Nimetafutiwa chumba hapa Moshi na dalali mara baada ya kukipata chumba nikamlipa dalali pesa ya usumbufu elfu20,kwa sababu nina muamini nikampa pesa ya kodi ya miezi 3 akamlipe mwenye nyumba kabisa kwani nilikuwa nimetoka kwa safari.
Sasa jana nimerudi nataka kuhamia kwenye hicho chumba mama mwenye nyumba akagoma nisiingie mpaka nimpe buku 15 za usumbufu alioupata wakati wa kujenga nyumba,nikamueleza hiyo habari mbona hakuna kabisa!
Amezidi kuwa mkali hadi nitoe hiyo pesa ambayo ni tofauti na ile ya kodi niliyompa,nimemwambia mi nipo chuo sina hela hiyo pia bado hataki na ile ya kodi niliyompa kaitumia hawezi nirudishia,sijui nifanyeji kumpa 15 naona sio haki kabisa na wala sijawahi sikia.
Naombeni busara zenu wadau.