Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Miaka ya nyuma nikiwa kwenye miji ya warusi jamaa mmoja alitaka kuniibia fedha kutoka kwenye mfuko wangu wa koti la baridi, nilimshtukia na akaona aibu kwani alikuwa ni mtu mzima sana kulinganisha na mimi, waliokuwa wamesimama pembeni yangu kwenye usafiri walimtazama na wakanitazama mimi halafu mambo yakaisha. Nikajiuliza kimoyomoyo ikiwa huyu mtu angenifanyia hivi nikiwa ndani ya mabasi ya Dar halafu nikampigia kelele za mwizi, iwapo angeweza kubaki salama.
Kibaka anayeiba taa ya gari barabarani huitiwa kelele za mwizi, wanaoweza kumzunguka mara nyingi hawamuachi salama.
Mwizi anayeiba laptop wakati foleni za gari hazitembei, na yeye ole wake akamatwe baada ya watu kupiga kelele maarufu za mwizi huyo mwizi huyo.
Umekuwa ni utamaduni wetu sisi waafrika kupinga kwa nguvu zote tabia ya mtu kuishi kwa kuiba, ndio maana mwizi anaanikwa hadharani na jamii iweze kumuadhibu.
Adhabu wanazopewa wezi mara nyingi husababisha vifo vyao, ingawa watu wa haki za binadamu wanapinga hii tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi.
Mtu mwenye cheo fulani anayeiba fedha za umma anayo bahati kwamba haonekani mbele ya macho ya watu wakati akiwaongezea machungu ya maisha yao. Lakini huyu naye anastahili adhabu ile ile ya kupigiwa kelele za mwizi huyo mwizi huyo.
Kwanini tuwe na double standards katika kushughulika na aina mbili za wezi, ambao kwa maadili ya kiafrika tunafundishwa kupinga kwa nguvu zote tendo zima la wizi?.
Madhara ya wizi mkubwa yanachangia katika kuwakatisha tamaa vijana wa kiume ambao wanaamua kung'oa taa za magari, wale wa kike wanaishia maeneo kama corner bar na sehemu nyingine ambazo wanalazimika kufanya mapenzi na mtu wasiyefahamu historia yake kiafya kwa ujira mdogo, ambao unadhalilisha utu wao.
Wezi wakubwa hatuwezi kuwapiga mawe na kuwachoma moto lakini angalau tunayo haki ya kuwafahamu, na kufahamu mienendo yote ya kesi zinazowahusu kuanzia siku wizi wao unapogundulika mpaka siku wanapohukumiwa vifungo.