Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Jumatano, Februari 18, 2026, inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mapingamizi yaliyowekwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, katika kesi ya uhaini inayomkabili.
Katika kesi hiyo namba 19605/2025, inayosikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, mshtakiwa Tundu Lissu, ambaye anajitetea mwenyewe, anapinga uhalali wa kizimba kilichopo ndani ya chumba cha mahakama kilichoandaliwa kwa ajili ya kutumiwa na shahidi wa siri (PW11) pamoja na mashahidi wengine wa siri watakaofuata. Lissu anadai kuwa kizimba hicho hakikubaliki kisheria.
Soma >
Kesi hiyo, inayosikilizwa kwa awamu (session), inaendelea mfululizo kuanzia Februari 9 hadi Machi 6, 2026.
Kada wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Patrick Assenga ni miongoni mwa waliofika katika Mahakamani Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam kufuatilia kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu.
Akiwa hapa mahakamani ameonyesha ishara ya vidole viwili ambayo CHADEMA wamekuwa wakiitumia huku wakisema 'people's power'.
Ikumbukwe mwaka 2025 Assenga alikihama chama cha CHADEMA na kuhamia CHAUMMA.
Tundu Lissu akiwasili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambako leo kesi ya uhaini inayomkabili inaendelea.
Leo, Februari 11, 2026, Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi mdogo katika kesi hiyo kufuatia pingamizi la Lissu dhidi ya matumizi ya mashahidi wa siri, akitaka watoe ushahidi wao hadharani.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche akiwa na baadhi ya Viongozi na Wajumbe wa chama hicho kwenye Chumba cha MAHAKAMA
Ukumbi wa Mahakama umejaa, huku wanachama mbalimbali wakiwa wametimia mapema kuanzia saa moja kamili. Viongozi mbalimbali pia wamefika, wakiwemo Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi, na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Sugu, ambaye alifika mapema sana. Aidha, Jenerali Ulimwengu pamoja na viongozi wa chama kutoka mikoa, wilaya na majimbo mbalimbali wapo hapa pia.
Muda mfupi uliopita, dua ya kiislamu na sala ya Kikristo zimetolewa. Maombi hayo yametia faraja na kugusa mioyo ya wengi waliokuwepo katika Mahakama.
Askari magereza wameanza kukagua ukumbi wa Mahakama, huku mawakili wa Serikali hawajafika hadi saa tatu na nusu asubuhi.
Leo, Mahakama inatarajiwa kusoma uamuzi mdogo kuhusu mapingamizi yaliyowekwa dhidi ya shahidi wa nne wa Jamhuri, P11, katika kesi ya uhaini. Baada ya usomaji wa ruling, usikilizwaji wa kesi utaendelea, ikiwemo shahidi P11 kutoa ushahidi wake kwa namna ambayo Mahakama itakayoyaamuru—ama ndani ya kiboksi cha siri au hadharani.
Kutoka chumba na.3 cha Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam ambapo Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amepanda kwenye kizimba kwa ajili ya kesi ya uhaini inayomkabili.
Wakati akipandishwa zimesikika kelele za shangwe "Rais, Rais, Rais"
Sehemu ya 158: Uamuzi wa Mahakama Kuu
Lissu amemaliza kupanga vitabu vyake na kukaa kiti chake akiwa amevalia miwani yake na kombati ya Chama. Muonekano wake unaonyesha mabadiliko chanya baada ya muda aliyokaa gerezani, huku kuonekana kuwa mwili wake umepungua kidogo.
Kesi imeanza rasmi baada ya askari magereza kuondoa vikwazo vya uso. Karani alimtambulisha Mkude ambaye alimwakilisha shahidi wa nne wa Jamhuri. Mshitakiwa, Mhe. Lissu, aliweka pingamizi dhidi ya shahidi huyo na kutoa pingamizi tano zenye msingi wa kisheria, yanayohusiana na kanuni za ulinzi wa mashahidi.
