Kessy amwaga wino rasmi Jangwani!!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
IMG-20160509-WA0005.jpg

Beki wa kulia wa Simba SC, Hassan Ramadhani Kessy (katikati) akitia dole gumba kwenye fomu za Mkataba wa Yanga kwa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili kuanzia mwezi ujao.

Zoezi hilo lilifanyika juzi usiku mjini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Kessy, Tippo Athumani na kushoto Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit
 
Hii yanga yenyewe ina import tu haiexport.
Mara nyingi timu bora hufanya hivyo angalia hata huko ulaya timu kama Man u, Man city, chelsea, Real madrid, Barcelona, buyern munich, etc huwa zinaimport wachezaj wazuri ili kuimarisha vikosi vyao na kuwa na vikosi vipana kwa ajil ya mashindando yanayo wakabili na mara chache sana vina export lakin zaid vinawatoa wachezaj kwa mkopo kwenda club zingine...nyie(Mikia fc) endeleen kulea na kukuza kisha wakisha kua na kujitambua wanaenda vilabu vingine vyenye vission na mission
 
Ila kama alishiri kuihujumu simba kwa namna yoyote ile, dhambi hiyo itamtafuna kila anapokwenda!
Huyu Hilo sio la kudhania, amehihujumu ndiyo maana mpaka kufikia kupigwa Na mchezaji mwenzie, wachezaji wanafahamiana. Ila Mimi nimuombee kila Kheri aendako afanikiwe, aishi maisha mapya. Ila atambue Mungu hamfichi mnafiki Leo kaonyesha kile kichodhaniwa na wengi, ila tumuachie Mungu maana Mungu hawezi beba Furaha ya mtu mmoja kwa kuhudhunisha wengi.
 
Huyu mtoto nilimchukia toka alipoipa bao Yanga makusudi na alipolazimisha apewe red card na Toto. Aende tu mamluki huyo.
Haya pateni ninyi Yanga kama utumbo ni kitoweo.

Ova
 
Haya maneno yanaonesha ni kiasi gani ulivyogubikwa na hasira kali na wivu.
Vipi,juzi ndiye aliyewafungisha kwa Mwadui FC?
Halafu Manara sijamsikia kitambo sana,hadi nina mashaka na uwepo wake nchini!

#HuuMchezoHauhitajiHasira
manara yupo. ila mji kamuachia julio atambe, maana toka ameshinda kale ka mechi ka juzi hataki kuondoka mjini.
 
Namtakia kila heri kwani ni ndoto za kila binadamu kwenda anapopaona patamsaidia maisha yake. Bado kijana mdogo ana muda mrefu wa kufanya vizuri. Angalizo langu ni kuwa kama kweli aliifanyia simba hujuma simba ajue kabisa hatadumu miaka mingi katika soka kwani hiyo dhambi ya usaliti itamtafuna tu popote aendapo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom