Keys Hotel

Rafiki yangu aliniambia Keys Hotel ya hapa Dar wanachoma mbuzi safi sana, leo nikaamua kwenda kupata lunch hapo, Nimekuta kweli mbuzi ipo na watu huwa wanakuja kula kwa wingi.
Kilichonishangaza kuna dada poa mchana wote wanawinda, Unakula wanakuangalia mwanzo mwisho, halafu wanaomba soda, sijui kwanini uongozi wa hotel wana waacha wasumbue wateja.

We ukifika pale kula nyama yako ya mbuzi jiendee zako tu..wale wako pale 24 hrs target yao kubwa ni wafanyabiashara wa kutoka Zambia, Malawi, Congo..nk sababu ndio sehemu wanayopenda kufikia..
 
Rafiki yangu aliniambia Keys Hotel ya hapa Dar wanachoma mbuzi safi sana, leo nikaamua kwenda kupata lunch hapo, Nimekuta kweli mbuzi ipo na watu huwa wanakuja kula kwa wingi.
Kilichonishangaza kuna dada poa mchana wote wanawinda, Unakula wanakuangalia mwanzo mwisho, halafu wanaomba soda, sijui kwanini uongozi wa hotel wana waacha wasumbue wateja.

Ulichokiona kiache hapohapo. Si umefwata mbuzi?
 
Iko mitaa gani ili nasi wa kuja tusijekuingia kwenye mtego siku tukitia maguu huko.
 
hawa madada ppoa walikuwa wanawawinda makamanda wa chadema, ndio wateja wao wakubwa
 
Back
Top Bottom