unaweza kulazimisha serikali kuundwa na waziri mkuu ambaye hatoki CCM. Hatuwezi kwenda huko tukiwa divided (tumegawanyika)."

Akielezea mafanikio ya Mbowe, Zitto alisema mwenyekiti huyo ameiwezesha Chadema kutoka kupata asilimia tatu ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2000 mpaka asilimia 8 mwaka 2005.

"Tunamshukuru kwa kukiimarisha chama chetu. Sasa ni wakati wa chama kuelekea kushika dola. Lazima kukiandaa chama kushika dola," alisema Zitto.

"Hiyo ndio kazi ambayo nimeombwa kuifanya na wana-Chadema mikoani na wilayani. Hii ndio kazi ambayo kwa moyo mzito nimekubali kuifanya."

Mbowe, 48, hakutaka kuzungumzia kwa jina uamuzi wa naibu katibu wake kugombea nafasi ya uenyekiti ambayo imekuwa ikipata mbadala bila ya upinzani mkali.

Mbowe ni mwenyekiti wa tatu wa chama hicho akifuwafuatia waziri wa zamani wa fedha, gavana na muasisi wa Chadema, Edwin Mtei; na baadaye naibu gavana wa zamani, Bob Makani. Wenyeviti hao waliachia madaraka kwa hiari yao.

Wakati uamuzi huo ukiashiria mpambano mkali baina ya wawili hao, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu amechukua fomu kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti.

Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, katika nafasi hiyo, Profesa Baregu anachuana na Maulida Anna Komu na Mbunge wa Mpanda Kati, Said Amour Arfi.

Alisema hadi jana, ambayo ilikuwa siku ya mwisho ya kurudisha fomu hizo, watu 33 walikuwa wamejitokeza kuwania uongozi katika Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), 33 Baraza la Vijana (Bavicha) na 13 Baraza la Wazee.

"Kikao cha wazee wa chama kitakaa Agosti 29 mwaka huu kupitia fomu za wagombea," alisema Dk Slaa.

Kwa mujibu wa Dk Slaa ili kutaka haki itendeke chama kimeamua kusimamisha uchaguzi wa ngazi ya mkoa katika Mikoa ya Mara na Mbeya kutokana na harufu ya rushwa, huku ikisimamisha chaguzi za Arusha na Manyara kwa sababu mikoa hiyo inaendelea kujikongoja.

Katika tukio jingine, Dk Slaa jana alimkabidhi kadi ya uanachama wa Chadema aliyekuwa katibu wa itikadi na uenezi wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Selasini alisema, ameamua kufanya hivyo ili kuendeleza mapambano ya kisiasa kupitia chama hicho ambacho alisema kimeonekana kuwa na nia ya dhati kuwafikia wananchi.

Alisema kuhamia kwake Chadema kutampa fursa ya kuwania ubunge wa jimbo la Rombo kama chama kitampitisha ili aweze kupambana na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Basil Mramba.


Chanzo:
http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=14150
 
kibanda ndiyo aina ya waandishi tuliyonao, nisingeshanga kama angekuwa anafanya kazi uhuru publishers lakini freemedia, ni aibu.
endelea Zitto, CHADEMA siyo CCM, mambo ya vijana ni taifa la kesho ni mambo ya CCM na ndiyo yameifikisha Tanzania hapa ilipo leo hii. tunahitaji mtazamo na msukumo mpya na katika hili uwezo ndiyo suala la kujadili si umri. kama umri ni hoja pengine Obama angemuachia mama Hilary lakini kwa vile alijijua kuwa ana uwezo aliendelea na leo ni raisi wa marekani.
Isitoshe katika siasa ni muhimu kujua wakati sahihi wa kugombea nafasi, nao ni pale wakati jina lako lipo juu na huu ni wakati wa Zitto si wa Mbowe. Mtazame Salim Ahmed Salim, hakusoma alama za nyakati wakati alipotaka Urais, ukweli wakati wake ulikuwa ni 1995 pale mwalimu alipomtaka aondoke OAU kuja kuchukua nafasi ya Mwinyi, alikataa ili amalizie muda wake OAU, nini kilimkuta alipojaribu mwaka 2005 alipopambana na mtandao wa mafisadi...historia imeandika. Go ahead Zitto this is your time man.
 
naungana kabisa na Bw Kibanda. Zito ingawa katiba inakuruhusu pasi na shaka lakini wewe bado kabisa kukomaa kisiasa anahitaji takriban miaka mitano zaidi ya kujijenga kisiasa kabla ya kuamua kugombea uongozi wa juu kabisa wa chama.

Zito kama kweli unataka uongozi wa juu kabisa katika siasa unahitaji upate uzoefu zaidi. uwe na subra.
lakini ukiangalia kwa upande mwingine inaweza ikawa ni ujanja wa kisiasa wa chadema kuonyesha kuwa Mbowe nae kapata mpinzani.
 
Naungana mkono na Kibanda,Zitto anapaswa kuwa mtulivu na mvumilivu,uamuzi wake unaweza kuwapa CCM nguvu zaidi.

Hivyo wakati huu si muafaka kwa malumbano ndani ya Chadema ni wakati wa kuwa pamoja na kuangalia njia za kukabilia na CCM mwakani..

Its true Kibanda, Zitto anaweza kujikuta kwenye anguko kuu....afikirie mara mbili si kila mtu maarufu anaweza kuwa MWENYEKITI wa Chadema...Zitto bado ni mchanga anahitaji kugain experience zaidi...
 
ZITO kaka...............HONGERA

Kibanda anajaribu kupotosha maana ya demokrasia, sipendi kusema kama hilo linafanyika kwa maslahi. Ni imani yangu kuwa kuna sababu za msingi sana zimfanyazo Zito kupanda jukwaani kujiuza dhidi ya "mentor" wake.

Nionavyo mimi:
Zito anapaswa AMA kunyamaza kimyaaaaaaaaa na kusonga mbele kwa kile ambacho tayari anakiamini, amekifanyia maamuzi na pia ana idadi nzuri tu ya wanaomuunga mkono AU kuweka sababu zote hadharani.
Kimsingi, kutoa sababu nusunusu kunaweza amsha changamoto nyingi ambazo si za lazima sana. Kwa mfano, kusema "Mbowe ni kiongozi mzuri sana wa chama ambacho kipo katika siasa za upinzani. Watanzania sasa ni lazima wapewe sera mbadala za kuonyesha kuwa tunaweza kutawala. Jambo la msingi kuliko vyote ni kuona chama kinabaki kimoja na imara. Hili ndilo lengo langu," alisema.(amenukuliwa na Boniface Meena katika gazeti la Mwananchi). Siamini kama hii ndiyo sababu pekee ya kufikia maamuzi hayo, kwani kama alishindwa kukiwekea chama sera hizo akiwa miongoni mwa viongozi wa juu kabisa wa chama, nini kitatushawishi kwamba hilo lawezekana akipata uenyekiti????? Je ni kutupa picha ya awali kwamba atakuwa dikteta kwa kuamua vyote anavyoviamini ni sahihi??
 
kuishi kwingi ni kuona mengi, UMRI NI KIGEZO
 
KIBANDA KWELI NJAA ITAKUUA!! Yaani uko radhi kuchafua professionalism yako kwa sababu ya kumfurahisha Mbowe!! Sasa naamini yale maneno ya mdau mmoja hapa (simkumbuki jina) kuwa wamiliki wa vyombo vya habari ndo wana influence nini kiandikwe katika vyombo hivyo!! Wakati ule Mengi na Rostam walipokuwa wanatumia vyombo vyao kukidhi matakwa yao, wengi walihamaki, sasa kazi imeamia Tanzania Daima.

Kibanda sipingi kuandika makala kutoa mtizamo wako, la hasha, ila ni namna ulivyojenga hoja zako. Ulivyoandika makala hata mtoto wa darasa la pili atagundua ulivyohamaki na kuonesha woga juu ya uamuzi wa zitto kugombea uenyekiti wa chadema!! Woga wa nini?

