Kesi ya Mramba sasa Novemba 18 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Mramba sasa Novemba 18

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Oct 20, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  Nora Damian
  KESI ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni inayowakabili mawaziri wa zamani Basil Mramba, Daniel Yona na Katibu mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja imepigwa kalenda hadi Novemba 18, mwaka huu.
  Kesi hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Sundi Fimbo kwa madai kuwa bado mwenendo wa kesi unapitiwa na jopo linalosikiliza kesi hiyo.

  Mwenendo huo unasubiriwa na pande zote mbili ili ziweze kutoa hoja kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.

Hakimu Fimbo alisema kuwa bado jopo linalosikiliza kesi hiyo halijamaliza kupitia mwenendo wa kesi hiyo, hivyo akaahirisha kesi hiyo hadi Novemba 18 mwaka huu.
  Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi kinyume cha sheria kampuni ya M/S Alex Stewart ya nchini Uingereza.

  Wakati huohuo, kesi ya wizi wa Sh6.3 bilioni za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu Tanzania (BoT) nayo iliahirishwa hadi Novemba 18, mwaka huu itakapotajwa tena.

  
Washtakiwa katika kesi hiyo ni, Johnson Lukaza na ndugu yake Mwesiga Lukaza.

Wakili wa Serikali Shadrack Kimaro aliomba mahakama kupanga tarehe ya kutajwa ili mahakama iweze kupanga tarehe ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

  Katika kesi hiyo,washtakiwa wanadaiwa kuwa kati ya Desemba mwaka 2003 na mwaka 2005 siku tofauti walikula njama ya kufanya ubadhirifu Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  Washtakiwa hao wanadaiwa kujipatia Sh6.3 bilioni baada ya kudanganya kuwa Kampuni ya Kernel Limited ya Tanzania imehamishiwa deni na kampuni ya Maruben Corporation ya nchini Japan.

  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
Loading...