Siyo kweli kwamba Mungu atatustukiza tu kiyama ili tupotee

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
792
1,007
Watu wengi wanatafsiri maandiko vibaya na kupotea kwa kuelewa vibaya ; ni kweli imeandikwa kuwa ile siku na ile saa hakuna anaeijua ila MUNGU Mwenyewe lakini hiyo haimaanishi wiki , wala mwezi , wala mwaka wala muongo wala karne. Tunaweza tukajua kabisa kwamba kiama kimekaribia ila hatutaijua tu siku.

Mbona hata kifo cha mtu binafsi Mwenyezi Mungu humpa mtu mhusika na wanaomzungula dalili kwamba mtu huyo karibu anafariki.

Kama ni wagonjwa huanza kuaga ama kutoa wosia, lakini kuna wagonjwa wengine hawajisikii kutoa wosia hata kama wamezidiwa vipi na utashangaa wanapona baadae, wazee wengi wakikiona kifo kimekaribia huwa nao wanajua na kuanza kufanya mambo yanayoashiria kuaga wanaobaki, kwa hiyo ni kawaida MUNGU kutuonyesha mwisho wetu iwe ni mtu mmoja mmoja ama dunia nzima japo hakuambii ni siku ipi hasa.

Ndio maana maandiko yanaongelea " SIKU ZA MWISHO" , Ni MUNGU anaetueleza dalili zote za siku za mwisho, ina maana haji tu kutushtukiza na ile siku ya kiama ili wote tupotelee motoni milele, tunaweza kujua kama vile mtu anapoona karibu anakufa anavyojua, tunaweza kuzijua siku kuwa zimekwisha sasa.

Tazama hiyo volcano uone picha ya ziwa la moto wa milele itakavyokuwa. Mungu anatumia mifano kutupa picha wanadamu maana muda umeisha tumeambiwa maneno hatuelewi, sasa anatumia model kutueleweaha lakini wapi, watu hawanahabari ndio wanajiselfie pale na kuondoka zao, hakuna kitu wanasemse kabisa. Lakini matukio hayo sio insignificant kabisa, yana logic yake mwenyezi Mungu anapoyaruhusu.

UFU 3​

Ujumbe wa Sardi

1 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika;
Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.

2Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu. 3Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako. 4Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili. 5Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake. 6Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ujumbe kwa Filadelfia
7 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika;
Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. 8Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu. 9Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda. 10Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. 11Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako. 12Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. 13Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ujumbe kwa Laodikia
14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika;
Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. 15Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
 
Kilaa nafsi itaonjaa umautii..

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo sio kule kufa , ile ni sehemu ndogo sana ya hicho kinachoitwa mauti,
Mauti inafuatia baada ya kufa, yaani kwa kule kumuasi Mwenyezi Mungu mtu akatengwa na Mwenyezi Mungu milele katika adhabu ya ziwa la moto.

Wote lazima kufa ila baada ya kufa ndio kutakuja kutofautiana na ndio panahitajika mazingatio. Na kile ni kifo cha roho ya mtu, kwahiyo kifo cha mwili wote tutakufa lakini kifo cha roho kinafuata kwa waliomuasi Mwenyezi Mungu peke yao. Wengine roho zao hazitaonja mauti hiyo ya milele, wao ni peponi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi wanatafsiri maandiko vibaya na kupotea kwa kuelewa vibaya ; ni kweli imeandikwa kuwa ile siku na ile saa hakuna anaeijua ila MUNGU Mwenyewe lakini hiyo haimaanishi wiki , wala mwezi , wala mwaka wala muongo wala karne. Tunaweza tukajua kabisa kwamba kiama kimekaribia ila hatutaijua tu siku. Mbona hata kifo cha mtu binafsi Mwenyezi Mungu humpa mtu mhusika na wanaomzungula dalili kwamba mtu huyo karibu anafariki. Kama ni wagonjwa huanza kuaga ama kutoa wosia, lakini kuna wagonjwa wengine hawajisikii kutoa wosia hata kama wamezidiwa vipi na utashangaa wanapona baadae, wazee wengi wakikiona kifo kimekaribia huwa nao wanajua na kuanza kufanya mambo yanayoashiria kuaga wanaobaki , kwa hiyo ni kawaida MUNGU kutuonyesha mwisho wetu iwe ni mtu mmoja mmoja ama dunia nzima japo hakuambii ni siku ipi hasa.
Ndio maana maandiko yanaongelea " SIKU ZA MWISHO" , Ni MUNGU anaetueleza dalili zote za siku za mwisho, ina maana haji tu kutushtukiza na ile siku ya kiama ili wote tupotelee motoni milele, tunaweza kujua kama vile mtu anapoona karibu anakufa anavyojua, tunaweza kuzijua siku kuwa zimekwisha sasa.
Tazama hiyo volcano uone picha ya ziwa la moto wa milele itakavyokuwa. Mungu anatumia mifano kutupa picha wanadamu maana muda umeisha tumeambiwa maneno hatuelewi, sasa anatumia model kutueleweaha lakini wapi , watu hawanahabari ndio wanajiselfie pale na kuondoka zao, hakuna kitu wanasemse kabisa. Lakini matukio hayo sio insignificant kabisa, yana logic yake mwenyezi Mungu anapoyaruhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Thibitisha Mungu yupo kweli na kwamba habari za kuwapo kwake si hadithi za uongo tu.
 
Thibitisha Mungu yupo kweli na kwamba habari za kuwapo kwake si hadithi za uongo tu.
Maumbile yote yanamthibitisha , maumbile hai na yasiyohai yote yanathibitisha, ukiwemo na wewe mwenyewe unathibitisha hilo.

WARUMI 1: 19-20

wewe si unajua simu hazijiumbi, wala magari hayajiumbi wala nyumba hazijitokezei tu , sasa unafikiriaje kuwamba wanyama wazuri na ndege wa kupendeza na milima inayovutia na mito inayopendeza na nyota na mawingu angani katika kushirikiana huko vinavyoshirikiana miaka na miaka vinaiweka dunia kubaki hai, kwamba nyuma yake hakuna mbunifu aliyefanya kazi yake ?

MWANZO 2: 1-2

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahisi kama mwisho wa dunia ni siku ya kufa ya mtu, kila mmoja na yake.
 
Watu wengi wanatafsiri maandiko vibaya na kupotea kwa kuelewa vibaya ; ni kweli imeandikwa kuwa ile siku na ile saa hakuna anaeijua ila MUNGU Mwenyewe lakini hiyo haimaanishi wiki , wala mwezi , wala mwaka wala muongo wala karne. Tunaweza tukajua kabisa kwamba kiama kimekaribia ila hatutaijua tu siku.

Mbona hata kifo cha mtu binafsi Mwenyezi Mungu humpa mtu mhusika na wanaomzungula dalili kwamba mtu huyo karibu anafariki.

Kama ni wagonjwa huanza kuaga ama kutoa wosia, lakini kuna wagonjwa wengine hawajisikii kutoa wosia hata kama wamezidiwa vipi na utashangaa wanapona baadae, wazee wengi wakikiona kifo kimekaribia huwa nao wanajua na kuanza kufanya mambo yanayoashiria kuaga wanaobaki, kwa hiyo ni kawaida MUNGU kutuonyesha mwisho wetu iwe ni mtu mmoja mmoja ama dunia nzima japo hakuambii ni siku ipi hasa.

Ndio maana maandiko yanaongelea " SIKU ZA MWISHO" , Ni MUNGU anaetueleza dalili zote za siku za mwisho, ina maana haji tu kutushtukiza na ile siku ya kiama ili wote tupotelee motoni milele, tunaweza kujua kama vile mtu anapoona karibu anakufa anavyojua, tunaweza kuzijua siku kuwa zimekwisha sasa.

