PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
KESI ZA KUMTUKANA RAIS ZINAONGEZEKA,
KUNA NJIA RAHISI YA KUMALIZA TATIZO :
Jana nimesoma tena kwamba kuna mwanamke Mbeya amefikishwa mahakamani na kunyimwa dhamana - kosa ni kumtukana Rais kwenye mtandao wa Facebook.
Kesi za kumtukana au kumkashifu Rais zipo nyingi tu kwa sasa,
zikihusisha wanasiasa na wananchi wa kawaida.
Kwa nini zaidi katika awamu hii ya uongozi?
Tukiri kuna tatizo mahali.
Mficha maradhi,
Basi kifo humuumbua.
Wala suluhisho SIO kutumia kila njia kutafuta wanaomtukana na kumkashifu ili kuwafungwa jela!
Falsafa zinasema,
ili kumaliza tatizo rekebisha chanzo,
sio ishara au matokeo yake.
Ni vema basi,
Rais wetu na washauri wake,
kujiuliza kwa nini hili jambo linazidi kuwa kubwa.
Inawezekana kabisa ikawa kwamba wananchi wa Tanzania wana hasira na Rais wao kwa kuwa hawamwelewi.
Badala ya kuagiza kamata kamata,
wafikirie namna ya kuboresha mawasiliano na wananchi.
Wakati wa Nyerere,
baada ya vita vya Kagera,
Tanzania ilipitia kipindi kigumu ambacho sidhani kama kitakuja kutokea tena.
Mwalimu Nyerere alikuwa hodari wa kuelewesha wananchi wake,
na hatukuona matukio ya kutukana sio kwa sababu tu hakukuwa na Facebook na WhatsApp
Groups wakati huo.
Watu waliendelea kumpenda Nyerere na hata kuitikia wito wake wa
"tujifunge mikanda miezi 18",
ambayo iliendelea sana tu.
Watu walikosa sukari hadi chumvi,
lakini hukusikia watu wakitukana hovyo kila kona.
Kwa nini kipindi hiki watu watukane kila kukicha?
Ni suala la kujiuliza sana.