Kibanda amemuudhi nani?

Kibanda amemuudhi nani?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Ilisemekana kuwa Dr.Stephen Ulimboka aliudhi watawala wa juu.Akatekwa,akateswa,akatupwa na siku ya pili akaokotwa Msitu wa Mabwepande. Sinema yake bado haijaisha.

Leo,'ametekwa' na kuteswa Ndugu yangu kiuandishi Absalom Kibanda. Sasa ameshatua Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kukosekana huduma stahiki Muhimbili na hospitali nyinginezo za Dar es Salaam.Naye ana majeraha kichwani na jichoni.Ameumizwa vibaya na yuko katika hali mbaya.

Absalom Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima linalosemekana kumilikiwa na CHADEMA(sina uhakika wa umiliki).Baadaye,akajiunga na New Habari Corporation kama Mhariri Mtendaji.New Habari Corporation inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na Rostam Aziz.

Ni juzi tu,Kibanda aliandika makala ya kumsifu Abdurahman Kinana akichagiza kuteuliwa kwa Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama cha Mapinduzi. Nimjuavyo Kibanda,ni mwandishi nguli na mahiri. Ni msema anachokiamini.

Kitendo cha kushambuliwa leo kinaacha maswali mengi. Kibanda amemuudhi nani tena? Kwanini sasa tabia ya kuteka na kutesa inaonekana kama ni dawa ya kuwakomesha wasemakweli?

Uchunguzi wa kina unahitajika hapa;tena haraka. Amasivyo,kila mtu atajilinda kwa namna anayoiona inafaa. Serikali ifanye kazi yake ya kuhakikisha ulinzi wa raia wake.
 
Siungi mkono suala la kuumizwa kwake.......namtakia mema juu ya afya yake!!!

Ila na nyie waandishi mna maisha yenu nyuma ya pazia na haswa linapokuja suala la siasa na uchaguzi.....!!!!!!!

Mnafungamana na viongozi na wanasisa........mnasikia na kuona mengi saana.....mengine mnatujulisha na mengine mnamezea......kwa faida ya nani.....nyie mnajua zaidi yetu....!!!!!!

Maisha yenu mnatakiwa muyachunge sana na kwa tahadhari ya hali ya juu...............just out of curiosity hivi waandishi wa habari "mahiri" mnachukua tahadhari gani juu ya maisha yenu...........deterrent mechanism ipi mnatumia kuhakiki usalama wenu?????

It is high time muangalie upya suala zima la kuwa na uwezo wa kujihami na kushambulia kama ikibidi haswa nyie investigating journalists.......

Wish him a fast recovery.......
 
Wamiliki wa gazeti la Tanzania Daima wachunguzwe.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
mh..pole zake!!!

ayo mengine siyajui...
 
Siungi mkono suala la kuumizwa kwake.......namtakia mema juu ya afya yake!!!

Ila na nyie waandishi mna maisha yenu nyuma ya pazia na haswa linapokuja suala la siasa na uchaguzi.....!!!!!!!

Mnafungamana na viongozi na wanasisa........mnasikia na kuona mengi saana.....mengine mnatujulisha na mengine mnamezea......kwa faida ya nani.....nyie mnajua zaidi yetu....!!!!!!

Maisha yenu mnatakiwa muyachunge sana na kwa tahadhari ya hali ya juu...............just out of curiosity hivi waandishi wa habari "mahiri" mnachukua tahadhari gani juu ya maisha yenu...........deterrent mechanism ipi mnatumia kuhakiki usalama wenu?????

It is high time muangalie upya suala zima la kuwa na uwezo wa kujihami na kushambulia kama ikibidi haswa nyie investigating journalists.......

Wish him a fast recovery.......
Umenena vyema mkuu
 
Haya mambo ukichunguza sana utagundua mengi ya kuogofya, hii nchi bwana..!
 
Undumilakuwili umemponza ... Aka njaa kali
 
Siungi mkono suala la kuumizwa kwake.......namtakia mema juu ya afya yake!!!

Ila na nyie waandishi mna maisha yenu nyuma ya pazia na haswa linapokuja suala la siasa na uchaguzi.....!!!!!!!

Mnafungamana na viongozi na wanasisa........mnasikia na kuona mengi saana.....mengine mnatujulisha na mengine mnamezea......kwa faida ya nani.....nyie mnajua zaidi yetu....!!!!!!

Maisha yenu mnatakiwa muyachunge sana na kwa tahadhari ya hali ya juu...............just out of curiosity hivi waandishi wa habari "mahiri" mnachukua tahadhari gani juu ya maisha yenu...........deterrent mechanism ipi mnatumia kuhakiki usalama wenu?????

It is high time muangalie upya suala zima la kuwa na uwezo wa kujihami na kushambulia kama ikibidi haswa nyie investigating journalists.......

Wish him a fast recovery.......

nakubaliana na wewe kabisa kuna kila haja ya hawa waandishi kujihami.
 
Amemuudhi yuleyule aliyeudhiwa na Ulimboka, Kubenea, Mwandosya, Mwakyembe, Jwani Mwaikusa, Mwangosi na wengineo wa namna yake.
 
Undumila kuwili itakuwa ndio sababu kuu kutekwa kwake na kupigwa!Pole sana Kibanda!
 
Mbona kama unataka kutuaminisha kitu fulani hivi? Tukio hili si la kwanza na katika yote yaliyopita hakuna anayejua nini chanzo chake. Haina haja ya kuunganisha matukio kwani hata yaliyo wazi kabisa hayajawahi kutolewa maelezo na vyombo husika
 
Ilisemekana kuwa Dr.Stephen Ulimboka aliudhi watawala wa juu.Akatekwa,akateswa,akatupwa na siku ya pili akaokotwa Msitu wa Mabwepande. Sinema yake bado haijaisha.

