Khah, First Date iliyonitoa jasho. . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Khah, First Date iliyonitoa jasho. . .

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kongosho, Apr 5, 2012.

 1. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  basi kipindi hicho kabinti nachipukia
  kabyuti byuti ila sio sana.

  Nimeombwa kutolewa out na kijana wa haja
  baada ya kukalkuleti nikawa nishafika bei, nikakubali kutoka naye.

  As usual, kama kwenye avatar yangu kibinti cha half kijijini/half mjini.

  Nikajipigilia kile nilichoona ni kizuri kuliko vyote, hata mwizi angeingia na kubeba sanduku siku hiyo sikuwa na hasara.

  Huyoo, nikaenda dinner.
  Nadhani nilikuwa over excited
  na kama kawaida yangu, I keep it real
  nikaona kweli huyu kuku akatupwe? Roho ikakataa kabisa.
  Kijana akajichanganya, akaenda toilet
  mie huku nikaruka kwa furaha
  Nikamfunga kwenye tissue paper yule kuku nikamtumbukiza pochini

  basi tumepiga stori weee, mara muda wa kuondoka ukafika
  tukatoka nje, wote hatukuwa na magari
  akaniambia nimsubiri pale afuate tax
  kama dakika 5

  siku ya kufa nyani ndo ilikuwa ile
  ile kaondoka niko nje ya hotel namsubiri
  patrol inapita, kulikuwa na wageni wazito kwenye hotel hiyo wa kiserikali sie hatuna habari
  si polisi wakanibeba kuelekea central polisi, uzuri nikamcal fasta nikamwambia anifuate

  kufika pale, pochi hukaguliwa na kuorodheshwa vilivyomo
  wakati bado naandikisha mali zangu ili niingie lock up
  huyu hapa naye kafika
  anashangaa yule kuku wa dinner anatokea kwenye pochi.
  Akauchuna tu, akaongea nao hapo akawaachia kidogo
  tukaondoka.

  Jamani yule kuku alini-embarass hadi uzeeni huwa ananitania sana.
  Eti kuku nilimla akafufukia kwenye pochi.

  Ulishawahi patwa mkasa kwenye first date?
  Hebu tupe mistari yako. . . .
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha! Big mama umetisha.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,221
  Trophy Points: 280
  hahhaahaaaaaaaaaaa loh!
  Mie hoi, kuku kafufufkia kwenye pochi.......
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ha ha ha, yaani nikikumbuka huwa nacheka sana.
  Sijui leo hiki kisa nimekikumbukaje lol

   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  lol...
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hujawahi patwa na mkasa kwenye first date?
  Imagine, mtu hata hujamzoea
  ndo kwanza umeupura vya kutosha

   
 7. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Konnie nakudai mbavu zanguuuuu... Hahahahhaahhahahahaaaaaa......

  Kwamba umekula kuku akatokea pochini?!
   
 8. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  shem mambo...

  (Konnie I am sorry)
   
 9. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umeonaje mambo ya Konnie...
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  wee utakuwa wa mjini
  unaijua fomula ya date.

   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ujana maji ya moto.
  Na busara za uzeeni ni experience tu.

   
 12. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,015
  Likes Received: 3,197
  Trophy Points: 280
  We si mwanaume? Au umejisahau?
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mi bado sijaanza vidate. Nitaleta mkasa wangu. Lol
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Poa shem, hujambo wewe?
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  bg mama mambo yake mazito aisee.
   
 16. queenkami

  queenkami JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  hii kali
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mie hizo ndude nazing'oa kwa vania kalipa.
  Hapa ni true story yangu.

   
 18. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Binti uka-take away kisela ha..ha..ha kazi kweli kweli sijui ulitaka ukanywee chai asubuhi? Kweli sisi wa uswahilini haturembi.Hii ni XXXL.
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kiukweli kilichonisumbua nikashindwa kumla ni Uma na kisu.
  Niliona ataruka juu kama ana mabawa lol

   
 20. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ha..ha..ha nakuelewa sana Kisu na Uma ni changamoto sana,ila siku ukialikwa kwa mchina utajua umuhimu wa kutovunga kuomba maji ya kunawa mikono...afadhali uma na kisu lakini kuna vile vijiti yaani sitaki kuvisikia kabisa vilishawahi kunilaza njaa mimi.Kisa na mimi nionekane hawavumi lakini wamo ilibidi asubuhi ninawe mikono mwenyewe ili kuziba mashimo.
   
Loading...