Kesi ya Lwakatare hatarini kufutwa tena

Kesi ya Lwakatare hatarini kufutwa tena

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283

KESI ya ugaidi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph huenda ikafutwa tena na kufunguliwa upya, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Duru za kisheria kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na mahakama zililieleza gazeti hili kwa nyakati tofauti kuwa kesi hiyo huenda ikafutwa tena na kufunguliwa upya kutokana na utata na makosa ya kisheria.

Kosa kubwa linaloelezwa kuwapo katika mashitaka mapya ni kuyaingiza mashitaka yanayowakabili watuhumiwa katika makosa ya sheria ya ugaidi wakati hayana sifa kisheria ya kuwamo katika makosa ya ugaidi.

Endapo kesi hiyo itafutwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, itakuwa mara ya pili kufutwa na kufunguliwa upya.

Baadhi ya wanasheria waliobobea, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa ofisi ya DPP imerudia kosa lile lile ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya kufungua kesi ya ugaidi dhidi ya watuhumiwa huku wakijua fika kwamba makosa yao hayajafikia kiwango cha ugaidi.

Kwa mujibu wa magwiji hao wa sheria ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, makosa ya watuhumiwa hao yamo katika kanuni za adhabu kama makosa ya kawaida kwa mujibu wa sheria, kifungu cha 384, hivyo ni makosa yanayostaili dhamana na hayamo katika makosa ya ugaidi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya polisi wanaochunguza kesi hiyo na ofisi ya DPP.

"Mashitaka yaliyofunguliwa ya ugaidi na DPP dhidi ya washtakiwa yametuweka katika wakati mgumu, maana tunahaha kupata ushahidi kuithibitishia mahakama kwamba hayo ni makosa ya ugaidi," alisema mmoja wa viongozi wa polisi wanaoendelea na uchunguzi wa kesi hiyo.

Kosa jingine kisheria linalodaiwa kufanywa na DPP ni katika shtaka la nne linalomkabili Lwakatare peke yake.
Katika shtaka hilo, Lwakatare anadaiwa kuwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi.

Inadaiwa kuwa Desemba 28, mwaka jana, Lwakatare akiwa mmiliki wa nyumba anayoishi Kimara King'ong'o, kwa makusudi aliruhusu kufanyika kwa mkutano baina yake na Ludovick wa kutenda kosa la ugaidi, kutaka kumteka nyara Denis Msacky, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi.

"Shtaka hili nalo lina makosa kisheria. Kwa wanasheria mahiri kama Tundu Lissu, mawakili wa serikali lazima wajipange. Kwa sababu sheria ya mikusanyiko ya watu, au tuseme kikao au mkutano kama shtaka linavyosema unaanza na watu wangapi?
"Ule mkanda wa video nimeuona, anaonekana Lwakatare akiongea, na mtu mwingine anapitapita na kusikika akiitikia. Maana yake kulikuwa na watu wawili tu. Hicho ni kikao au mkutano?" alihoji mwanasheria huyo.

Habari zaidi zinasema kuwa ili kupata ushahidi wa kutosha kuthibitisha ugaidi unaodaiwa kufanywa na Lwakatare, polisi wanadaiwa kutumia kila mbinu zikiwamo chafu kujaribu kupata ushahidi.

Juzi Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba na Sheria wa CHADEMA, Tundu Lissu, alifichua kile alichokiita moja ya mbinu chafu zinazofanywa na polisi.

Lissu ambaye ni mmoja wa wanasheria katika kesi ya Lwakatare, alidai kuwa polisi kwa kushirikiana na baadhi ya vyombo vingine vya usalama na ujasusi, vimekuwa vikitengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia mahakamani katika kesi ya ugaidi inayomkabili Lwakatare na mwenzake.

Alisema mbali na hayo, pia kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi ya Lwakatare mahakamani.

Lissu alisema mpaka sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi na Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.
"Awali walipewa sh 400,000, wakapewa tena sh 300,000, pia wakapewa sh 35,000 mara mbili. Na pesa zote hizo walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa," alisema Lissu.

Hata hivyo, Lissu alikataa kuwataja vijana hao wa CHADEMA waliopewa fedha hizo. Lakini akamtaja mmoja wa wafanyakazi wa chama hicho aliyekuwa makao makuu (jina tunalihifadhi) na alikwishakufukuzwa kazi kwa kukosa uaminifu, kuwa alikuwa anawafuata na kuwapa fedha hizo.

Habari zinasema kuwa bila kutumia ujanja huu, kesi hiyo inaweza kufutwa na kufunguliwa upya kama ilivyofutwa awali.

Machi 20, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ilimfutia kesi ya makosa ya ugaidi Lwakatare na Ludovick kisha kuwakamata tena na kuwafungulia kesi mpya yenye mashtaka yaleyale ya ugaidi.

Ingawa kesi inapofutwa na DPP hakuna sababu zinazoainisha kufutwa kwake, lakini kesi ya awali ilifutwa kutokana na makosa ya kisheria.

Inaelezwa kuwa kwa vile makosa yake yanahusishwa na ugaidi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina uwezo wa kuisikiliza, lakini badala yake Hakimu Emilius Mchauru aliamua kuisikiliza kinyume na sheria.

Hata hivyo baada ya kesi ya awali kufutwa na watuhumiwa kuachiwa, Lwakatare na mwenzake walikamatwa tena na kufikishwa mahakamani hapo kisha kufunguliwa kesi mpya namba 6/2013, ambayo imepangiwa hakimu mpya, Aloyce Katemana badala ya Mchauru.

Mashtaka mapya yanayowakabili watuhumiwa wa kesi hiyo inayovuta hisia za wengi ni manne.
Shtaka la kwanza linaangukia kwenye sheria ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2002 na makosa matatu yote yanaangukia kwenye sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2002.

Shtaka la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284 cha sheria ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2002.

Chini ya shtaka hilo, inadaiwa kuwa Desemba 28, mwaka jana huko Kimara King'ong'o Stopover, washitakiwa kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Dennis Msacky, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi.
Kosa la pili ni la kula njama ambalo pia linawakabili washtakiwa wote.

Shtaka hili lipo chini ya kifungu cha 24(2) cha sheria ya kuzuia ugaidi Na. 21 ya mwaka 2002 ambapo wanadaiwa kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msacky.

Shtaka la tatu ambalo pia linawakabili washitakiwa wote ni la kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi.
Inadaiwa kuwa Desemba 28, mwaka jana, washtakiwa hao walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyara Msacky.

Shtaka la nne linamkabili Lwakatare peke yake ambalo ni kuwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi.

Inadaiwa kuwa Desemba 28, mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki wa nyumba hiyo iliyopo Kimara King'ong'o kwa makusudi aliruhusu kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msacky.




[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Kesi ya Lwakatare hatarini kufutwa tena
• Polisi, ofisi ya DPP wanyosheana vidole

na Mwandishi wetu
Tanzani Daima

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
[/TD]
 
Wameshaumbuka Mkuu sasa wako busy katika juhudi zao muflisi za kuipanga upya movie yao ambayo watazamaji wameishaistukia. Mara kesi imefutwa mara imefunguliwa tena!!!, Usanii mtupu!!!! Vyombo vyote vya dola (polisi, jeshi na mahakama) vimekuwa ni vitengo vya magamba havina credibility hata chembe!!!

wataumbuka tu ccm
 
Mungu atazidi kumwongoza Lwakatare na siri zao hao wanaoonea binadamu zitafichuka zaidi kwa njia ya midomo yao wenyewe.
 
kama ni haki ya lwakatare mungu anaipigania michezo michofu ya namna hii ina mwisho wake 2015
 
Mimi kinachonishangaza ni kiasi cha fedha zinazodaiwa kuhusika kwenye usaliti, transactions kwa Ludovick ilikuwa 50,000/- hawa laki 4, 3, yaani mtu anaweza kutenda jambo la kwenda hadharani kusema uongo, kuandaa mipango ambayo anajua jamiii itamchukia kwa elfu, 50, laki, hata milioni 10? Itafaa sana tukiwaondoa hawa CCM madarakani tuuangalie upya mfumo wetu wa elimu, hata mtu wa darasa la saba inatakiwa awe na uwezo wa kupambanua mambo kuliko ilivyo sasa graduate ana ubongo wa mjusi!!
 
Polisi na Ofisi ya DPP wanazidisha chuki dhidi y CCM
 
Mimi kinachonishangaza ni kiasi cha fedha zinazodaiwa kuhusika kwenye usaliti, transactions kwa Ludovick ilikuwa 50,000/- hawa laki 4, 3, yaani mtu anaweza kutenda jambo la kwenda hadharani kusema uongo, kuandaa mipango ambayo anajua jamiii itamchukia kwa elfu, 50, laki, hata milioni 10? Itafaa sana tukiwaondoa hawa CCM madarakani tuuangalie upya mfumo wetu wa elimu, hata mtu wa darasa la saba inatakiwa awe na uwezo wa kupambanua mambo kuliko ilivyo sasa graduate ana ubongo wa mjusi!!

Mkuu, sidhani kama ni hiyo elfu 50, laki ... waliyopewa ndiyo iliyowafanya "waasi na kuongopa dhidi ya Chadema". Nahisi hizo ni pesa za uendeshaji tu wa huo mkakati mkuu. Ninaamini wameahidiwa vi milioni kadhaa na maisha bora kama alivyosema Lissu mkuu. Hiyo ahadi ya vi milioni na maisha bora ndo imewafanya wakubali kuwa "makuadi" wa huu "uhalifu" mkuu. Huenda huu ndo utekelezaji wa kauli mbiu yao ya, " maisha bora kwa kila Mtanzania mkuu".
 
Mungu hakika atajidhihirisha juu ya huu udhalimu wa Magamba,ndugu wapenda mabadiliko tuendelee kuiombea CDM tupo kwenye kipindi kigumu lakini uwezo wa Mungu tutayashinda haya majaribu
 
Mungu Mkubwa banaaa!!!...Magamba wanataka kufanya kazi ambazo hawana utaalamu nazo za kutengeneza movie ili kumharibia maisha mtu na kukisambaratisha chama ambacho wanakiona ni tishio kubwa kwao katika kutimiza ile ndoto yao ya "Kutawala Tanzania milele." Movie yao imeflop vibaya sana wanahaha huku na kule kutafuta madirectors wapya ili waitengeneze upya!!! Kwa Watanzania wote wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu chama cha magaidi Tanzania kimejulikana rasmi.

Mungu atazidi kumwongoza Lwakatare na siri zao hao wanaoonea binadamu zitafichuka zaidi kwa njia ya midomo yao wenyewe.
 

KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nguri wa muziki wa kwaya hapa nchini, Mheshimiwa Kapteni John Komba, aliimba wimbo unaosema kwamba amani ya nchi imetoweka.

Katika wimbo huo, Komba ambaye nyimbo zake mara zote hubeba ujumbe mzito uliojaa kila aina ya vionjo vya uzalendo, anatahadharisha kwamba tunakoelekea siko, akiwa anatoa mifano kwa kuzitaja nchi mbalimbali ambapo neno ‘amani' ni msamiati adimu sana.

Bila shaka Komba kasukumwa na mwenendo wa hali ya mambo ulivyo kwa sasa hapa nchini kwetu kwa kutunga wimbo huo.

Huu ni mwenendo wa maisha unaoonesha kwamba amani kwa sasa imegeuka kero hapa nchini, hivyo kila mmoja kutaka kutumia kila njia anayoona inamfaa kutimiza malengo yake bila kufungwa na neno ‘amani'.

Njia hizo za kutaka kufanikisha malengo kwa mtindo haramu wa ‘liwalo na liwe', bila kuyatilia maanani madhara yanayoletwa na mtindo huo wa maisha, ndio unatafsiriwa kama ugaidi kwa sasa.

Zamani, kwa mfano, tulizoea kuyasikia makundi ya kijambazi (kigaidi), huko Ulaya na Urabuni, hasa nchini Italia ambako kulikuwa na vikundi vya Mafia na Red Brigades pamoja na kile cha Uarabuni cha Black September. Makundi hayo yalipotaka kufanya uhalifu, iwe wizi, kuua mtu au uhalifu wa aina yoyote ile, yalikuwa na kawaida ya kutuma ujumbe kwa wahusika na kisha yanautekeleza uhalifu huo kwa muda uleule yanaokuwa yameupanga.

Matukio ya aina hiyo hapa kwetu tuliyazoea kama hadithi tu za kusimuliwa bila kuelewa kuwa upo wakati yatakuja kuwa sehemu ya maisha yetu.

Tulimuomba Mungu atuepushie mbali ili tuendelee kukitunza kisiwa chetu cha kijani katikati ya jangwa, kisiwa cha amani, utulivu na upendo.

Lakini inasemwa kwamba Mungu huwasaidia wanaojisaidia. Yaani wanaojibidisha kukipata kile wanachokiomba kwa Mungu.

Jambo la kusikitisha na kushangaza ni kwamba kwa sasa kisiwa chetu cha kijani kibichi kinaanza kunyauka huku baadhi yetu wakishangilia, kama machizi, wakiifurahia hali hiyo.

Kwa sasa kauli maarufu ya ‘liwalo na liwe' inaonekana kutekelezwa na kutimizwa! Potelea mbali hata tukiwa kama wengine wasiovijua amani, utulivu na upendo.

Kwani wao si binadamu kama sisi! Ndivyo tunavyoelekea kukisambaratisha hivyo kisiwa chetu sisi wenyewe, kisiwa cha amani, utulivu na upendo.

Aisifuye mvua imemnyeshea. Nayaandika haya baada ya kupata ujumbe mfupi wa maandishi (sms) uliojaa kila aina ya vitisho vya kigaidi kufuatia mawazo yangu niliyoyatoa gazetini.

Juma lililopita niliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari: ‘Ni CCM dhidi ya matakwa ya walio wengi'.
Ilikuwa ni makala ya kisiasa, nikijaribu kukishauri chama hicho tawala hapa nchini kuyakubali na kuyaheshimu mabadiliko yanayoamuliwa na wananchi.

Nimeiandika CCM kama taasisi bila kumgusa mtu yeyote binafsi, sababu naamini kwamba CCM ni taasisi.
Watu wanakuja na kupita au kuondoka CCM inabaki. Kwahiyo haina maana kumlenga mtu katika ushauri wa aina ile, awe mwenyekiti, katibu mkuu wala yeyote mwingine katika chama kilicho katika muundo wa taasisi.

Baadaye mwendo wa saa 12 na dakika moja, Jumapili jioni, nikapokea ujumbe mfupi wa maandishi kutoka namba 0684107933 ukisema kwamba: ‘Uko mwandishi wa CHADEMA!! Kazaneni lakini siku yenu inakuja, na kamwe hamtaweza kuikwepa kwa vyovyote vile. CHADEMA iendelee kuwatumia kumtukana JK kila mnapoandika makala zenu!! Siku yaja nitakojoa mdomoni mwenu mmoja hadi mwingine."

Mtu yeyote aliyeisoma makala hiyo inayotajwa hawezi kuonesha mahali popote nilipomtaja Rais Kikwete.
Mtu huyo nikamjibu kwamba hiyo sms nitaishughulikia kisheria, ndipo akajibu hivi: "Shughulika hata leo mbwa mkubwa wewe!! Unajua kwanza unamjibu nani?
Shughulika hata sasa kama utasalimika." Hiyo ilikuwa saa 12 na dakika 24 siku hiyohiyo.

Baadaye saa 12 na dakika 32 akatuma sms nyingine akisema kwamba: "Nasema hivi, tukitaka hata leo tutakufuata kwako kesho wakusome kila gazeti."

Huo ni ujumbe wa kigaidi ambao miaka ya nyuma mtu angeweza kuupuuza kuwa ni jaziba tu iliyompata mtu kutokana na kutoyazoea matukio ya kigaidi.

Lakini kwa sasa kuupuuza ujumbe wa aina hiyo ni lazima mtu upimwe akili zako kuona kama ziko sawasawa.

Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kauli ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Kamuhanda, pale alipokuwa akisakamwa kwa maswali na marehemu Daudi Mwangosi, wakati wakijiandaa kwenda kijijini Nyololo, Mfindi, ambako CHADEMA walikuwa wanafungua matawi ya chama chao.

Kamuhanda alimuuliza Mwangosi: "Hivi wewe mbona hutosheki na majibu ninayokupa? Basi utatosheka huko mbele." Askari mwingine akahadharisha kwamba: "Tunakokwenda huko Mfindi si ajabu wengine wakarudi majina tu."

Na kweli, Mwangosi alirudi jina tu, si kwa sababu nyingine yoyote bali kwa kutimia yale waliyoyasema makamanda wa Polisi. Mwangosi akawa ametosheka na majibu na kurudi jina tu. Kijana akachomolewa roho yake na waliopaswa kuulinda usalama wake! Hiyo ndiyo Tanzania ya sasa!

Kwahiyo baada ya kuupata ujumbe huo wa kigaidi ikanibidi nipeleke taarifa usalama wa raia. Kule polisi wakanipatia RB, TBT/RB/1997//2013, na kunishauri nifungue kesi.

Mshangao ukaja wa nimfungulie nani kesi! Nikajiuliza hivi naweza kuifungulia kesi namba ya simu?
Sababu mawazo yangu yalikuwa kwamba polisi watamtafuta mwenye namba hiyo wamkamate na kumfungulia mashitaka ya jinai kwa kumtishia maisha mwananchi mimi nikiwa shahidi namba moja.

Kwahiyo suala hilo nimeiachia polisi kwa imani kwamba ina uwezo wa kumtafuta huyo gaidi ili kumfikisha mbele ya sheria ikiwa imenihakikishia usalama wangu.

Vitendo hivi vya kutishiana maisha na kufanyiana uhalifu na baadaye kikundi fulani cha watu kudai kwamba ndicho kinachohusika na uhalifu huo tulivizoea kwingine, si hapa kwetu. Lakini kwa bahati mbaya sana sasa hivi tunavishuhudia hapa kwetu!

Tumeanza kushuhudia watu wakitekwa na kudhuriwa, mifano ya karibuni ni ya Dk. Ulimboka na Kibanda. Ila tofauti na kwa wenzetu hatuwaoni wanaojitokeza kudai kuwa ndio wanaohusika na unyama huo, tukiacha kituko cha mtu mmoja aliyedaiwa ni raia wa Kenya kwamba alijitokeza na kusema eti ndiye aliyemteka Dk. Ulimboka.

Hali hii tunayojaribu kuitoa kama haikutafutiwa dawa ya haraka inaweza kutuleta kwenye hitimisho la kwamba Tanzania si salama tena. Maana huwezi kujua adui atatokea upande gani na kwa wakati gani kuja kukudhuru.

Na kibaya zaidi hujui adui yako ni nani. Ni kwa tatizo hilo tutaanza kusema heri ya nchi kama Somalia ambako watu wanajua Al-shabaab wako upande gani au DRC wanakoelewa kwamba M23 wanakaa msitu fulani.

Ni rahisi kujihami na adui unayejua nyendo zake tofauti na hali kama hii inayotaka kuota mizizi hapa nchini, hali ambayo huwezi kujua nani adui yako, kwa nini kawa adui na atatokea upande gani kukushambulia.