Pingamizi la kwanza lilihusu kizimba maalumu cha kutolewa ushahidi, huku mshitakiwa akidai kuwa majaji hawawezi kuona tabia za shahidi. Mahakama imekubaliana kuwa shahidi lazima aonekane kwa majaji, hivyo kizimba kirekebishwe ili kiweze kukidhi matakwa ya kanuni ya tatu.
Pingamizi la pili lilihusu kanuni ya tano kuhusu mashahidi wanaolindwa, ambapo Mahakama ilikubaliana kuwa mashahidi wa siri wamebainishwa na hakukuwa na ulazima wa kutaja majina yao. Pingamizi la tatu lilihusiana tena na kizimba cha shahidi, na Mahakama ilithibitisha kuwa kizimba ni muhimu ili kulinda mashahidi wakati wanatoa ushahidi.
Kwa hiyo, Mahakama imeona kuwa mashahidi hawa waendelee kulindwa kama ilivyopangwa kwenye amri, wakati wa kutoa ushahidi na hata baada ya kumaliza.
Sehemu ya 159
Anaendelea kusoma uamuzi Jaji Ndunguru
Pingamizi la nne lilihusiana na suala la fair trial na haki ya kusikilizwa.
Kwamba atashindwa kumdodosa pia shahidi vizuri kwasababu atakuwa haonekani na hawezi kumuhoji shahidi vizuri.
Mshitakiwa aliturejesha kwenye Katiba na Mikataba ya kimataifa juu ya haki sawa mbele ya Sheria.
Mahakama imetafakari hoja hiyo kwa makini haikuona ni kwa namna gani mshitakiwa atashindwa kumuhoji shahidi kwasababu hamuoni sura yake.
Pingamizi la tano kuhusu kifungu cha 194 cha CPA marekebisho yake hayakutangazwa kwenye gazeti la serikali hivyo ni Sheria ambayo haijaanza kutumika na sehemu ya pili mshitakiwa anasema kanuni za ulinzi wa mashahidi zimetengenezwa baada ya yeye kuwa ameshakamatwa na kufikishwa Mahakamani hivyo haziwezi kufanya kazi baada ya yeye kufikishwa mahakamani.
Upande wa Jamhuri walisema sheria za mwenendo zinatumika hata baada ya kuwa tayari mshitakiwa alishafikishwa mahakamani.
Je Sheria hiyo ilikuwepo wakati mshitakiwa alishafunguliwa mashitaka? Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi zimetengenezwa na Jaji Mkuu kwa mujibu wa kifungu cha 194 (3) cha CPA kilikuwepo toka mwaka 2018.
Hivyo basi vinaeleza kuwa ulinzi wa mashahidi unavyotakiwa kufanyika.
Jaji Mkuu amepewa mamlaka ya kutengeneza hizo kanuni za mashahidi hivyo basi kutengeneza kanuni mwaka 2025 wakati kanuni hizo zimetengenezwa chini ya kifungu cha 194 ambacho kilikuwepo toka mwaka 2018 basi hatuwezi kusema kanuni hizo ni sheria mpya.
Hata kanuni hizi zisingekuwepo basi hatuwezi kusema mashahidi wasingeweza kulindwa kwasababu kanuni hazikuwepo au hazijatungwa.
Mahakama imeridhika kuwa kifungu cha 194 kilikuwepo kabla ya kanuni hizi za 2025 na hatuwezi kusema sheria ya ulinzi wa mashahidi haikuwepo lengo la kanuni hizo ni kurahisisha utekelezaji wa kifungu cha 194 cha Sheria ya mwenendo wa Makosa ya jinai.
Wakati upande wa Mashitaka walitoa gazeti kuonesha sheria hiyo ilitangazwa na Mshitakiwa alisema hakufanikiwa kupata gazeti hilo na kusema sheria hiyo haikutangazwa.
Kifungu cha 63 na 64 cha ushahidi wa judicial notes kuwa sheria hiyo ipo na kuamini.
Mahakama imejiridhisha kuwa sheria hiyo ilitangazwa na imekubali pingamizi moja na mapingamizi mengine manne yaliyobaki Mahakama imeyakataaa.
Hivyo kizimba kirekebishwe na tuendeleee na usikilizwaji wa kesi kama ilivyoamriwa hapo juu.
Anasimama Renatus Mkude anasema baada ya kupata amri na uamuzi wa Mahakama tunaomba ahirisho ili kizimba kirekebishwe.
Anaitwa Mh. Lissu aseme.
Anasema yeye anapinga kesi kuahirishwa.
Jamhuri wa Mashahidi 30 na waliolindwa wapo 11 na 19 hawajalindwa sasa walipaswa kujua kuwa mahakama ikikataa mashahidi kulindwa lazima wawe na shahidi mwingine wa kuleta.
Hii ya kuahirisha kesi kwasababu ya kurekebishwa kizimba ni kunionea na kunikosesha haki zangu.
Waheshimiwa Majaji mimi sina hatia yoyote hii ya kuahirisha kesi kwa sababu hii siiungi mkono kwasababu mkiahirisha mimi naenda kukaa jela.
Anasimama Mkude tena anasema Mheshimiwa tuliwaandaa hao mashahidi wa siri kwa sasa hatuna shahidi mwingine yeyote na huo ndio utamaduni wetu wa kuendesha hizi kesi Mawakili wa Serikali kwahiyo hoja ya kuahirisha iko pale pale. Tunaomba tuahirishe kizimba kirekebishwe.
Naona Majaji Wanateta hapa.
Anawasha kipaza sauti Jaji Ndunguru.
Anasema tumesikia hoja zote, shauri hili litaendelea kesho Februari 12, 2026 saa tatu asubuhi.
Katika kesi hiyo namba 19605/2025, inayosikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, mshtakiwa Tundu Lissu, ambaye anajitetea mwenyewe, anapinga uhalali wa kizimba kilichopo ndani ya chumba cha mahakama kilichoandaliwa kwa ajili ya kutumiwa na shahidi wa siri (PW11) pamoja na mashahidi wengine wa siri watakaofuata. Lissu anadai kuwa kizimba hicho hakikubaliki kisheria.
Soma >
- Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu kuendelea Februari 9 hadi Machi 6, 2026
- Shahidi wa Kesi ya Lissu (P7): Nauli ya kuja mahakamani leo nimepewa na mwanamke wangu. Ndiye ananiweka mjini
- Kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 17, 2026, mashahidi wa Jamhuri wasiopungua watatu wangojewa
- Kesi ya uhaini dhidi ya Lissu: Shahidi wa saba kati ya 30 wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa Siri (P6): Lissu alisema tunakwenda kuvuruga uchaguzi na kukinukisha
- Kesi ya Lissu: Hiki ndicho Kizimba cha mashahidi wa kificho, kilichosababisha Kesi kuahirishwa
- Baada ya takribani miezi mitatu, kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 9, 2026
- Kesi ya Lissu: Mahakama yaagiza Kizimba cha Mashahidi wa siri kirekebishwe Majaji wawaone. Kesi kuendelea Feb 12, 2026
- Kesi ya uhaini ya Lissu, mahakama kutoa uamuzi wa mapingamizi leo Feb 11, 2026
- Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu kuendelea Februari 9 hadi Machi 6, 2026
- Shahidi wa kesi ya Lissu (P7) anasema alikamatwa mara tu baada ya kuangalia video ya Lissu iliyokuwa Jambo TV
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa siri (P5): Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha, uchaguzi mkuu hautafanyika
- Mama wa CHADEMA azimia mahakamani baada ya Lissu kudai kunyimwa chakula
- Mahakama kuu, Kanda ya Dar es salaam Tarehe 11 Februari, 2026 kutoa uamuzi mdogo katika kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu