Kesi ya mafisadi wa Escrow, PAP, IPTL na Singasinga Sethi dhidi ya Kafulila

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
KESI YA MAFISADI WA ESCROW, PAP, IPTL NA SINGASINGA SETHI DHIDI YA MHE KAFULILA WAKITAKA KAFULILA AWALIPE 100M KUENDELEA KISUTU KESHO.

Kesi hiyo No 239 of 215 iliyofunguliwa na Kampuni za IPTL,PAP na Mkurugenzi wa PAP Bw Singh Sethi itaanza kuunguruma kesho Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mchauru baada ya pande mbili kushindwa kukubaliana nje ya mahakama( mediation) kufikia May9.2016.

Kesi hiyo ilifunguliwa upya Mahakama ya Kisutu baada ya kufunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salama, kesi No 110 ya 2014 ambayo ilitupwa kutokana na hoja kwamba madai walalamikaji kuwa walipwe fidia ya 310bn kama fidia ya kuchafuliwa na Mhe Kafulila nje ya Bunge kuonekana ni madai ya jumla na hivyo Mahakama Kuu haiwez kushughulikia madai ya jumla isipokuwa Mahakama za chini.

Nikawasababu hiyo, walalamikaji waliamua kuifungua kesi hiyo Mahakama ya Kisutu na kupunguza madai kutoka 310bn waliokuwa wamedai Mahakama Kuu hadi 100m ambayo wameomba kulipwa Mahakama ya Kisutu.

Walalamikaji kwa upande wao wanawakilishwa na Wakili Makandege wakati upande wa mlalamikiwa Mhe Kafulila anawakilishwa na Wakili Mtobesya na Masawe.

Katika hatua nyingine, Mawakili wa Mhe Kafulila wameingiza leo Mahakamani nyaraka za aina 6 ambazo wamepanga kuzitumia katika kesi hiyo kuthibitisha madai ya Mhe Kafulila dhidi ya walalamikaji kuwa walipora mabilioni kwenye akaunti ya tegeta escrow kifisadi, Nyaraka hizo ni; Mkataba wa IPTL vs Tanesco wa mwaka 1995, Mkataba wa Tegeta Escrow wa 2006, Ripoti ya Ukaguzi maalumu wa CAG kuhusu miamala ya Tegeta Escrow ya 2014, Ripoti ya PAC yenye maazimio ya Bunge ya Novemba 2014, Uamuzi wa awali wa Mahakama ya Benki ya dunia wa Feb12,2014 pamoja na Hukumu ya Mahakama hiyo ya Benk ya dunia ilotolewa Septemba 2016.

Katika hatua nyingine, Mhe Kafulila kupitia mawakili wake amepanga kuiomba Mahakama ielekeze ripoti ya uchunguzi wa PCCB kuhusu ufisadi huu iwasilishwe mahakamani pamoja na ripoti ya Baraza la Maadili iliyoendesha mashtaka kuhusu sakata hili na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Rais nayo yaletwe Mahakamani ili kuthibitisha ukweli wa jambo hilo.
 
Back
Top Bottom