PreGE2025 Kesi ya Uhaini ya Lissu yaahirishwa hadi Julai 01, 2025

PreGE2025 Kesi ya Uhaini ya Lissu yaahirishwa hadi Julai 01, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Blessed Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
221
Reaction score
659

View: https://www.youtube.com/live/oU5eT7Dimu0?si=BYYHRNCBHOz_0_ye

Siku hazikawii kufika, usikilizwaji kesi ya Lissu huo umewadia. Kama mnakumbuka wakayi uliopita upande wa mashtaka walisema wanahitaji muda zaidi kukamilisha upelelezi na wakaambiwa tarehe itakayopangwa kutakuwa hakuna nafasi ya hiki kisinngizio tena.

Je, nini kitatokea leo, upande wa mashtaka watatupa taulo na kuomba kutoendelea na kesi?

Wacha tusubiri kuona nini kitajiri.

====

GtjHLxzaUAAdaTv.jpg
Wananchi, wanachama na viongozi wa Chadema wakiendelea kuwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu




Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche akiingia katika chumba cha mahakama kwa ajili ya kufuatilia mashauri yanayomkabili mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.


Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dkt. Wilbroad Slaa akiingia katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kufuatilia kesi zinazomhusu Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu



Ulinzi umeimarishwa nje mahakama ya Kisutu.


Gari za jeshi la Magereza na Polisi zikiingia katka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam ikiwa ni msafara wa peke yake unaoonekana kumbeba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Lissu ili kuja kufuatilia mashauri yanayomkabili.

Tofauti na siku zingine leo Lissu aliingizwa kwa namna ya tofauti ambapo hata upatikanaji wa picha yake ulikua mgumu huku waandishi wakifanikiwa kuinasa t-shirt pekee(ya no reform no election) iliyozoeleka kuvaliwa na Lissu akiletwa mahakamani.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wananchi tayari wameingia ndani ya ukumbi wa Mahakama. Anasubiriwa Tundu Lissu kupandishwa kizimbani. Hakimu pia aingie na kesi iendelee pale ilipoishia.



Dada wa Tundu Lissu, Mchungaji Rose Lissu ameongoza maombi katika chumba ambacho inafanyikia kesi ya Lissu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam.


Tayari Hakimu ameingia kwenye chumba cha mahakama kabla ya Lissu kuingia ambapo hajapata nafasi ya kuwasalimia waliohudhuria mahakamani hapo na kuishia kutikisa kichwa pekee.

TUNDU LISSU AIOMBA MAHAKAMA KUMRUHUSU KUKABILIANA NA MAWAKILI WA SERIKALI YEYE MWENYEWE BADALA YA MAWAKILI WAKE.

"Leo hii hapa tulipo ni siku ya 68 tangu nilipoletwa mbele ya mahakama yako tukufu na kusomewa mashtaka ya uhaini, siku 68 na toka siku niliposomewa mashtaka ya uhaini, Mh. uliagiza nipelekwe magereza nikawe mfungwa mahabusu na kwa siku 68 hizi nimekuwa mahabusu, kwa wiki moja gereza la Keko na tangu Ijumaa kuu nimekuwa gereza kuu la Ukonga siku 68.

Mawakili wangu hawa wamekuja kunitembelea gerezani ili tushauriane namna ya kukabiliana na mashtaka haya, hawajaacha kuja mahakamani, hawajaacha kuja magereza na muda wote ambao wamekuja katika siku hizi 68 hawajaruhusiwa kuniona na kuwasiliana na mimi. Hawajaruhusiwa kuonana na mimi na kuzungumza na mimi kwa faragha.

Kitu ambacho kimetokea Mh. ukiingia kwenye gereza kuu la ukonga unapopita reception kuna kachumba kulia, hako kachumba kamegawanywa mara mbili, na ukuta wa kioo, unapokuja wanasimama nyuma ya kioo upand wa reception na mimi nasimama upande mwingine wa kioo tunawasiliana kwa simu na mawakili, tunawasiliana kwa simu. Hakuna fursa ya kubadilishana nyaraka na mimi nina manyaraka mengi sana, hakuna fursa ya kuandika chochote kwa sababu hakuna meza hakuna kiti, mnazungumza kwa simu.

Kama mfungwa mwenye mawakili nina haki ya kuonana na mawakili in confidence ni haki, sio mapenzi ya bwana jela ni haki kama ambavyo nitafafanua hapa."

"In fact Mh. Hakimu kuna wakili mmoja alinitembelea hapa nikapiga sana kelele bwana jela akaniambia kama unaona simu haiwezekani akaniambia njoo ukae hapa reception palipojaa maafisa wa magereza, muongee yeye yupo upande wa pili wa lile lilango la green la chuma yupo upande wakili, mimi kipo upande wa gereza tunazungumza maafisa wote wa gereza kama walivyo hapa wananiangalia kila mtu ananisikiliza ninachozungumza.

Na kwenye simu Mh. hiyo simu anaisikiliza nani mwingine, nani anayejua kwamba kuna mtu mwingine huko anayesikiliza tunachozungumza. Nani anayejua kwamba kwenye 'control room' hakuna vinasa sauti. Sasa Mh. twende kwenye sheria. Mh. Nataka nikusomee kanuni ya 13 ya prisons (prison management regulations 1987, GN 60 of 1987 inasema hivi

'Every prisoner shall be given all reasonable opportunities of communication with his legal adviser or with such other person as the officer-in-charge may approve as representing the interests of the prisoner and a visit to a prisoner by the legal adviser or such other person shall take place within the sight but out of hearing of a prison officer.'
Hii kanuni kuu kwamba wakili wanatakiwa wasisikilizwe maneno wanayoyazungumza na mtu mwingine yeyote, ni sehemu ya sheria kuu za kimtaifa Mh. Hakimu. Na nataka nisome The body of principles for the protection of all persons under any form of detention or imprisonment. Zinaitwa maarufu kama The Mandela principles, Kanuni za Mandela zilipitishwa na baraza kuu la umoja wa mataifa, zilipitishwa kwa resolution of the general assembly of united nations resolution number 43/173 of 9th December 1988. Kanuni kuu kuhusu ulinzi wa watu wote ambao wako mahabusu au wamefungwa. Kanuni ya 18 ya mandela's principles,

1. A detained or imprisoned person shall be entitled to communicate and consult with his legal counsel.

2. A detained or imprisoned person shall be allowed adequate time and facilities for consultations with his legal counsel.

3. The right of a detained or imprisoned person to be visited by and to consult and communicate, without delay or censorship and in full con-fidentiality, with his legal counsel may not be suspended or restricted save in exceptional circumstances, to be specified by law or lawful regula-tions, when it is considered indispensable by a judicial or other authority in order to maintain security and good order.

4. Interviews between a detained or imprisoned person and his legal counsel may be within sight, but not within the hearing, of a law enforce-ment official.

5. Communications between a detained or imprisoned person and his legal counsel mentioned in the present principle shall be inadmissible as evidence against the detained or imprisoned person unless they are connected with a continuing or contemplated crime.

Mh. haki ya kwanza niliyonayo kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa magereza ni haki ya kuabudu Mungu, haki ya ibaada. Kanuni ya 14 ya hizi prison management regulations vilevile ipo kwenye Mandela's Principles. Na haki ya kuabudu kila Jumapili wakristo na mimi ni mkristo, wanafanyiwa ibaada gereza kuu la Ukonga. Na kwenye sikukuu za kikristo wafungwa wanafanyiwa ibaada gerezani mimi nilipelekwa Ukonga siku ya ijumaa kuu na nilipopokelekwa nilimuomba mkuu wa gereza nikasali sala ya ijumaa kuu akakataa, Jumapili ya pasaka akakataa, Jumatatu ya Pasaka Bw. Jela nataka niende kusali, akakataa na maekataa nimeomba na amekataa kila jumapili including ya jana. Wafungwa wengine wote wanakwenda kusali isipokuwa mimi.

Kanuni ya 14 inasema

Visits by ministers of religion
(1) A minister of religion shall be admitted at proper and reasonable times to a prison to visit prisoners.

(2) A minister of religion shall be permitted to hold religious services at such hours and in such places as the officer-in-charge may permit and the officer-in-charge shall make such arrangements for the holding of religious services and for the religious instruction of prisoners shall not in any way interfere with the routine and administration of the prison.


Tunaruhusiwa kufundishwa dini, kama hujabatizwa ama, hujapata kipaimara au Komunyo utafundishwa hayo mambo ili ubatizwe au upate Kipaimara au uwe unapata mwili wa bwana na tatu inasema,

(3) The attendance of prisoners at religious services and religious instruction shall be voluntary.
Sio lazima hatulazimishwi kwenda kanisani, unaaenda ukitaka, mimi nimetaka nimekataliwa kwa siku 68. Kwa hiyo Haki yangu ya kuabudu imekiukwa vibaya sana, haki yangu ya kisheria na nimewaambia mawakili wangu wamenipambania wameshindwa.

Tundu Lissu, ameieleza Mahakama kuwa anakabiliwa na mazingira magumu na ya kutisha gerezani, akidai kuwa licha ya kutokuhukumiwa adhabu ya kifo, amekuwa akihifadhiwa katika eneo maalum la wafungwa walioko kwenye orodha ya kusubiri kunyongwa (death row) katika Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

La tatu Mh. Ninakaa wapi gerezani Ukonga, Mh Hakimu, gereza la ukonga lina sehemu kuu mbili, kuna sehemu ambayo wafungwa wote waliohukumiwa maisha, miaka 30, miaka mitano, mahabusu na nini wanakaa, alafu kuna sehemu moja 'special wing' ambalo wanakaa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, mimi nakaa kwenye hiyo sehemu wanaokaa wanaosubiri kunyongwa, nimewekwa death row, Mh. Ukiwa death row maana yake nataka nikusomee sheria kanuni ya 33 inazungumzia wale walioko death room

(1) Notwithstanding anything contained in these Regulations, a prisoner under sentence of death shall–

(a) be confined apart from other prisoners and shall be under the constant supervision of two prison officers by day and by night;


Ukikaa death room Mh. kama ninavyokaa mimi wakati sijahukumiwa kifo angalau bado pengine tutafika huko, sheria inasema wale waliohukumiwa kifo wanatakiwa watengenishwe na wafungwa wengine wote. Mimi nimekaa death row tangu ijumaa kuu mpaka hapa tulipo, na nikitoka kwenda kuonana na ndugu zangu nafuatana na ndugu zangu muda wote kama inavyotakiwa waliohukumiwa kifo, mimi sijahukumiwa kifo. Ukiwa death row Mh. kama ambavyo nimekuwa, bado una haki kwa mujibu wa sheria hii kwa mfano nilizungumza habari ya haki ya kuabudu

33. Prisoners of diet of prisoner by medical officer

(1) Notwithstanding anything contained in these Regulations, a prisoner under sentence of death shall–
(c) be permitted to receive visits by a minister of the religious denomination to which the prisoner belongs;

Kwa hiyo hata wa death row wana haki ya kuabudu, wote wanakataliwa, na mimi.

Ukiwa death row, pamoja na kuwa umehukumiwa kifo, sheria inasema

(e) be allowed such diet and such amount of exercise as the Commissioner may direct;

Wanaruhusiwa kufanya mazoezi, kufanya mazoezi kwenye chumba changu ninachokaa Mh. hapo death row imezungukiwa na ukuta hivi, nyuma ya cello ninayokaa ni uwanja mkubwa wa mpira wa miguu na wafungwa kila siku wanacheza mpira, wanatembea wanaotaka kutembea, wanakimbia wanaotaka kukimbia, wanafanya mazoezi wanaotaka kufanya mazoezi isipokuwa waliopo death row. Wa death row hawatoki nje ya death row, hawana fursa ya mazoezi ambayo sheria imesema wanaruhusiwa kufanya mazoezi. Sasa mimi siwezi kucheza mpira miguu yangu ipo kama ilivyo, huwa nafanya mazoezi ya Kutembea na tangu nimekuwa death row kila siku kuanzia jumatatu mpaka ijumaa. Napumzika Jumamosi na Jumapili kwa sababu Mungu nae alipumzika siku ya saba, lakini around monday to friday natembea around hizo block nne za death row. Sasa hilo eneo nalotembelea, ni mifereji ya maji machafu.


Sheria ya Magereza inasemaje, (Prisons Act) sura ya 58 naomba uangalie kifungu cha 72,

Prisoners under sentence of death shall be confined apart from other prisoners in a special cell or ward. The treatment of the Prisoners under sentence of death shall be such as may be prescribed

Sheria kuu ya magereza inasema sisi ambao sio death row inmates tusikae na watu na watu wa death row

Upande wa Jamhuri ulijibu kuwa haukupata nafasi ya kuwasilisha hoja zao kuhusu madai hayo, Mahakama ikisema imeyapokea maelezo hayo kama taarifa na itaangaliwa kwa mujibu wa taratibu za kiutawala.

KESI YAHAIRISHWA HADI JULAI 01, 2025

Hatimaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu hadi Julai 1, 2025 kwa ajili ya kusubiri Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupitia jalada la kesi hiyo ili kuona kama iende Mahakama Kuu au hapana.

Hatua hiyo inatokana na Upande wa Mashtaka kuomba ahirisho mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franko Kiswaga ambapo Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga alisema jalada la kesi hiyo lipo kwa DPP analipitia kisha atatoa taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia na kama kesi hiyo iende Mahakama Kuu au hapana.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kiswaga ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 1, 2025 ambapo kesi hiyo iliitishwa leo kwa ajili ya kutajwa.

Lissu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 3, 2025 ndani ya Jiji la Dar es salaam kuwa siku hiyo kwa nia ya uchochezi aliushawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku akitamka na kuandika maneno kumshinikiza kiongozi Mkuu wa Serikali ya Tanzania.

Juni 2, 2025, upande wa mashtaka uliieleza Mahakama kuwa jalada la upelelezi lilikuwa limeshawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), lakini baada ya DPP kulipitia alibainisha kuwa kuna jambo ambalo bado lilikuwa halijakaa sawa hivyo alilirejesha tena kwa wapelelezi kufanyia kazi eneo hilo.

Kutokana na taarifa hiyo, kiongozi wa Jopo la waendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga aliomba Mahakama itoe ahirisho mpaka tarehe nyingine.​
 

Attachments

  • snapins-ai_3656033797805921646 (1).mp4
    11.4 MB
Siku hazikawii kufika, usikilizwaji kesi ya Lissu huo umewadia. Kama mnakumbuka wakayi uliopita upande wa mashtaka walisema wanahitaji muda zaidi kukamilisha upelelezi na wakaambiwa tarehe itakayopangwa kutakuwa hakuna nafasi ya hiki kisinngizio tena.

Je, nini kitatokea leo, upande wa mashtaka watatupa taulo na kuomba kutoendelea na kesi?

Wacha tusubiri kuona nini kitajiri.

Hakutakuwa na lolote jipya kwa sababu Kesi yenyewe hii ni ya kupikwa.
 

Attachments

  • Screenshot_2025-06-15-22-13-02-1.png
    Screenshot_2025-06-15-22-13-02-1.png
    433.8 KB · Views: 15
sheria zibadirike mawakili wa serikali, polisi na wahusika wa upelelezi wapewe siku za kufanya upelelezi siku zikiisha basi kesi ifutwe na waambiwe kulipa gharama za kesi

wananakaa wanasumbua watu kwa upumbavu wao tu
 
Nasisi hatutaki watupe tauro , wacha Ngoma iendelee wamthibitishie UHAINI wake , vinginevyo huu upuuzi wakubambikiana kesi zakimama utakuwa mkubwa sana.

Tunachotaka nikwamba
Kesi iendelee na tutawashinda fidia zetu tutachukua na Urais tutachukua

Kamtu kameotea tu kiti hakana hata haibu na wenye inji yao.
 
sheria zibadirike mawakili wa serikali, polisi na wahusika wa upelelezi wapewe siku za kufanya upelelezi siku zikiisha basi kesi ifutwe na waambiwe kulipa gharama za kesi

wananakaa wanasumbua watu kwa upumbavu wao tu
na pia wageuziwe kibao - wakae mahabusu Siku sawa / zilezile mtuhumiwa alivyokaa. Labda hili ndilo litarudisha weledi wao na kuacha danadana
 
Siku hazikawii kufika, usikilizwaji kesi ya Lissu huo umewadia. Kama mnakumbuka wakayi uliopita upande wa mashtaka walisema wanahitaji muda zaidi kukamilisha upelelezi na wakaambiwa tarehe itakayopangwa kutakuwa hakuna nafasi ya hiki kisinngizio tena.

Je, nini kitatokea leo, upande wa mashtaka watatupa taulo na kuomba kutoendelea na kesi?

Wacha tusubiri kuona nini kitajiri.
Juma Ibrahim yule aliyestaafu juzi kisha kupa' hint' kuhusu hili.
 
Back
Top Bottom