Kesi za uchaguzi hoi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi za uchaguzi hoi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 16th January 2012 @ 14:59

  KESI nyingi za uchaguzi zilizofunguliwa baada ya uchaguzi mkuu mwaka juzi, hazitasikilizwa na kumalizika kwa wakati, kutokana na ukata unaoikabili Idara ya Mahakama nchini.

  Hadi sasa ni kesi nne tu kati ya 43 ndizo zinaendelea kusikilizwa katika mahakama mbalimbnali nchini kwa kuwa hakuna fungu la fedha za kutosheleza shughuli za Mahakama ikiwa ni pamoja na za uendeshaji kesi hizo.

  Aidha, kukosekana kwa fedha hizo katika Mahakama kumedaiwa pia kusababisha baadhi ya watumishi wake kukosa uadilifu na hivyo kujihusisha na rushwa kwa sababu mishahara inachelewa.

  Jaji Kiongozi Fakih Jundu, jana aliwaambia waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika Mahakama ya Rufani ya Tanzania jijini Dar es Salaam ya kumwapisha Batista Mhelela kuwa Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Sumbawanga na kukiri ukata kutamalaki ndani ya mhimili huo.

  Jaji Jundu alisema Mahakama ina changamoto kuu ambayo ni hali ngumu ya kifedha, jambo linalosababisha kesi za uchaguzi kushindwa kusikilizwa kama sheria inavyotaka na kumalizika katika kipindi cha miezi sita tangu kufunguliwa.

  "Kesi nne tu ndizo zinazosikilizwa sasa na muda tulishaishiwa, tukaomba kuongezwa miezi sita nayo itaisha, kwa sababu bado miezi minne iishe, itabidi turudi bungeni kuomba ufumbuzi," alisema Jaji Jundu.

  Alisema Mahakama iliomba fedha za kuendeshea kesi hizo kiasi cha Sh bilioni 2.3 lakini hadi sasa ni Sh milioni 300 tu ndizo zilizotolewa na ambazo hazitoshelezi kabisa.

  Jaji Kiongozi alisema hali ya Mahakama katika kipindi hiki ni ngumu kifedha ingawa Bunge limepitisha Mahakama ipewe fungu.

  "Sheria imepita, kwamba Mahakama tuwe na fungu, lakini haijafahamika ni kiasi gani zitatolewa kwa mwaka, tunashauri Serikali angalau ingepanga ni asilimia kadhaa ili kuwe na uhakika kama ambavyo alipendekeza Jaji Mkuu mstaafu, angalau ingekuwa asilimia 2," alisema Jaji Kiongozi.

  Jaji Jundu alisema bajeti iliyopita, Serikali iliiahidi Mahakama kuipa Sh bilioni 20 kwa ajili ya shughuli zake zote, lakini hadi sasa ni Sh bilioni 5 tu ndizo zilizoifikia.

  Kesi zingine
  Alisema Mahakama imeshindwa kuendesha kesi nyingine zikiwamo za mauaji kwa sababu ya gharama, ikiwa ni pamoja na kulipa mashahidi.

  "Mahakama inalalamikiwa kila siku, kuwa tunachelewesha kesi, lakini ni kutokana na kukosa fedha ya kuziendesha, tukitembelea magereza malalamiko ni hayo hayo, lakini tukipata fedha hali haitakuwa hiyo, mambo yatakwenda na lawama zitakwisha," alisema Jaji Jundu.

  Akizungumzia rushwa, alisema si watumishi wote wa Mahakama wanajihusisha na vitendo vya rushwa kama inavyoelezwa, lakini wananchi watoe ushirikiano, mtu akiombwa rushwa atoe taarifa mhusika akamatwe, lakini hakuna anayefanya hivyo.

  "Rushwa inayozungumzwa ipo, lakini pia mtu anaweza kuonekana na kitambi au amevaa suti akaonekana mla rushwa, hiyo ni dhana tu, tupeleke malalamiko kunakohusika ili wala rushwa
  wakamatwe," alishauri.

  Ukata na uadilifu
  Alisema ni kweli wapo baadhi ya mahakimu na watumishi wasio waaminifu, lakini pia wapo wengine wengi ambao ni waaminifu, lakini wanaweza kuhukumiwa kwa hisia tu.

  Baada ya kuapishwa, Mhelela alisema changamoto kuu ni mishahara finyu kwa watumishi wa Mahakama inayochochea rushwa kutawala.

  "Kutolipa mishahara vizuri watumishi, inachangia ubadhirifu katika utoaji haki sawa, Serikali ingejipanga kulipa watumishi vizuri na kwa wakati, hali ingekuwa shwari, siku zijazo nashauri kozi zifanyike ili kupata watumishi waadilifu na kutokomeza rushwa," alisema Mhelela.

  Alishauri ajira za watumishi wa Mahakama ziangaliwe upya ili kuhakikisha wanaajiriwa watumishi waaminifu ili kutoa haki inakostahili. Kabla ya uteuzi huo Mhelela alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Ruvuma.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Oh yeah sababu zimebaki miaka 2 uchaguzi mwingine
   
 3. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyie demokrasia ni luxury kwa maskini wa Tanzania! Ukiona hivyo kesi nyingi inaelekea nanbari one waelekea kushindwa kwa hiyo kwa makusudi kada wa CCM AG Werema akaamua kuweka budget ndogo ili majaji wakate tamaa kwa mujibu wa Ndugai posho kibao mara kumi ya wabunge! Kuna haja ya kuachana na hizi by elections kwa hiyo in case akishinda mtu wafanye tu kupishana aliyeshinda anakuwa mbunge bila haja ya kuchota 19billion za walipa kodi kumchagua mnayemjua atashinda. Huu ni zaidi ya uhaini! After all wabunge job description zao ziko vague anybody can fit? Kuna mbunge ana Phd mwingine darasa la saba utapangaje kazi?
   
 4. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Je, kifo cha Regia ndio mwisho wa kesi ya kupinga ushindi wa Mteketa? Sheria inasemaje kuhusiana na hilo, kwani shahidi mkuu sasa hayupo duniani.

  mods - hii sio tanzia so sitegemei mtaiunganisha kwenye uzi usiohusiana na mada tajwa isipokuwa tu kama upo uzi pacha.
   
 5. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sehemu unayotegemea utapata haki kwa wakati na muda stahili, ndio kuna ukata wa kufa mtu, Wazifanye tu kuwa mahakama za kibiashara tujue moja.
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Lazima waendelee na Kesi ya Ms. Mtema sababu sheria zilikiukwa
   
 7. S

  STIDE JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii siri-kali bwana!! Yaani ktk bilioni mbili na zaidi walizoombwa wametoa milioni mia tatu tu!!
  Ktkt bilioni 20 za bajeti wametoa bilioni 5 tu!!
  Lakini pia mbona Mh. Ndugai anasema posho na mishahara ya hawa jamaa ni janga la kitaifa!!? Inamaana hawaridhiki?
  Mimi nashindwa kuelewa hapa wana Jf, hivi kuna idara yoyote ndani ya Tz yetu mambo yanaenda sawa kweli? Ni ipi!!?
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Sheria ipo wazi mlalamikaji Akifa ,kesi inakufa..........

  Minongono iliyopo msibani ni kuwa hata uchaguzi ungefanyika Leo Regia alikuwa anamwacha Abdul Mteketa kwa mbali sana........na walio karibu naye wanasema alikuwa anamuhofia sana Regia.....na hata yeye anakiri kuwa alimpa changamoto .........wale Wenye Imani za kimababu nao wanahisi kamtupia "kitu". Misiba ya kiafrika hili ni jambo la kawaida kuongelewa .


   
 9. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Huo ndio uhalisia wenyewe. Kesi ilikuwa ni kupinga matokeo yaliyompa mheshimiwa ushindi. Bahati mbaya Mungu amemuita na kwa hiyo kesi yake imeshapitwa na matukio maana uchaguzi utarudiwa hata hatma ya kesi itakuwa ni uchaguzi ulikuwa halali
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Lakini Regia hakukata rufaa, aliamua kuachana na suala hili kwa hiyo nadhani kesi haipo mahakamani kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa hapa katika thread fulani zilizohusu msiba wake.
   
Loading...