Kibanda kifupi umekurupuka kuandika makala dhaifu na isiyo na mashiko hata tone, umeonesha namna gani usivyoweza kuyazuia mapenzi yako binafsi kwa Freeman Mbowe.

Kibanda unatofauti gani na Yusufu Makamba anayewapigia magoti kina Lowassa na kuwazuia viongozi wa CCM mkoa wa Tabora kuhudhuria mapokezi ya spika Sitta???

Zitto endelea kufanya na kusimamia kile unachofikiri na kuamini ni sahihi!!

Shame on you A. Kibanda!!
 
Msiogope wana Chadema na wapenda demokrasia nchini. Hii ndiyo Demokrasia sahihi. CHadema wanataka kuionyesha CCM kuwa mambo ya kumzuia mtu asigombee wakati katiba haisemi hivyo, ni kudumaza demokrasia.Zitto anaposema anataka kukijenga chama kuelekea kushika dola hana maana kuwa MBowe hawezi ila ana maanisha kuwa dola haiwezi kushikwa sawasawa kama chama hakina demokrasia ya kweli - yaani CCM haifai kushika dola kwani haina demokrasia ya kweli. Pia anapozungumzia kuwa na sera mbadala haina maana kuwa yeye binafsi ndiye mwenye sera mbadala bali Chama kwa ujumla.

Juu ya suala la kufukuzana, hapa anawasema waziwazi CCM ambao mwenye mawazo mbadala anatishiwa kufukuzwa - Angalia walivyomtishia Sitta
 
Watoto wa Mungu;
Maoni yangu ni kuwa kama Mbowe ni kiongozi mzuri, na Zitto pia kiongozi mzuri katika level ileile, what is the problem km Zitto naye akichukua nafasi hiyo? Kianachohitajika hapa ni kiongozi mzuri na mwenye uwezo wa kukipeleka mbele chama, na si jina la mtu. Mi nadhani Zitto angepata hiyo experience, halafu Mbowe agombee Urais, 2010 au Dr. Slaa. Wakipata au hata wasipopata, next election 2015 Zitto naye agombee urais tena, ili naye apate experience hiyo. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo inaweza ikakifanya chama kama hiki kuweza kujenga viongozi wenye nguvu wa kuweza kukikabili vizuri chama chochote kinachokishilia dola!Hivyo napingana 100% na hoja ya mwandishi wa makala!
 
Wanachama wengine wa Chadema wakigombea mnawapata uchafu kwenye magazeti; wasipogombea mnalalamika Chadema haina Demokrasia.!!

Huwezi kuwa na demokrasia kwenye chama bila ya kuwa na wagombea wazee na vijana walio tayari kugombea uongozi.


Ipi ni kazi ngumu, kuwa mwenyekiti wa chama au kuwa Mbunge.??!!

Wacha Zitto amwage sera zake, wanachama waamue.
 
Kama kuna watu wasio na busara hapa Duniani mmoja wao ni Huyu Kibanda katika Makala yake hii, kwa jinsi kibanda alivyoandika ni wazi kuwa haitakiii mema chadema, nani asiyejua kuwa Gazeti la Tanzania daima ni mali ya Mbowe family? ni bora atumie style nyingine ya kumpigia debe Mbowe na sio style hii uchwara ambayo hata mtoto wa miaka mitano hadanganyiki..

Comperatively sometimes CCM tunawaonea...
 
Go Zitto,go Zitto, goooo Zittoo,gooooooooo,..

Huyu mwandishi hatufai hata kwa lumangia.

Nyakati hizi si za kuanza biashara ya umri katika uongozi.

Ninaimani hata hapo anapofanyia kazi ana majungu sana na unafiki mkubwa pale kijana anapoonekana kushine kiutendaji.

Anatakiwa aanze yeye kung'ka hapo kwenye kiti chake na kuwaachia vijana wachape kazi,siyo kuanza kuandika utumbo utumbo kama huu, anghraaaaaaa

Inatia aibu eti mhariri mtendaji, kweli mtendaji ama mpotoshaji,....???????

Beba form Zitto na simama kidete katika hilo, wacha demokrasia itawale.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom