Kiama cha mafisadi wa epa chakaribia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiama cha mafisadi wa epa chakaribia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Oct 5, 2008.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Date::10/4/2008
  Hatima ya mafisadi wa EPA yakaribia ukingoni
  Na Ramadhan Semtawa

  HATIMAYE siku za kubaini mbivu na mbichi kwa kujulikana hatma ya mafisadi walioza zaidi ya sh 133 bilioni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), zimewadia.


  Awali ilikuwa ni miezi tangu Rais Jakaya Kikwete, kutangazia umma katika hotuba yake kupitia bunge hapo mwishoni mwa mwezi Agosti na kueleza kurejesha zaidi ya sh 53 bilioni, sasa zimebaki siku.


  Maswali mawili makubwa yaliyopo katika 'mwezi huu wa EPA' ni kama Timu ya Rais itaweza kurejesha fedha zote zikiwemo sh 42.6 bilioni, ambazo zimeibwa na makampuni tisa ambayo taarifa zake nyingi ziko nje ya nchi na kiasi kingine katika sh 90.3 bilioni.


  Swali la pili, baada ya makampuni na watuhumiwa kurejesha fedha hatua gani za kijania zitachukuliwa kwani tayari wanaharakati wametaka watuhumiwa wafikishwe mahakamani kwa makosa ya jinai, huku serikali ikiwa imewatega mafisadi hao.


  Ufisadi wa EPA umegawanyika katika makundi mawili, ambayo ni wizi wa sh 90.3 bilioni zilizoibwa na makampuni 13 yaliyotumia nyaraka za kughushi na sh 42.6 bilioni zilizoibwa na makampuni tisa, ambayo uhalali wa malipo yake ndiyo wenye shaka.


  Lakini, ukweli wa yote hayo unatarajiwa kujulikana katika kipindi cha siku 26 ambacho ni hapo Oktoba 31, kama ambavyo Rais alionya ambao hawatakuwa wamerejesha fedha katika kipindi hicho, Novemba mosi wawe mahakamani.


  Hata hivyo, akizungumzia kwa kifupi uchunguzi huo unaondelea, Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali (IGP) Said Mwema, alionya kwamba hakuna fisadi wa EPA atakayepona.


  IGP Mwema akisisitiza, alisema jeshi la siyo kweli kwamba uchunguzi huo amechiwa Rais, bali unaendelea kwa umakini.


  "Uchunguzi bado unaendelea, ripoti kamili itatoka Novemba mosi, hatuja mwachia Rais jukumu hili bado liko mikononi mwetu tunalifanyia kazi," alionya IGP Mwema.


  Onyo hilo la Mwema liko nyuma ya onyo la Amiri Jeshi Mkuu, ambaye katika hotuba hiyo alionya kwamba, ifikapo Novemba mosi wote watakaokuwa hawajaresha fedha walizoiba EPA, watafikishwa mahakamani Novemba mosi.


  Rais akisisitiza hilo kwamba, watuhumiwa wa EPA wako katika hali mbaya ingawa wanapita mitaani na 'kupiga' tai shingoni, alisema hatakuwa na huruma na wote watakaokiuka hilo.


  Onyo hilo la Rais linalotiwa nguvu na kauli ya IGP Mwema, linazidi kuweka Watanzania mkao wa kusubiri kuona utekelezaji kivitendo kwa watuhumiwa hao.


  Hadi sasa Watanzania walio wengi, wnaonekana kukatishwa tamaa na hatua za serikali katika kushughulikia tuhuma hizo za ufisadi, ingawa imekuwa ikipongezwa na wafadhili wakiwemo Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).


  Lakini, jambo kubwa ambalo hadi sasa linatia shaka katika fedha hizo, pia ni wapi zilipo kwani BoT haina akaunti hiyo, ingawa serikali yenyewe inasema zipo katika akaunti maalumu.


  Uamuzi wa Rais kuongeza muda wa uchunguzi, kutoka miezi sita hadi Oktoba 31,umezingatia zaidi upatikanaji wa taarifa zinazohusu ufisadi wa sh 42.6 bilioni, ambazo sehemu kubwa ya makampuni yake yako nje na kutegemea taarifa za Polisi wa Kimataifa (Interpol).


  Miongoni mwa makampuni ya nje yanayotajwa kuwa wadai halali lakini wakalipwa mengine ni Maruben na Toyota, ambayo taarifa za uhusiano wao kibiashara na waliolipwa fedha za EPA zikiwa ngumu kuzipata.


  Deni la EPA hadi mwaka 1999 lilifikia dola 623 milioni, ambazo kati ya hizo dola 325 milioni zilikuwa ni deni la msingi na dola 298 ni riba na kisha baadaye deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni.


