Kibanda ajitoa kamati ya Nchimbi...

Mi nadhani nchimbi na wenzake wangeomba bunge lipitishe muswada wa wabunge kuvaa kiasili wapendavyo once a week wawapo mjengoni. Kama vile baadhi ya mashirika yalivyoruhusu uvaaji wa casual wear ijumaa. basi bungeni warushu uvaaji wa vazi la asili.
 

Kwa hiyo mkuu kama serikali yetu isingekuwa inanyanyasa waandishi wa habarii fundamentally wewe suala la kamati ya kiserikali kutumiwa katika vazi la taifa kimsingi huna tatizo nalo? Tatizo lako ni hii serikali yetu na unyanyasaji wake wa waandishi, au siyo?
 
Duuu, pamoja na UBOVU WA KIINGEREZA umetufumbua mengine zaidi. Aksante mkuu.
 
Hivyo eeh?

Kibanda uko mfukoni mwa mafisadi,na kule ccm kuna vita vya kumalizana sasa mkono wenye nguvu unamaliza kambi adui na wewe ni mhadhirika mmoja wapo.Vipi bwana kibanda kama husingepelekwa polisi na mahakamani ungekubali kuwa katika kamati hii ya kiupuuzi ya mavazi la taifa?Nchimbi anajua analolifanya ndio maana aliwachaza waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari ili nae atupe karata zake 2015.Wiki iliyopita Jenerali aliandika Raiamwema kuwa waandishi wakiwasaliti wananchi siku waandishi wakipata matatizo wananchi watafurahia wakisema tulikuwa tukiwambia lkn mnadharau
 
Tukizidi kuwaachia waendelee kutula mbele na nyuma tutakwisha. Kama tulivyopanga tuwatoe madarakani, juu ya waandishi mimi nasubiri kuona hao wengine kama watakaa kimya, the likes wa wakina makwaia wa kuhenga, hao waliobaki wote wanaishi kwa kumtegemea nchimbi kwa hiyo hawana la kufanya, kwa wakina Hebby Gunze, TBC, clouds na ndugu zetu ITV hapo wamefika after all hawajaijtwa kwa utashi wao. Sasa kama wangekua ni professionals nao wangejitoa ama kumu advise waziri kwa kuwa kibanda ni mwenyekiti wa wahariri, basi hata wahariri wangetakuwa kutoa statements za ku support. Mawaziri wa Tanzania bwana, nasikia huyu bwana siku ya kujadili ombi la mkenya sholei kupewa kibali cha kufanya kazi ama la aliacha bunge dodoma na kuja dar kuhudhuria kamjadala hako, yaani hakuwa na imani na PS wake na watu wengine kufanya maamuzi hayo, watu wa usalama walishangaa jinsi huyu bwana alivyo wa bei ya kutupa, eti ndio wanaotaka urais wa 2015 anauza taifa kwa kulambishwa viunga, hivi ni kweli Tanzania hii hakukuwa na mtu wa kuendesha kakampuni ka mwananchi ni mpaka waziri aje kusimamia swala hilo? halafu kaja kwa gari la serikali na mafuta ya kodi za watanzania kumtetea sholei ale katika nafasi ya mtanzania.
 
Hili vazi la wapi watanzania tunamchora tu huyu mwenye Phd ya kufoji? mashindano yalishafanywa na washindi wakajazwa tele kwenye media hivi mpaka leo wanasubiri next step toka serikalini, sasa hili vazi la nchi gani? hivi kama tanzania tumeshindw akujitangaza nje kupitia maajabu ya dunia kama the highest peak of Africa, wonders za Serengeti, Olduvai gouge na sasa Arusha kulikogundulika fuvu na nyayo za watu wa mwanzo kabisa, madini ya Tanzanite inayopatikana Tanzania peke yake, tutaweza kwa urojo wa vazi la Tanzania ambalo waziri anataka libuniwe na marafiki zake wasio na fani wala uwezo huo. Hivi kweli small education ni kazi kuna mtu anamuona Joseph kusaga ni wa utamaduni sababu ana TV na radio ya vijana? amesha chair nini ama hivyo vikao vya birthday ya JK? Hongera waziri kwa kutuleta kwenye viwango vyako vya chini, sisi wengine hatujawahi kuweko huko ndio maana tunashangaa na kuzidi kujiuliza huyu JK ana source hivi vituko vya mawaziri toka soko gani? shift ama third hand? kwa nini wakati kuna premium market ya watendaji hapa nchini? jamani watanzania wenzangu msikate tamaa shikilieni hapo mlipo hawa watu wanaondoka tuchukue na kuendesha nchi yetu kama watu
 
Mimi nataka kuwa na vazi la Taifa na tuko Watanzania wengi tunataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…