Kiashiria cha pesa kupotea: BOT yashusha zaidi deposit ratio toka 9% hadi 7% kwa mabenki kunusuru ukata mifukoni

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Hiki ni kiashiria hakuna fedha na wanachokifanya na kupunguza kiasi cha fedha za mabenki walizoweka kama dhamana ili kiasi hicho kiende kwenye mzunguko ikimaanisha fedha hakuna mifukoni
IMG-20180824-WA0037.jpg
 
Too late!

Capacity ya hawa watu ni kufanya siasa za hovyo hovyo kama ku..unua wapinzani feki na sio kusimamia issue za msingi kama uchumi!!

Unavuruga uchumi wa maelefu ya watu alafu unategemea eti Mtatiro,Waitara au Kafulila akihamia kwenye chama chako ndio wewe na chama chako mtakubalika kwa wananchi.Hii sijui ni akili ya wapi!!

Nadhani Kuna Ph Dada inabidi zihakikiwe!!
 
Namba hazindanganyi! Na hapo tayari benki kama nane hivi zimejifia. Lakini ni sawa ndio uchumi unapaa hivyo. Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, uongozi unahitaji busara, hekima, weledi,maono na utulivu wa kimawazo. Misifa misifa tu na maamuzi kukurupuka havijawahi kumwacha mtu salama.
 
Sikuona sababu ya kumcopy mkuu wa TRA!
TRA na BOT wanatakiwa wafanye kazi in concert.

Kwenye habari za kodi za miamala kupandatulipata aibu sana,TRAna BOT walipishana lugha, mmoja anasema kodimpya italipwana makampuni ya simu, mwingine akasemaitalipwa na mwananchi.

Kwahiyoni muhimuwawasiliane vizuri, kama kuna maswali wanyooshe kablahaijawa dhahma kubwa.
 
Wanakumbuka shuka kunakucha, Haya ndo mambo walitakiwa kuyafanya mapema sana toka mwanzo!.

Ile move ya kuondoa pesa za serikali kutoka kwenye mabenki ya biashara ilifanywa emotionally zaidi kuliko rationally!, Serikali haikujua kuwa ina wajibu na faida kwa nchi kuwa na Mabenki imara na wakati huohuo kuwa na mzunguuko reasonable wa fedha nchini!

Ondoa huyo Waziri mpango, mipango yake imetufikisha hapa
 
Back
Top Bottom