  Hata hivyo, chini ya Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme) wa mwaka 1994 kati ya serikali na Benki ya Dunia (WB), waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya fedha wanazodai, wapo waliokubali na wengine kukataa na kuongeza hadi mwaka 2004 taarifa zinaonyesha jumla ya dola 228 zililipwa chini ya mpango huo.


  Mpango huo baadaye ulileta matatizo ambayo yalibainika katika Ukaguzi wa Hesabu za BoT za mwaka 2005/06, ambao ulifanyika Agosti mwaka 2005, ambao ulionyesha matatizo katika ulipaji wa madeni kwa utaratibu huo wa idhini ya kulipwa wakala wa mdai katika akaunti ya EPA.


  Kukatokea kutoelewana kati ya BoT na Mkaguzi Deloitte and Touche, aliyegundua tatizo hilo, ndipo serikali iliingilia kati na Desemba 4, 2006, ilimuagiza CAG kuhakikisha ukaguzi huo unafanyika kwa kina.


  Mwaka 1985, EPA ilihamishiwa moja kwa moja BoT, na ndipo mwaka juzi kulipoibuka utata wa tuhuma za ufisadi katika akaunti hiyo kwa mahesabu ya mwaka 2005/06.


  Januari mosi, Rais aliunda timu ya uchunguzi wa ufiasdi huo wa zaidi ya sh 133 bilioni, kumtimua kazi aliyekuwa Gavana marehemu Dk Daud Ballali, hata hivyo timu hiyo ilikabidhi ripoti yake Agosti 18 na Rais kuongeza muda hadi Oktoba 31.
   
 2. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2008
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Keep dreaming (vigaravyo si zahabu shaba pia hughilibu)
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Siasa za bongo usanii ndo unatawala na lack of seriousness and committment ya viongozi wetu
   
 4. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  i thought kuna jipya kumbe ndo yaleyale ya kila siku, usanii mwingi sana kwenye siasa za bongo
   
 5. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Raisi Kikwete alisema:

  "tumekubaliana kwamba itakapofika tarehe 31 Oktoba,2008 mwisho ambaye hakulipa mpaka tarehe 1 Novemba, 2008 awe amefikishwa Mahakamani ili Mahakama itusaidie kupata fedha za watu."

  Huyu mwandishi anataka kuonyesha kana kwamba kuna uwezekano wa mashitaka ya jinai dhidi ya wezi wa EPA. Aidha ni kilaza ambae haelewi kinachoendelea nchini na hatoelewa hata kikimgonga usoni, au, anajua vyema kwamba yatakuwa ni mashitaka ya madeni ila anadhani mbinu ya kutia tia presha ni kujifanya kwamba unategemea hatua kali zaidi ya madai. Sasa hii mbinu kwanza ni ku present uongo kwa wananchi, kana kwamba Raisi na Polisi ya Mwema imeahidi mashitaka ya jinai.

  Pili, hiki kitu kama ni mbinu ya mwandishi kuiwekea presha serikali, inakuonyesha kwamba haelewi kwamba Raisi alichoamua na kutangaza Bungeni sio rahisi kikabadilishwa na powerless minions kama kina Mwema na Hosea. Huwezi kumuwekea presha Mwema, Hosea na Raisi kwa kujifanya eti hutambui kwamba wameshaamua kwamba hakuna kesi za jinai hapa. Crummy press ya bongo isichoelewa ni nini hasa ?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  nimesoma habari hii sijaona hicho kiama kipo wapo!!!!!
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Same old sh*t!
   
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  True 100%, Kichwa cha habari kikuuuuubwa ndani mhhh...
   
 9. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hakuna kitu...sh*t
   
 10. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umemkamata mwizi, ushaidi wa kutosha upo, lakini ndiyo kwanza unamtandikia kapeti jekundu na kumbembeleza huyo mwizi. Hapa hakuna story zaidi ya usanii tupu.

  Jakaya na serikali yake inabidi wakubali kwamba Pesa za EPA zilitumika kuwapeleka madarakani kwani hawakuwa na pesa kipindi kile cha uchaguzi na hivi sasa wanatafuta pesa ili walipe deni hilo na riba. Bila shaka wananchi wataelewa na watasamehe, lakini vinginevyo Mmmmmmm
   
 11. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa mfano ikitokea tarehe 1 November wakipelekwa mahakamani mtabadili kauli? Mi naona jambo jema ni kwamba kabla ya kuwa wakali zaidi tumpe tena hizi wiki tatu. hata mimi sina imani sana, lakini tukumbuke pia kwamba patient hapa jamiiforum haipo kabisa.
   
Loading...