Kiapo cha wajumbe wa bunge maalumu la katiba ni batili kisheria

Seif al Islam

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
2,156
638
kwa wanaofatilia kwa karibu kikao cha bunge maalumu kinachoendelea sasa watakuwa wamebaini upungufu na ubatli mkubwa katika kiapo kinachotolewa na wajumbe wa bunge maalumu la katiba ambacho kimeainishwa katika kifungu cha 9(2) a cha kanuni za bunge kinachosomeka, “mimi.............niliyeteuliwa kuwa mjumbe wa bunge maalum, naapa/nathibitisha kwamba nitakuwa mwaminifu na mtiifu kwa jamhuri ya muungano wa tanzania na kwa kadri ya uwezo na ufahamu wangu, nitatimiza wajibu wangu na kufanya kazi zinazonihusu bila ya upendeleo. ewe mwenye mungu nisaidie” ubatili wenyewe upo katika maeneo mawili makubwa.kwanza ni kwa kiapo chenyewe kushindwa kuweka bayana na kuainisha utofauti wa wajumbe walioteuliwa na rais kwa mujibu wa kifungu cha 22(1) c cha sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012 sura ya 83 yaani wajumbe wanaotokana na makundi na taasisi mbalimbali na wale wajumbe wanaotokana na bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania yaani waliotokana na kifungu cha 22(1)a na wale wa baraza la wawakilishi kutoka zanzibar yaani wa kifungu22(1)b.kama kinavyosomeka hapo juu hakitofautishi aina hizi mbili za wajumbe.hili ni tatizo linaloweza kutwisha kwa kwanza kamati ya kanuni ya akina lissu ,jussa na dr tulia na wajumbe wote wa bunge maalumu. udhaifu mwingine na unaosikitisha zaidi ni jinsi wajumbe wengine wanavyojiongezea maneno mengine yasiyokuwepo kwenye kiapo kama vile kama kilivyoainishwa katika kanuni ya 9(2) ya kanuni za bunge maalumu kwa kuweka maneno kama “ee mwenyenzi mungu katika kristo yesu”, “mwenyenzi mungu mweza wa yote” na mengine mengi yasiyokuwepo katika kanuni za bunge zinazoonyesha kiapo.kisheria viapo hivyo ni batili na walioviapa hawawezi kutenda lolote halali ikiwa viapo vyao ni batili.ni alama nyingine ya kukosa umakini katika mambo muhimu.inasikitisha sana! kwa kutambua udhaifu huu wa kiapo, ni wajumbe wachache niliowashuhudia wakitoa kiapo wakitofautisha wajumbe walioteuliwa na rais na wale walioupata ujumbe kwa mujibu wa mamlaka ya bunge na hao ni tundu lissu na jussa ambao ni wajumbe wa kamati ya kanuni.leo ni siku ya kwanza kanuni hizi zilizobishaniwa kwa karibu wiki mbili zinaanza kutumika na kukanyagwa bila woga.tusubiri tuone ni kwa jinsi gani kanuni hiziz zitafuatwa baada ya kuanza kwa kuminywa hii leo.nawasilisha
 
Hata baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wakati wa kuapa Wabunge kulikuwa na vituko hivi hivi na nilianzisha mada juu ya hilo!
Mwenzetu Barak Obama ilibidi arudie kiapo baada ya kumisplace maneno ya kiapo!
Huku kwetu ni kanyaga twende ili mradi maneno yote yapo! Hata mtu akiongezea maneno kwetu hiyo sio taabu hata kidogo, ili mradi watu wawahi tujisenti twa 300,000/-!
 
Back
Top Bottom