Kesi ya utapeli - Muamala M-Pesa wapokelewa kortini

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,224
1,676
SHAHIDI upande wa mashtaka Koplo Waziri, amewasilisha muamala wa M-Pesa kama ushahidi mahakamani.

Ushahidi huo unawasilishwa katika kesi ya kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu inayomkabili Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Mnec) Wilaya ya Karatu, Daniel Awaki.

Akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha, Nestory Baro, alidai kuwa mshitakiwa Awaki alipokea Shilingi milioni 2.2 mali ya Philemon Mang’ehe, aliyekuwa mnunuzi wa vitunguu.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Eliainenyi Njiro, Koplo Waziri alidai baada ya kuchukua maelezo ya Awaki aliandika barua ya uchunguzi wa mawasiliano ya simu ya mshitakiwa kwenda kampuni ya Vodacom.

Shahidi huyo alidai uchunguzi huo ulilenga kujua mawasiliano ya namba ya simu ya Shaban Mnyaki 0765840584 aliyejitambulisha kama meneja wa shamba la vitunguu la Awaki na kudaiwa kupokea kiasi hicho cha fedha mali ya Philemon Mang’ehe mnunuzi wa vitunguu.

Shahidi huyo alidai baada ya kupata muamala huo ulionyesha jinsi mlalamikaji (Mang’ehe) alivyotuma fedha kwenda kwa Mnyaki Novemba 16, mwaka 2014.

Muamala huo ulionyesha kuwa fedha hizo zilitumwa saa 8:46 alasiri na dakika tatu baada ya kupokelewa Mnyaki alizituma kwenda kwa Haruna Kasimu ambaye shahidi alidai kutomfahamu.

Mapema Mang’ehe alidai kuwa Mnec na Shabani walimtapeli na kujipatia kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo, Wakili Severinus Lawena, anayewatetea Awaki na wenzake, alitaka kujua iwapo muamala huo umewataja wateja wake.

Kwa upande wake, shahidi alidai kuwa taarifa zilizopo mahakamani hapo ambazo zilipokelewa kama kielelezo cha ushahidi namba mbili hazionyeshi fedha hizo kutumwa kwa mtuhumiwa wa kwanza ambaye ni Mnec.

Lakini alipotakiwa kuonyesha iwapo meneja wa sasa wa shamba la vitunguu aliyetajwa kwa jina la Rehema ambaye ni mshtakiwa wa tatu kama alipokea fedha kutoka kwa malalamikaji shahidi alidai kutokuwa na ushahidi wa moja kwa moja.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa tena Aprili 29, mwaka huu.

Chanzo: NIPASHE
 
Hii ni hatua kubwa sana, sasa hata makampuni ya simu ni rahisi kuyafikisha mahakamani kwa upotevu wa miamala ya fedha inayotokea aghalabu
 
Back
Top Bottom