Kesi ya Mahalu:Rais Mstaafu B.W. Mkapa Kortini Mei 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Mahalu:Rais Mstaafu B.W. Mkapa Kortini Mei 8

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by WomanOfSubstance, May 1, 2012.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 8, mwaka huu kumtetea aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu.Wakili anayemtetea Balozi Mahalu, Mabere Marando alisema jana kwamba Mkapa atapanda kizimbani siku moja baada ya Profesa Mahalu kumaliza kutoa utetezi wake.

  Awali, akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ilvin Mgeta Wakili Marando alisema Mei 8, kutakuwa na shahidi mwingine wa mwisho muhimu ambaye hata hivyo, hakumtaja.
  Alipoulizwa kuhusu shahidi huyo nje ya Mahakama, Marando alimtaja kuwa ni Rais Mstaafu Mkapa na baadaye alipopigiwa simu kutoa ufafanuzi zaidi alisema: “Mkapa ni shahidi wa Mahalu hivyo atafika mahakamani kutoa ushahidi wake kwa maneno.” Source :http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/22523-kesi-ya-mahalumkapa-kortini-mei-8.html

  Swali ni je, Mkapa akikubali kwenda "kutoa ushahidi kwa kumtetea Mahalu", haitamweka pabaya kwamba anaweza kujikuta akitakiwa mahakamani kwa kesi mbalimbali maana kuna mlolongo wa mashauri yanayotokana na watendaji wa kipindi chake kukiuka sheria mbalimbali.
  Wanasheria hebu nongesheni mjadala huu kwa kuzingatia zaidi SHERIA na SIYO SIASA.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Wewe unaona kuwa atakuwa amejivua kinga?!, je; huyu raiis wa sasa ambaye anawaongoza watendaji na mawaziri wake kugawana raslimali za taifa atajipimaje?. Visa na visasi vya Huyu raisi wa sasa ndivyo vinawafikisha marais wastaaf hapo tulipo, hata hivyo mwambie huyu rais wako wa sasa kuwa "ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji". Hii vita aliyoianzisha kuanzia kwa "Liumba na sasa mahalu" lazima iishe naye.
   
Loading...