Kesi ya madai: Naombeni ushauri katika hili

otimbiotimbi

Senior Member
Dec 12, 2019
100
135
Ndugu wana JamiiForums, nina kesi ya madai ambapo upande wa pili una wakili na upande wangu nilimuweka wakili akala hela akaingia mtini.

Tulipewa muda wa kupeleka majibu ya hoja zilizokuwa zimetolewa na upande wa pili lakini kutokana na mwanasheria wangu kutokuwa na ushirikiano, nikaomba kuongezewa muda wa kuleta majibu ambapo nilimpa mwanasheria mwingine aandae majibu lakini hayakukamilika kwa wakati ambao ulipangwa na mahakama.

Nilipofika mahakamani ikapangwa tarehe ambayo mahakama itatoa maamuzi au la.

Naombeni ushauri nifanye nini kwakuwa mdeni tulikuwa tunalipana na slip za benki zipo na kiasi alichoandika kuwa ananidai si kweli.
 
Kwa maelezo yako wewe utakuwa umeshindwa kupeleka kitu kinaitwa Written Statement of Defence(WSD) katika muda uliotakiwa kufanya hivyo na hata ulipoongezewa muda wa kupeleka majibu hayo, ukashindwa pia.

Kama ni hivyo, basi mahakama inaweza kuamua kesi isikilizwe upande mmoja(Ex parte). Na hukumu ikitoka itakuwa ni defualt judgment dhidi yako.

Lakini kabla ya hukumu ya kesi iliyosikilizwa upande mmoja haijatolewa, unaweza kupeleka maombi ya mahakama kutengua amri yake ya kesi kusikilizwa upande mmoja ili sasa uruhusiwe kupeleka utetezi wako na msikilizwe wote(inter partes)

Lakini hata kama hukumu ikitoka kwa kesi iliyoendeshwa upande mmoja, bado unaweza kupeleka maombi nadani ya siku 60, kama una sababu nzuri, ya kuomba mahakama itengue hukumu yake na kuruhusu msikilizwe wote.

Lakini pia maelezo yako yamenipa idea kwamba huenda kuliwekwa pingamizi( Preliminary Objection) kuhusiana na kesi, halafu wenzako wakapeleka hoja zao ndani ya muda uliopangwa, na wewe hukupeleka hoja zako ndani ya muda uliopewa. Na hata ulipongezewa muda hukupeleka hoja zako.

In this case, mahakama itatoa uamuzi (ruling) juu ya pingamizi bila ya hoja zako. All in all, tafuta wakili akusaidie na kukushauri kwa kina.
 
Mkuu Otimbi pole sanaa na maswahibu hayo, ni wazi hayo malumbano ya hoja yalikua ni Final Submissions kwa maana ya utetezi wa hoja wa kina baina yenu na wakili wako kala kona kuona kufanya uvivu kupiga research, au what so ever, kikubwa ni kujua tu unafanya nini kwa wakati huu basi!

Kikawaida kushindwa kufanya jambo flani ktk kesi yako hasa baada ya order ya mahakama kukutaka wewe ufanye jambo ilo hua kuna kupelekea wewe kushindwa kesi yako kwa asilimia 90, izo 10 ni pale mahakama ijiendeshe kwa maoni yake yenyewe bila kuongozwa ndo itende haki juu yako ambapo kisheria tunasema mahakama ime rule on its own motion, hili ni very rare kutokea pia, sasa basi ni wakati wako ukafanya maombi madogo kwenye hio hio mahakama uombe kuongezewa muda kwa mara nyingine kwa kua sababu zako ni reasonable ambapo unaweza kuonhezewa muda au usiongezewe muda, kama hauto ongezewa muda kuna remedies zake ambazo ukimtafta wakili muelewa atakusaidia na mambo yakawa juu ya mstali.

Chukua risiti zako andaa kila aina ya ushaidi na ulizia tume ya maadili ya mawakili iko wapi? au ulizia ofisi ya chama cha mawakili Tanganyika uende wakakupe muongozo bure tu, huko kwenye hii tume utamfungulia mashitaka rasmi wakili husika kwa makosa yake ya kula hela na kukimbia, kukataa kuja kukuwakilisha mahakamani wakati amekula hela yako, kukusababishia hasara kubwa nk.

Usiofu hakuna utakalo lipoteza, pole sanaa kwa maswaibu hayo.

Wakili.
 
Back
Top Bottom