Kiama Cha Kweli Kutokea Oktoba 21 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiama Cha Kweli Kutokea Oktoba 21

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 26, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kiama hakikutokea jumamosi mei 21 kwakuwa Mungu aliwaonea huruma watu wake lakini oktoba 21 mwaka huu kiama kitatokea kweli na kuua watu wote ambapo watu wema watapaishwa mbinguni kuonana na Yesu.
  Baada ya kujichimbia hoteli akiwakimbia watu waliokuwa wakitafuta ukweli kwanini kiama hakikutokea mei 21 kama ilivyotangazwa, Mchungaji Harold Camping amejitokeza na kusema kuwa kiama cha kweli kitakuwa oktoba 21 na dunia yetu hii itaangamizwa miezi mitano baadae.

  Mchungaji Camping mwenye umri wa miaka 89 alijitokeza toka machimboni na kutangaza kwenye radio yake ya Family Radio kuwa walikosea mahesabu ya biblia wakati wa kutabiri mwisho wa dunia.

  Lakini Camping aliongeza kuwa kiama cha kweli kitatokea mnamo oktoba 21 mwaka huu.

  Mchungaji huyo wa California alisema kuwa kutotokea kwa kiama mei 21 kumetokana sana na nguvu za kiroho na wala si nguvu za asili.

  Camping aliongeza kuwa Mungu aliwaonea huruma watu kuwaangamiza kwa matetemeko makubwa ya ardhi lakini hiyo oktoba 21 hakutakuwa na huruma ya Mungu na kiama kitatokea kweli.

  Akiongea kwa muda wa lisaa limoja na nusu, mchungaji Camping alisema "Hakutakuwa na sababu za kiroho ifikapo oktoba 21, dunia itaangamizwa na itatoweka ndani ya muda mchache".
   
 2. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kiama cha uongo,kiama cha ukweli aaagggrrr.....psychosis
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Huyo mchungaji angechukuliwa hatua za kisheria kwa kuidanganya dunia!
   
 4. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Siyo makosa yake uchungaji na hisabati wapi na wapi??ivi hata kwenda kwa mungu kwahitaji uwe unajua hesabu??duh kama ndo ivo basi vilaza wote ni mali ya shetani.
   
Loading...