R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,578
| |
[TD="bgcolor: #ffffff"]
| MWENYEKITI wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba amesema mwanasheria wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anatapatapa kutokana na kutaka jukwaa hilo lifutwe kwa sababu linajishughulisha na siasa kinyume cha sheria. Kauli hiyo imekuja baada ya Mwanasheria wa CCM, Godwin Kunambi kudai kuwa jukwaa hilo limevunja sheria ya mwaka 2002 kifungu cha 20 kinachokataza asasi za kiraia kujihusisha na masuala ya siasa. Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Kibamba alisema hakushangazwa na kauli hiyo kwa sababu imetolewa kwa makusudi, ili kuupotosha umma wa wapenda demokrasia nchini. Kibamba alisema anapingana na kauli ya mwanasheria huyo wa CCM kuwa jukwaa hilo limejiunga na muungano wa vyama vya siasa. Alisema kilichofanywa na jukwaa hilo ni kuunga mkono umoja wa vyama vya siasa vilivyoko ndani ya Bunge kupinga kuburuzwa na CCM katika upitishwaji wa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba. |
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
[/TD]