SnowBall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 3,054
- 2,840
Ahsante sana bro...umenisaidia sana na mimi
Ubarikiwe!!
Ubarikiwe!!
shule yako kiwango gani? huja wahi kuwa monita, au kilanja, au kufanya morning talk shuleni? vipi hujafanya hata ngojera, maigizo primary hadi secondari? au "John Kisomo"?
Wewe hata ukienda TSJ au British Council kwa sasa hautaweza sababu unaumwa unaitaji tiba.
Dawa ya muda mfupi..
1.soma kichekesho nenda kawaambie watu wako wa karibu, wakicheka, una andika point fanya hivyo anagalu mara 10, kwa watu tofauti vichekesho tofauti.!!
2. Tunga story (ukweli/uongo/matukio ya zamani ya shule) kisha simulia, wape mda watu wakuulize, waelewe, wacheke, kama ni kuchekesha au wasikitike kama ni ya kusikitisha. Unaweza zigawa katika makundi, za kufurahisha, na za kusitikitisha (usizitoe siku moja kwa kundi moja).
3. kama ni mwanaume ukiwa njiani kwenda au kurudi kazini, daladala au chombo chochote cha usafiri, hata kwa mguu msemeshe mwanamke (kama mwanamke msemeshe mwanaume) mfanye aongee nawewe, ( she has to pay attention on YOU) kwa sababu ndo unaanza unaweza ukaanza na maswali madogo madogo kama 5, kisha ukafikisha 50 kwa watu tofauti, ambao hujakutana nao kabla.
Tiba ya muda wa kati
1 .Soma hadithi kisha isimulie kwa kifupi bila kupoteza maana, fanya kila mtu avutiwe aweza kutaka kusikiliza!
2. Ongea peke yako ndani na kujirekodi video/audio kisha baada ya muda sikiliza je unaeleweka unavutia mtu kusikiliza? 3. Angalia filamu, chagua "role model" actor jinsi anavyo ongea kisha na wewe jaribu kumugiza....... ( ila za kibongo sikushauri, kidogo za kinegeria na za kimarekani ( hasa kama ofisi yako inatumia ng'eri)
Jaribu hizo kwanza kisha utaniambia.
wakatabahu!!