Leo,'ametekwa' na kuteswa Ndugu yangu kiuandishi Absalom Kibanda. Sasa ameshatua Afrika Kusini kwa matibabu zaidi baada ya kukosekana huduma stahiki Muhimbili na hospitali nyinginezo za Dar es Salaam.Naye ana majeraha kichwani na jichoni.Ameumizwa vibaya na yuko katika hali mbaya.

Absalom Kibanda alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima linalosemekana kumilikiwa na CHADEMA(sina uhakika wa umiliki).Baadaye,akajiunga na New Habari Corporation kama Mhariri Mtendaji.New Habari Corporation inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na Rostam Aziz.

Ni juzi tu,Kibanda aliandika makala ya kumsifu Abdurahman Kinana akichagiza kuteuliwa kwa Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama cha Mapinduzi. Nimjuavyo Kibanda,ni mwandishi nguli na mahiri. Ni msema anachokiamini.

Kitendo cha kushambuliwa leo kinaacha maswali mengi. Kibanda amemuudhi nani tena? Kwanini sasa tabia ya kuteka na kutesa inaonekana kama ni dawa ya kuwakomesha wasemakweli?

Uchunguzi wa kina unahitajika hapa;tena haraka. Amasivyo,kila mtu atajilinda kwa namna anayoiona inafaa. Serikali ifanye kazi yake ya kuhakikisha ulinzi wa raia wake.

Ukweli gani kausema Kibanda? au propoganda zake ndo unasema ukweli?
 
Kibaya zaidi wametumia strategy zilezile zilizotumika kwa Ulimboka wamejua wakitumia hizo hawatafikiriwa wao watafikiriwa walewale waliofanya kwa Ulimboka. Poor Him. get well soon. Ila mimi nafikiri Huyo mwandishi anajua zaidi na ndiye wa kusema ukweli.

Kitu kingine kinachonipa maswali. baada ya kusikia taarifa ya habari kuwa Mlinzi alipoona amevamiwa akaanza kuhangaika kuwaita majirani tema baada ya wavamizi kuondoka. Kwa nini alisubiri wavamizi waondoke ndio awaite majirani?

- Pia hiyo nyumba yake iko peke yake haijapakana na nyumba nyingine ambazo zina walinzi ambao wangeweza kuto msaada?

- Hivi alikuwa anaishi peke yake yeye na mlinzi tu? hakuna watu wengine kwenye nyumba alilokuwa anaishi?
nimejiuliza maswali hayo nimekosa majibu na pia nikahisi huenda pia Mlinzi alikuwa anajua au pia alikula njama na wavamizi. maana pia inaonekana alichelewa kufungua mlango makusudi ili tendo lifanyike. ni mawazo yangu tu. Unajua hali iliivyo sasa nchini kwenye inatufanya vichwa vyetu kila linapotoke tatizo na majibu yasipatikana tunakuwa tunawaza vibaya.

Mungu tusamehe waja wako.
 
Hali hii kwa waandishi wa habari mpaka Lini?

Si Mara ya kwanza kuona waandishi wahabari Wakikumbwa na misukosuko yakupigwa na hata kuuwawa, ukweli inatiauchungu sana.

Nalazimika kuandika haya wenye kuchukia nawachukie na wenye kuona kuna haja ya mamlaka husika sasa kuchukua hatua stahiki kuhakikisha hali hii inakomeshwa wataungana nami.

Kwanza ilikuwa kwa Saed Kubenea na Ndimara walivamiwa huku kubenea akimwagiwa Tindikali tena ofisini kwake, baadae ikajakwa mwandishi wa habari Daudi Mwangosiambaye yeye aliuwawa, ikaja kwa mwandishi mwingine huko kanda ya Ziwa na leohii kwa mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Absarom Kibanda, hali hii mpaka lini?

Ni ukweli usipingika kuwa katikakuandika kuna kundi litaguswa kwa mazuri na lingine litagushwa kwa kudhanilinaonewa, lakini hii ndio kazi yetu kuwapashahabari, kukosoa pale palipo na mapungufu, kusifia pale panapopaswakuelimisha na kuhabarisha .
Sasa katika hili wanataka tuandikehabari gani? Tuzipike habari? Tunahitajiuhuru wa habari jamani , tuwahabarishe watanzania , sasa tuandike nini ikiwa kila tunachoandika ni kibaya? Upo wapiuhuru wa habari? Juzi Kubenea, jana Mwangosi , leo Kibanda Kesho sijui atakuwanani?

Tunaliomba jeshi la polisi kufanya uchunguziwa kina kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Hii inatia uchungu sana na aliyefanya haya ana lengo moja la kudhoofisha fani na utendajiwetu, lakini hawajui kwamba tupo kazini na tunafanya kazi kwa manufaa yawatanzania wote, kama unaona huitaji kuguswa kwa mabaya na kalamu zetu basikuwa muadilifu, tukuandike kwa mazuri , kwa faida ya watanzania wote waliokomijini na wale wasiofikiwa.

‘’ UKATILI ULIOFANYWA KWA KIBANDA UNAPASWA KULAANIWA VIKALI’’

Mungu msaidie Absalom Kibanda aponeharaka arudi katika utendaji wake wa kazi wa kawaida. Daima mbele haturudinyuma.
_________________________________
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom