Kesi ya msingi ya Zitto Kabwe kuanza kusikilizwa tarehe 21/02/2014...

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
YALIYOJIRI MAHAKAMANI HII LEO WAKATI ZITTO KABWE ANAWASILISHA PINGAMIZI LA KUTOJADILIWA NA KAMATI KUU YA CHADEMA HAPO KESHO,

1526978_172829729593906_1780052713_n.jpg

Na, Hans Kasapa.
Leo Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe, mbunge wa Chadema, Kigoma Kaskazini. Kamati Kuu ya Chadema inatarajia kuanza kikao chake kesho na moja kati ya agenda zake ni kupokea utetezi wa Zitto Kabwe kuhusu uanachama wake dhidi ya tuhuma 11 zilizotolewa hapo awali. Hata hivyo ikumbukwe kuwa baada ya Kamati Kuu kumvua nyadhifa Zitto Kabwe, aliandika barua ya notisi ya kukata rufaa kupinga maamuzi ambayo ni kinyume cha katiba, kanuni na taratibu za chama.

Katika barua hiyo aliomba mwenendo wa mashtaka ili kukamilisha rufaa rasmi. Mpaka sasa hajajibiwa badala yake Zitto Kabwe ameitwa na chombo kilekile, kwa kosa lilelile, kwa adhabu kubwa zaidi. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na misingi ya haki asili (natural justice).

Hivyo amekwenda mahakamani kuomba mahakama izuie Kamati Kuu isijadili au kuamua chochote juu ya uanachama wake mpaka atakapopata fursa ya kukata rufaa kwenye Baraza Kuu kwa mujibu wa katiba ya chama.

Baada ya majibizano ya kisheria ya masaa 4 yaliyotokana na pingamizi 3 zilizowekwa na jopo la mawakili wa Chadema, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za wakili msomi Albert Msando na kutupilia mbali pingamizi hizo.

Mahakama imetoa amri ya kuzuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe. Pia mahakama imeagiza Chadema ipeleke majibu yao dhidi ya haki ya kiapo ya Zitto hapo kesho tarehe 03/01/2014.
Ieleweke kuwa kesi iliyopo mahakamani ya 01/2014 ni ya Zitto Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema, na hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa na Kitila Mkumbo au Samson Mwigamba.

Kesi ya msingi imepangiwa kuanza kusikilizwa tarehe 21/02/2014.

kuna harufu ya upotoshaji hapa, nasubiri kesho saa tatu nitakuwa mahakama kuuuuu, manake vyanzo vyangu vya habari vimenitonya kuwa maamuzi ya ajadiliwe ama asijadiliwe yatatolewa kesho mapema kwani kapingamizi hako katasikilizwa.
 
div 5 mnatuchosha kama enzi za masalia mwisho wa siku mkaonyesha mzigo ulipo we subirini ndo mtaisoma namba CHADEMA YATOSHA
 
Mtanisamehe lakini nyie akina tuntemeke pengine mnaumaskini wa akili lakini kwa tabia yenu hii hta umaskini wa kipato pia...ni maskini wa kila kitu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
huyu jaji utamwa niliwai kuambiwa na jaji kiongozi kuwa yeye ndiye wanamtumia katika maswala ya kisiasa na kiserekali
 
Asante kwa taarifa ya kesi ya msingi. Lakini kuna maswali mengi bado yahapo wazi. Je ni nini hasa Bwana Zito anataka. Je anataka mahakama iamuru afutiwe mashitaka yake mbele ya kamati kuu? mashitaka ambayo tayari ameyajibu? au anataka rufaa yake isikilizwe katika baraza kuu au anataka mahakama sasa ifanye kazi ya wanachama ya kuamua hatima ya Zito. Amri ya mahakama ya kuzuia Chadema isijadili chochote juu ya Zito inahusu hata vitu ambavyo havilalamikiwi mahakamani? Zito ataweza kugombea uongozi wa chama chake akiwa ameweka zuio la yeye aweze kujadiliwa? je yeye ana haki ya kujadili chama chake wakati kukiwa na zuio la mahakama?
 
Huyo ndo zitto kabwe, anatenda hiki na anasema kile, mtu yeyote anayemuunga mkono kwa hoja yake 100% inabidi asifikiri zaidi, mfano wa kauli tata za zitto ni sitagombea ubunge mwaka 2015, nitagombea urais, nitakwenda kufundisha naacha siasa. Nk. Ni full mchanganyiko! Bado mapesa ya uswis!
 
YALIYOJIRI MAHAKAMANI HII LEO WAKATI ZITTO KABWE ANAWASILISHA PINGAMIZI LA KUTOJADILIWA NA KAMATI KUU YA CHADEMA HAPO KESHO,

1526978_172829729593906_1780052713_n.jpg

Na, Hans Kasapa.
Leo Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe, mbunge wa Chadema, Kigoma Kaskazini. Kamati Kuu ya Chadema inatarajia kuanza kikao chake kesho na moja kati ya agenda zake ni kupokea utetezi wa Zitto Kabwe kuhusu uanachama wake dhidi ya tuhuma 11 zilizotolewa hapo awali. Hata hivyo ikumbukwe kuwa baada ya Kamati Kuu kumvua nyadhifa Zitto Kabwe, aliandika barua ya notisi ya kukata rufaa kupinga maamuzi ambayo ni kinyume cha katiba, kanuni na taratibu za chama.

Katika barua hiyo aliomba mwenendo wa mashtaka ili kukamilisha rufaa rasmi. Mpaka sasa hajajibiwa badala yake Zitto Kabwe ameitwa na chombo kilekile, kwa kosa lilelile, kwa adhabu kubwa zaidi. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na misingi ya haki asili (natural justice).

Hivyo amekwenda mahakamani kuomba mahakama izuie Kamati Kuu isijadili au kuamua chochote juu ya uanachama wake mpaka atakapopata fursa ya kukata rufaa kwenye Baraza Kuu kwa mujibu wa katiba ya chama.

Baada ya majibizano ya kisheria ya masaa 4 yaliyotokana na pingamizi 3 zilizowekwa na jopo la mawakili wa Chadema, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za wakili msomi Albert Msando na kutupilia mbali pingamizi hizo.

Mahakama imetoa amri ya kuzuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe. Pia mahakama imeagiza Chadema ipeleke majibu yao dhidi ya haki ya kiapo ya Zitto hapo kesho tarehe 03/01/2014.
Ieleweke kuwa kesi iliyopo mahakamani ya 01/2014 ni ya Zitto Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema, na hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa na Kitila Mkumbo au Samson Mwigamba.

Kesi ya msingi imepangiwa kuanza kusikilizwa tarehe 21/02/2014.

Meengi yatasikika,,ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni,,Eti naskia na yule mchungaji wa iringa anaeitwa msigwa anahamasisha wanachama kuunga mkono suala la zitto kutimuliwa...!!,,inashangaza sana,yeye kaja jana tuh anajiona ana uchungu na chama kushinda wale walokijenga???chdema kinashangaza sana,hili suala la zitto tuh limesimamisha mipango yao yote siku tukiwapa nchi kuongoza kweli wataweza kuhimili vishindo vya ndan na nje ya nchi kweli hawa??Huu utaratibu wa kupokea maagizo toka kwa Ayatollah Mtei ndio chanzo kikuu cha mtafaruku ndan ya chama hki,undugu na kujuana Juana,,udini na ukabila ukabila,ukanda na uasi wa sharia za mungu muumba ndio kwa kias kikubwa kunapelekea kama chama hiki kuonekana kimepigwa laana hivi kuelekea 2015,,CCM imeshindwa kuongoza nchi,then watu ambao walikuwa wanapewa tumain hilo wanashindwa kujiongoza sembuse hata wenyewe kw wenyewe na kuheshim katiba ya chama chao,,je wataweza ongoza taifa na kuheshim katiba ya taifa letu??
 
Huyo ndo zitto kabwe, anatenda hiki na anasema kile, mtu yeyote anayemuunga mkono kwa hoja yake 100% inabidi asifikiri zaidi, mfano wa kauli tata za zitto ni sitagombea ubunge mwaka 2015, nitagombea urais, nitakwenda kufundisha naacha siasa. Nk. Ni full mchanganyiko! Bado mapesa ya uswis!

That's politics..!!wewe maamuma ndio usioelewa,Struggle For Political power is by all means...!!
 
Naona movie limefika patamu

Kesi hii haina mashiko na Zitto anajaribu kununua tu muda!Wakili wa Zitto n mbumbumbu kwenye kesi za katiba!

1.Kuvuliwa nyadhifa SIO HUKUMU bali ni process ya kwenda kwenye hukumu
2.Zitto HANA "Miranda " yyt inayo suport madai yake kuwa hapaswi kuhukumiwa mara mbili kwa kesi ile ile
3.Leo ndiyo itajulikana kama CC iendelee kumjadili au hapana na wala sio kama alivyo potosha mleta mada
 
Tuntemeke anataka kucheza na akil za watu asubil aone leo,hawa washaur wa zitto ndio waliomfksha hapa
 
Heko chadema,kafukuzeni hako kajamaa.Kamekuwa kanadhani kanaweza kuwa juu ya chama.Hizo pingamizi za mahakamani kalizoanza kuzileta ni mbio za sakafuni tu,na zitaishia ukingoni.

Zito kwishney,anafuata nyayo za Kafulila sasa.

NAFURAHI SANA
 
aendelee kuzunguka kigoma kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji
 
YALIYOJIRI MAHAKAMANI HII LEO WAKATI ZITTO KABWE ANAWASILISHA PINGAMIZI LA KUTOJADILIWA NA KAMATI KUU YA CHADEMA HAPO KESHO,

1526978_172829729593906_1780052713_n.jpg

Na, Hans Kasapa.
Leo Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam imetoa zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe, mbunge wa Chadema, Kigoma Kaskazini. Kamati Kuu ya Chadema inatarajia kuanza kikao chake kesho na moja kati ya agenda zake ni kupokea utetezi wa Zitto Kabwe kuhusu uanachama wake dhidi ya tuhuma 11 zilizotolewa hapo awali. Hata hivyo ikumbukwe kuwa baada ya Kamati Kuu kumvua nyadhifa Zitto Kabwe, aliandika barua ya notisi ya kukata rufaa kupinga maamuzi ambayo ni kinyume cha katiba, kanuni na taratibu za chama.

Katika barua hiyo aliomba mwenendo wa mashtaka ili kukamilisha rufaa rasmi. Mpaka sasa hajajibiwa badala yake Zitto Kabwe ameitwa na chombo kilekile, kwa kosa lilelile, kwa adhabu kubwa zaidi. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na misingi ya haki asili (natural justice).

Hivyo amekwenda mahakamani kuomba mahakama izuie Kamati Kuu isijadili au kuamua chochote juu ya uanachama wake mpaka atakapopata fursa ya kukata rufaa kwenye Baraza Kuu kwa mujibu wa katiba ya chama.

Baada ya majibizano ya kisheria ya masaa 4 yaliyotokana na pingamizi 3 zilizowekwa na jopo la mawakili wa Chadema, Jaji John Utamwa alikubaliana na hoja za wakili msomi Albert Msando na kutupilia mbali pingamizi hizo.

Mahakama imetoa amri ya kuzuia kwa muda Kamati Kuu ya Chadema kujadili na kuamua suala lolote linalomhusu Zitto Kabwe. Pia mahakama imeagiza Chadema ipeleke majibu yao dhidi ya haki ya kiapo ya Zitto hapo kesho tarehe 03/01/2014.
Ieleweke kuwa kesi iliyopo mahakamani ya 01/2014 ni ya Zitto Kabwe dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu wa Chadema, na hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa na Kitila Mkumbo au Samson Mwigamba.

Kesi ya msingi imepangiwa kuanza kusikilizwa tarehe 21/02/2014.

Zitto anajipotezea muda, ni heri kwake angeachana na chadema, hata mahakama kuu ikishinikiza asifukuzwe leo atafukuzwa kesho, kama hupendwi hupendwi tu, kujipendekeza kuna gharimu sana, CCM nacho ni chama na walioko huko ni watu tena watanzania

Aongee na JK vizuri, huenda akamtendea vyema akaachana na Chadema, akapoteza ubunge lakini akahamia CCM Mh Rais akamteua kuwa Mbunge na labda na uwaziri juu

Anafaa kuwa Waziri wa Fedha huyu! Labda akiwa Waziri wa fedha yale mabilioni yaliyofichwa yatarudi, madawa yakaongezeka hospitalini pamoja na vifaatiba, shuleni atleast madawati, vitabu, na waalimu wakaboreshewa maslahi yao elimu ikawa bora

Ajipange sipendi kumuona Chadema sababu anavuruga chama, ila napenda kumuona sehemu nyingine hasa CCM anakoungwa mkono 100%
 
Zito ana haki zote za kufanya hivyo , tuache ushabiki maana wengine ni bendera fuata upepo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom