Kibadeni afichua hujuma Simba, Brandts ashangaa

Joined
May 28, 2013
Posts
91
Reaction score
17
Kibadeni afichua hujuma Simba,
Brandts ashangaa
_________________________________________________

KOCHA wa Simba Abdallah Kibadeni amelaumu
kuwa kuna hujuma imefanyika kwa wachezaji
wake, wakati Mholanzi wa Yanga, Ernest Brandts
amesema wachezaji wake hawako kiprofesheno. Kibadeni aliweka wazi kuwa Yanga isingeweza
kuwafunga mechi hiyo lakini kwa sababu kuna
watu wamevamia kambi yake na kuwadanganya
wachezaji wakacheza chini ya kiwango. “Nawajua wachezaji wangu, kiwango kile si chao,
hawakutaka kucheza ndiyo maana tulifungwa
mabao yale matatu kipindi cha kwanza. Kuna watu
wanakuja kambini na kuwapandikiza maneno
wachezaji na hao waliopandikizwa maneno
hawakucheza vile inavyopaswa kipindi cha kwanza wakaruhusu mabao matatu ya haraka
haraka,”alisema Kibadeni katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam jana Jumapili. “Tulivyokwenda mapumziko, nilizungumza nao na
nikawaambia, mmeshawapa mabao matatu
yanatosha, sasa chezeni mpira,”alisema Kibadeni
ambaye alienda mbali na kuwazungumzia kiungo,
Abdulhalim Humoud ‘Gaucho’ na winga, Haruni
Chanongo ambao aliwatoa na kuwaingia, Said Ndemla na William ‘Gallas’. “Siwezi kuwataja kwa majina, watajijua na
kujichuja wenyewe. Yule Humoud nilimpanga kwa
makusudi kama mlivyoona ndiyo maana
nilimtoa,”alisema Kibadeni ambaye wiki iliyopita
alikuwa akilalamika kwamba kuna wachezaji ndani
ya Simba ambao wanamtengenezea majungu kwavile anawaambia ukweli na hawataki kufuata
utaratibu wa kambi yake.

Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernest Brandts alisema:
“Tulistahili kushinda na ninachowalaumu
wachezaji wangu hawako kiprofesheno kwa
sababu baada ya kushinda mabao 3-0 kwenye
mapumziko waliingia wanashangilia wakati mechi
inaendelea. Nilishangaa sana. “Wakati wa mapumziko walivyoingia kwenye
vyumbani walikuwa wanashangilia kama
wameshinda mchezo, mpaka nikashangaa, sare
wameitaka wenyewe, tulipata nafasi nyingi na
tukashindwa kuzitumia. Timu nzima ilikuwa na
upungufu, Luhende na Chuji walifanya makosa mawili yakatugharimu,”alisisitiza Brandts. Na alipoulizwa kama kuna hujuma, Brandts alisema
inawezekana. “Haiwezekani tuongoze mabao
matatu na baadaye warudishe yote, haiwezekani
wachezaji wametuhujumu na kinachotakiwa
tuwachomoe baadhi yao,”alisikika shabiki mmoja
maarufu.
 
Huyo shabiki wa Yanga asijekuwa Steve wakulialia maana hajambo.
 
Rubbish from both couchers. Hivi hata wazungu nao wana porojo?

Kibadeni siwezi kumshangaa maana ni mmatumbi mwenzetu.
 
Chanongo kwa kiwango alichoonyesha jana si chake, huenda labda hakuwa vizuri au ana mahaba na Yanga au labda kweli waliambiwa wacheze chini ya kiwango kama anavyosema kocha, Jana Chanongo hakucheza vizuri.
 
Haya mambo ya simba na yanga ni majanga tu nchi hii soka haiwezi kuendelea kwa staili hii na wanaoharibu ni hawa hawa viongozi wetu
 
It's what it's....

Hayo maneno ya Kibadeni ni kutaka kujikosha tu kwa kuhofia dhahma ya wanachama...

Hivi kwani ni mara ya kwanza kwa Simba kufungwa na Yanga au kutoa nao suluhu??

Anaacha kuwapongeza wachezaji wake kwa kupigana na walau kuambulia pointi moja...

Lakini anaibuka na kubwabwaja kama gari la mkaa linalopanda mlima wa Kibamba Darajani...

Hao Yanga aliokuwa akicheza nao walikuwa wamekatwa miguu kwamba washindwe kuwafunga...!!!

Ujinga mtupu
 
Chanongo kwa kiwango alichoonyesha jana si chake, huenda labda hakuwa vizuri au ana mahaba na Yanga au labda kweli waliambiwa wacheze chini ya kiwango kama anavyosema kocha, Jana Chanongo hakucheza vizuri.
Chanongo amelewa sifa
 
kwanza aliruhusuje watu kuingia kambini?
It's what it's....

Hayo maneno ya Kibadeni ni kutaka kujikosha tu kwa kuhofia dhahma ya wanachama...

Hivi kwani ni mara ya kwanza kwa Simba kufungwa na Yanga au kutoa nao suluhu??

Anaacha kuwapongeza wachezaji wake kwa kupigana na walau kuambulia pointi moja...

Lakini anaibuka na kubwabwaja kama gari la mkaa linalopanda mlima wa Kibamba Darajani...

Hao Yanga aliokuwa akicheza nao walikuwa wamekatwa miguu kwamba washindwe kuwafunga...!!!

Ujinga mtupu
 
Kibadeni naye haachi uswahili,kweli tumbili ni yuleyule kabadilisha msitu tu,hata huyo muthungu tayari kawa mdaku,nimeamini mpira wa bongo ni majanga
 
Mie naona Kocha wa yanga katoa sababu ya Kimsingi. Wachezaji wake walikosa professionalism. Muda wa game ni dakika tisini, wao wana relux kwa sababu tu wamefunga mwanzoni. Lakini Kocha huyo ana makosa ilibidi awajenge psychologically kwamba mchezo haujaisha mpaka dk ya mwisho. Hivyo asiwatupitie lawama kuwa hawana professionalism maana ni kazi yake ku- instil hiyo professionalism kwa wachezaji na ndio maana analipwa.

Kibadeni sielewi anacho sema. Mpira unachezwa uwanjani kama tulivyoona. Maswala ya hujuma ni huko huko klabuni maana hayana nafasi katika sheria za mpira. Aongelee perfomance ndani ya uwanja, otherwise kama alijua kuna hujuma kwa nini awapange wachezaji walionunuliwa?
 
hivi watanzania tumerogwa?watu mnaacha kutafuta sababu za kiufundi zilizowagharimu mnaanza kumgafuta mchawi....damn u
 
Kibaden uwezo wake wa kufikiria na kufundisha ndiyo umeisha hapo!
wasipo mbadilisha hawatafika popote, kocha mzima huwezi kutoa lawama za kipuuzi kama hizo
 
haya, story za kiswahili zinaanzia hapo!
Haya ndio mambo yanayofanya mpira wetu uendelee kuporomoka kila kukicha, wanaoona mbele zaidi wanasema hizi timu mbili zikifa ndipo tunaweza kuepuka hadithi za kiswahili kama hizi. Mbona hawajasema lolote walivyocheza na Mbeya City!?
 
Mie naona Kocha wa yanga katoa sababu ya Kimsingi. Wachezaji wake walikosa professionalism. Muda wa game ni dakika tisini, wao wana relux kwa sababu tu wamefunga mwanzoni. Lakini Kocha huyo ana makosa ilibidi awajenge psychologically kwamba mchezo haujaisha mpaka dk ya mwisho. Hivyo asiwatupitie lawama kuwa hawana professionalism maana ni kazi yake ku- instil hiyo professionalism kwa wachezaji na ndio maana analipwa.

Kibadeni sielewi anacho sema. Mpira unachezwa uwanjani kama tulivyoona. Maswala ya hujuma ni huko huko klabuni maana hayana nafasi katika sheria za mpira. Aongelee perfomance ndani ya uwanja, otherwise kama alijua kuna hujuma kwa nini awapange wachezaji walionunuliwa?
akili ya mchezaji wa bongo hata ulete mapsychologists wa Bacelona au Arsenal huenda wasisaidie chochote. Ndio maana utasikia 'wafadhili' wakisema kuwa "ukifunga goli milioni moja" ...hiyo ndio soccer industry ya bongo, ombeeni tu Mbeya city, Azam waendelee kuimarika ili watuondoe kwenye hizi nonsenses!

Kama Kibadeni alitamka hayo it is very sad. Wajenge vijana, acha kuwananga. Kucheza chini ya kiwango ni jambo la kawaida katika mpira. Wachezaji wahimizwe kuacha kuwasikiliza wachumia tumbo wacheze mpira.
 
MBYCITY HOYEE! AZAM OYEE! wakti mnajadili mechi ya jana na eti wengne kila kona dar na tz nzima wanashanglia droo, wamesahau kuwa vinara wa ligi ni azam na mbycity. Naanza mapenzi na timu zinazo kua kisoka!
 
Hutachelewa kuzisahau hizo timu zako unazotaka kushabikia sahivi, msingi uliojengwa kwenye timu za Simba na Yanga huwezi kuubomoa kirahisi rahisi namna hiyo. Kwa watanzania walio wengi ukitaja Simba na Yanga hiyo ni habari nyingine kabisa timu ziko kwenye mioyo yao.
 
Mkuu Masuke, hoja yako inaelekea kuwa na mashiko lakini usisahau kuwa mtaji mkubwa wa Simba na Yanga inasemekana ni sawa na mtaji wa chama fulani cha siasa ...yaani umasikini na ujinga! Wengi wanasema hivi vitu viwili vikipungua vitaendana na kupungua kwa supporters wa hizi timu kama ilivyo kwa hicho chama cha siasa.

Similar Discussions

Back
Top Bottom