Tazama hiyo volcano uone picha ya ziwa la moto wa milele itakavyokuwa. Mungu anatumia mifano kutupa picha wanadamu maana muda umeisha tumeambiwa maneno hatuelewi, sasa anatumia model kutueleweaha lakini wapi, watu hawanahabari ndio wanajiselfie pale na kuondoka zao, hakuna kitu wanasemse kabisa. Lakini matukio hayo sio insignificant kabisa, yana logic yake mwenyezi Mungu anapoyaruhusu.

Mungu ameumba vyote kwa kupenda kwake wala hataharibu chochote alichokiumba. Viumbe vipo katika hali isiyo na mwisho ya kubadilika, vingine vinatoweka kwa mtindo huo na vingine vinatokea.

Ziwa la moto ni viumbe vile vinavyokwenda kinyume na mpango wa Mungu. Hivi vinaharibika au kwa maneno mengine vinapata uharibifu.
 
Unaweza ukatengeneza bustani halafu ukamkabidhi mtu fulani awe anakutunzia lakini akafail kuitunza , miiba na magugu vikamea kwa kishikamana na mimea mizuri na kushonana haswa,
Ukija ni lazima ulime na kupalilia vyote pamoja uvichome moto, na ulime upya, aliyekabidhiwa na mwenye bustani nani mwenyemakosa hapo ?
Ni mtunza bustani,

MWANZO 2: 15

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio kule kufa , ile ni sehemu ndogo sana ya hicho kinachoitwa mauti,
Mauti inafuatia baada ya kufa, yaani kwa kule kumuasi Mwenyezi Mungu mtu akatengwa na Mwenyezi Mungu milele katika adhabu ya ziwa la moto.

Wote lazima kufa ila baada ya kufa ndio kutakuja kutofautiana na ndio panahitajika mazingatio. Na kile ni kifo cha roho ya mtu, kwahiyo kifo cha mwili wote tutakufa lakini kifo cha roho kinafuata kwa waliomuasi Mwenyezi Mungu peke yao. Wengine roho zao hazitaonja mauti hiyo ya milele, wao ni peponi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna moto kumbe!!..maana pakihubiriwa roho ovu zitapotezwa wakati zile njema zitakua zikimtukuza mungu huko mbinguni
 
Maumbile yote yanamthibitisha , maumbile hai na yasiyohai yote yanathibitisha, ukiwemo na wewe mwenyewe unathibitisha hilo.

WARUMI 1: 19-20

wewe si unajua simu hazijiumbi, wala magari hayajiumbi wala nyumba hazijitokezei tu , sasa unafikiriaje kuwamba wanyama wazuri na ndege wa kupendeza na milima inayovutia na mito inayopendeza na nyota na mawingu angani katika kushirikiana huko vinavyoshirikiana miaka na miaka vinaiweka dunia kubaki hai, kwamba nyuma yake hakuna mbunifu aliyefanya kazi yake ?

MWANZO 2: 1-2

Sent using Jamii Forums mobile app
Maumbike hayathibitishi Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.

Maumbile yanathibitisha Mungu huyo hayupo.

Angekuwepo, usingekunya wala kukojoa.

Kunya na kukojoa kunatokana na inefficiency in energy processing. Ni waste products.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote asingetengeneza viymbe wenye miili yenye inefficiency.

Pia, miili inakufa. Mungu huyo angekuwapo asingetenganisha viymbe wake wapendanao kwa kifo.

Maumbile yanaonesha Mungu huyo hayupo.

Jaribu tena.
 
Mungu ameumba vyote kwa kupenda kwake wala hataharibu chochote alichokiumba. Viumbe vipo katika hali isiyo na mwisho ya kubadilika, vingine vinatoweka kwa mtindo huo na vingine vinatokea.

Ziwa la moto ni viumbe vile vinavyokwenda kinyume na mpango wa Mungu. Hivi vinaharibika au kwa maneno mengine vinapata uharibifu.
Thibitisha Mungu yupo kweli na kwamba hizi habari za kuwapo kwa Mungu si hadithi za uongo tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom