Kesi ya Meya anayeshtakiwa kwa mauaji yapigwa kalenda

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125










Meya%20Mwanza%282%29.jpg

Meya wa Jiji la Mwanza, Leonard Bandiho Bihondo



Kesi ya mauaji inayomkabili Meya wa Jiji la Mwanza, Leonard Bandiho Bihondo (64) pamoja na washtakiwa wenzake watatu, jana ilitajwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini hapa.
Kesi hiyo ilitajwa kwa mara ya nne mbele ya Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Amon Kihimba.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Pius Hirra, uliiambia mahakama kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Kesi hiyo ya jinai namba 16/2010 ya mwaka 2010, ilitajwa kwa mara ya kwanza Mei 21, mwaka huu na iliahirishwa na Hakimu Hirra hadi Julai 16, mwaka huu.
Meya Bihondo anatetewa na wakili wa kujitegemea, Deo Mgengele.
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni Jumanne Osca, mkazi wa Mkoa wa Kigoma, Baltazar Shausi pamoja na Abdu Ausi, ambao ni wakazi wa Kata ya Isamilo jijini Mwanza.
Watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Isamilo, Bahati Stephano (46), aliyefariki dunia kwa kuchomwa kisu kifuani.
Oscar ndiye anayetuhumiwa kumchoma kisu Bahati Mei 14, mwaka huu kisha kutimua mbio kabla ya kukamatwa.
Bihondo alikamatwa Mei 19, mwaka huu wakati akiwa kwenye uwanja wa ndege jijini Mwanza akirejea kutoka Dar es Salaam, baada ya kutajwa na watuhumiwa wenzake



CHANZO: NIPASHE

Hi Nchi Yetu inaongozwa na Viongozi Wauaji kama hawa? Tutafika kule tunakokwenda jamani?
 
Back
Top Bottom