Kesi za EPA................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi za EPA................

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 27, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Hukumu ya Maranda na EPA yaiva


  na Happiness Katabazi


  [​IMG] MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imesema Aprili 29 mwaka huu itatoa hukumu ya kesi ya wizi wa sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayomkabili Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda na mpwa wake, Farijala Hussein.
  Jopo la mahakimu wakazi linaloongozwa na Saul Kinemela, Focus Bambikya na Elvin Mugeta, lilisema limefikia uamuzi huo baada ya wakili wa utetezi Majura Magafu kuiambia mahakama hiyo kuwa wamefunga ushahidi wao na Naibu Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface na Ben Lincoln kueleza kazi iliyobaki ni kwa mahakama kutoa hukumu yake.
  Hakimu Kinemela alisema kesi hiyo ilifunguliwa rasmi Novemba 4 mwaka 2008, jopo hilo limeweza kusikiliza ushahidi uliotolewa na pande zote mbili na kwamba hivi sasa wanaenda kuandaa hukumu yake.
  Kwamba kesi hiyo itakuja kutajwa Februari 25 na Aprili 29 mwaka huu, ndiyo jopo hilo litatoa hukumu yake.
  Hiyo ndiyo kesi pekee ambayo imekaribia kufikia hatua ya hukumu kuliko kesi nyingine za EPA zilizofunguliwa mfululizo Novemba 4, mwaka 2008.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Hizi kewsi jamii kamwe haitazielewa kama zinalenga ya kutenda haki kama watendaji wakuu kwenye hayo mabenki hawashitakiwi kwa uzembe na kwa kutowajibika...........................tunataka kuona nyangumi ndiyo wanatinga mahakamani na wala siyo dagaa..............
   
Loading...