Meengi yatasikika,,ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni,,Eti naskia na yule mchungaji wa iringa anaeitwa msigwa anahamasisha wanachama kuunga mkono suala la zitto kutimuliwa...!!,,inashangaza sana,yeye kaja jana tuh anajiona ana uchungu na chama kushinda wale walokijenga???chdema kinashangaza sana,hili suala la zitto tuh limesimamisha mipango yao yote siku tukiwapa nchi kuongoza kweli wataweza kuhimili vishindo vya ndan na nje ya nchi kweli hawa??Huu utaratibu wa kupokea maagizo toka kwa Ayatollah Mtei ndio chanzo kikuu cha mtafaruku ndan ya chama hki,undugu na kujuana Juana,,udini na ukabila ukabila,ukanda na uasi wa sharia za mungu muumba ndio kwa kias kikubwa kunapelekea kama chama hiki kuonekana kimepigwa laana hivi kuelekea 2015,,CCM imeshindwa kuongoza nchi,then watu ambao walikuwa wanapewa tumain hilo wanashindwa kujiongoza sembuse hata wenyewe kw wenyewe na kuheshim katiba ya chama chao,,je wataweza ongoza taifa na kuheshim katiba ya taifa letu??YALIYOJIRI MAHAKAMANI HII LEO WAKATI ZITTO KABWE ANAWASILISHA PINGAMIZI LA KUTOJADILIWA NA KAMATI KUU YA CHADEMA HAPO KESHO,Na, Hans Kasapa.
Leo Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe, mbunge wa Chadema, Kigoma Kaskazini. Kamati Kuu ya Chadema inatarajia kuanza kikao chake kesho na moja kati ya agenda zake ni kupokea utetezi wa Zitto Kabwe kuhusu uanachama wake dhidi ya tuhuma 11 zilizotolewa hapo awali. Hata hivyo ikumbukwe kuwa baada ya Kamati Kuu kumvua nyadhifa Zitto Kabwe, aliandika barua ya notisi ya kukata rufaa kupinga maamuzi ambayo ni kinyume cha katiba, kanuni na taratibu za chama.
Katika barua hiyo aliomba mwenendo wa mashtaka ili kukamilisha rufaa rasmi. Mpaka sasa hajajibiwa badala yake Zitto Kabwe ameitwa na chombo kilekile, kwa kosa lilelile, kwa adhabu kubwa zaidi. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na misingi ya haki asili (natural justice).
Hivyo amekwenda mahakamani kuomba mahakama izuie Kamati Kuu isijadili au kuamua chochote juu ya uanachama wake mpaka atakapopata fursa ya kukata rufaa kwenye Baraza Kuu kwa mujibu wa katiba ya chama.
Baada ya majibizano ya kisheria ya masaa 4 yaliyotokana na pingamizi 3 zilizowekwa na jopo la mawakili wa Chadema, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za wakili msomi Albert Msando na kutupilia mbali pingamizi hizo.
Mahakama imetoa amri ya kuzuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe. Pia mahakama imeagiza Chadema ipeleke majibu yao dhidi ya haki ya kiapo ya Zitto hapo kesho tarehe 03/01/2014.
Ieleweke kuwa kesi iliyopo mahakamani ya 01/2014 ni ya Zitto Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema, na hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa na Kitila Mkumbo au Samson Mwigamba.
Kesi ya msingi imepangiwa kuanza kusikilizwa tarehe 21/02/2014.
Huyo ndo zitto kabwe, anatenda hiki na anasema kile, mtu yeyote anayemuunga mkono kwa hoja yake 100% inabidi asifikiri zaidi, mfano wa kauli tata za zitto ni sitagombea ubunge mwaka 2015, nitagombea urais, nitakwenda kufundisha naacha siasa. Nk. Ni full mchanganyiko! Bado mapesa ya uswis!
Naona movie limefika patamu
YALIYOJIRI MAHAKAMANI HII LEO WAKATI ZITTO KABWE ANAWASILISHA PINGAMIZI LA KUTOJADILIWA NA KAMATI KUU YA CHADEMA HAPO KESHO,Na, Hans Kasapa.