Wakati wa sakata la madawa tumeweza kupingwa kiwango cha maadili/uwajibikaji wa viongozi wetu.
- Kufuata sheria na Taratibu za nchi
- Mchakato mzima ulionesha ukiukaji mkubwa wa sheria/kanuni ikiwemo sheria yenyewe ya udhibiti wa madawa ya kulevya. kwa kutokuheshimu sheria, kulipelekea pia watu kadhaa kukosa adabu kwa viongozi husika, ikwemo waliowasema vibaya viongozi wa nchi bila ya kuwa na stara lkn pia wapo waliokaidi wito na kupuuzia kabisa na wenye mamlaka wakashindwa kuchukua hatua.
- tunachjifunza hapa, ni kuwa endapo viongozi hawatosimamia sheria, watapuuzwa na kudharauliwa na jamii.
- Kutozingatia maadili ya uongozi (Professionalism)
- unaweza kuona umuhimu wa seminar elekezi baada ya sakata hili. naomba tuorodheshe makosa ya kimaadili au kitaalamu yaliyofanyika.
- Mkuu wa mkoa(DSM) vs wabunge
- tusingetegemea aina ya maneno waliyokuwa wanarushiana. hawa ni viongozi lazima wangekuwa na platform sahihi ya kujibishana tofauti zao
- Kamanda wa Polisi na majibu ya vipimo vya Manji/msako kwa wema
- Haikuwa jambo sahihi kwa kiongozi wa usalama kutamka hadharani majibu ya vipimo vya mtu, hata kama huyo mtu angekuwa mjeuri kiasi gani. kamanda alipaswa kukusanya ushahidi na kupeleka mahakamani na sio mapambano binafsi na kuanza kuanika waharifu kwenye vyombo vya habari.
- Mkuu wa mkoa(DSM) vs wabunge
- unaweza kuona umuhimu wa seminar elekezi baada ya sakata hili. naomba tuorodheshe makosa ya kimaadili au kitaalamu yaliyofanyika.
- kujibishana kivijembe na wananchi au wakosoaji wengine wa utendaji wako
- viongozi wengi wamekuwa na tabia za kujibishana vijembe na wananchi ktk mitandao ya kijamii. matokeo yake wanaishia kudhalilika kwa kuanikwa mambo yao binafsi, wanapoteza heshima binafsi na zile za nafasi zao. inawawekea ugumu kupata support kwa wananchi kwa vile aina hii ya maisha inawamega mno.