Sina hakika kama simba imetibu tatizo kwa kuwatimua King Kibadeni na Julio,inawezekana wanamchango wa tatizo lakini je aina ya wachezaji wetu wa Simba nayo siyo tatizo jingine?Ninachokiona hapa na kwamba sisi Simba tunatishwa na kivuli cha Yanga na kwa hali hii tarehe 14th Dec mechi ya mtani jembe kati yetu na Yanga itakuwa ishu kubwa.Safari hii malkia wa nyuki hayupo,huyo mzungu sijui nani atajitokeza kuokoa jahazi kwa kumlipa mishahara yake.Hadi leo Patrick Lewing yupo hapa bongo anaidai Simba,haijamalizza madeni imeleta mzungu mwingine ambaye naye atafukuzwa tu wala hana muda.Afadhali timu wangemkabidhi tu Matola amalizie mzunguko wa pili,
Nimechoshwa na ubabaishaji wa viongozi wetu Simba.Kimoja ambacho kamati ya utendaji imekifanya kwa usahihi na ninawapongeza ni kutuondolea mwanasiasa katika timu.akajiandae na uchaguzi mkuu ujao kwani huko nako kama anababaisha kama alivyokuwa akifanya Msimbazi basi amekwisha