Kiama:Serikali kurudisha katika umiliki wake Mashamba na Makampuni yaliyobinafsishwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,711
149,960
Serikali inakusudia kurudisha katika umiliki wake Mashamba na Makampuni yaliiyowahi kubinafsishwa kwa watu ambao wamekiuka mikataba ya ubinafsishaji.

Msajili wa Hazina,Lawrence Mafuru jana alitoa orodha ya makampuni 514 yaliyobinafsishwa na kuyataka yawasilishe serikalini taarifa za utekelezaji wa mikataba yao.Makampuni mengi yanatajwa kuvunja mikataba hiyo kwa kubadili matumizi ya viwanda/mashamba hayo,kutoyaendeleza n.k

Miongoni mwa makampuni,taasisi na mashamba yaliyobinafsishwa ni pamoja na New Savoy Hotel,Kunduchi Beach Hotel,Hotel 77,New Mwanza Hotel,New Safari Hotel na Embassy Hotel.

Kwa taarifa zaidi soma: www.ippmedia.com

Uzuri,kama habari inavyoeleza, hapa kuna wanasiasa ambao waliwatumia majina ya watu binafs (surrogate) kumilikia makampuni /mashamba haya na sasa nafurahi nao wataisoma namba.

Lakini mh.Raisi, mbona serikali yako iko kimya kabisa kuhusu mikataba ya ubinafsishaji wa nyumba za serikali?!
 
Last edited:
Nashauri serikali ianze kuwa serious na VETA pamoja na SIDO,taasisi hizi mbili zikitumika vizuri zinaweza kuwa injini ya mapinduzi ya viwanda hapa Tanzania. VETA itumike ktk kuchochea mapinduzi ya teknolojia wakati SIDO iwe kwaajili ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati. Tukizitafutia taasisi au makampuni ya nje kwaajili ya kuanzisha ushirikiano ili wabadilishane uzoefu na utaalam tutafika mbali sana,Hivyo viwanda vitakavyorejeshwa ktk umiliki wa serikali viwe chini ya SIDO.
 
Back
Top Bottom