Ndiyo maana nasema hali hii ya uadui usiotabirika inawafanya wananchi waanze kuishi kwa mashaka bila kuelewa majaliwa yao ya kesho. Hii ni hali ambayo tunahitaji kuipiga vita kwa pamoja maana ndani yake hakuna aliye salama.

Mfano, Kamanda Barlow angeendaje Kitangiri, kule Mwanza, kama angeelewa kuna maadui zake wanaouwinda uhai wake maeneo yale?

Pamoja na kwamba makala yangu iliyonizulia vitisho ilikuwa inakihusu Chama Cha Mapinduzi, nimefarijika kuona kwamba ndani ya chama hicho kumbe bado wamo wanasiasa wa kweli.

Wanasiasa wasiouchukulia upinzani wa kisiasa kama uadui. Mnatofautiana kiitikadi lakini mnabaki marafiki wa kweli mkiwa watani tu wa kisiasa.
Yupo rafiki yangu ambaye ni kada wa CCM aliyefadhaishwa sana na sms hizo za vitisho nilizotumiwa.

Rafiki yangu huyo kahangaika sana akinishauri tufanye nini katika kujaribu kumbaini huyo gaidi.
Na kadiri juhudi zake zinavyoonesha si ajabu tukafanikiwa kumpata mhusika.

Sina budi kumshukuru na kumpongeza kada huyo wa CCM na mtani wangu kisiasa kwa ungwana wake na uzalendo wa kweli aliouonesha. Natamani awe mfano wa kuigwa kwa wanasiasa wengine hapa nchini.

Kada huyo wa CCM kaonesha kuwa hana umimi, ambalo ni tatizo linalosababisha watu kuanza kufanyiana vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia kwa sasa.

Nasisitiza kwamba hakuna mtu (mwanasiasa) yeyote aliye tayari kumfanyia ugaidi mwenzake kwa msukumo wa mapenzi ya chama chake, iwe kwenye chama tawala au kwenye vyama vya upinzani.

Mambo haya ya kufanyiana ugaidi ni matokeo ya ufisadi ambao unatawaliwa na tabia ya umimi, tabia ya mtu kuangalia tu nafsi yake tu.

Ndiyo maana tunawashuhudia watu walio makada wa chama kimoja wakiwindana ndani ya chama chao kutaka kutoana roho. Haiwezekani kwamba wanayafanya hayo kwa lengo la kukijenga na kukiimarisha chama chao.

Sababu wakishatoana roho ndio mwisho wa nguvu zao katika chama. Kinachopiganiwa hapo ni umimi na wala chama hakipati kitu.

Komba kayaona, amani imetoweka. Tuwe pamoja kuupiga vita au tukubali kuukumbatia ugaidi kwa kuuendekeza ufisadi.


[TD="bgcolor: #FFFFFF"]

Tumeamua kuukumbatia ugaidi?
Prudence Karugendo
Tanzania Daima
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
 
Tuendele na M4C ,Achana na magamba ni matope tuuuuuu.twendeni mwendo mdundo
 
Huyo katibu mkuu wa ccm mkoa wa morogoro aliyetajwa na ludovic kwenye maojiano na polisi kuwa nae muhusika mbona hakamwatwi? Na yule kijana waliosema alikamatwa igunga kwa kosa kumwagia tindikali kada wa ccm ameishia wapi?ccm na polisi mmepanga mambo mengi ambayo mwisho wake ni mbaya kwenu.
 
Mimi kinachonishangaza ni kiasi cha fedha zinazodaiwa kuhusika kwenye usaliti, transactions kwa Ludovick ilikuwa 50,000/- hawa laki 4, 3, yaani mtu anaweza kutenda jambo la kwenda hadharani kusema uongo, kuandaa mipango ambayo anajua jamiii itamchukia kwa elfu, 50, laki, hata milioni 10? Itafaa sana tukiwaondoa hawa CCM madarakani tuuangalie upya mfumo wetu wa elimu, hata mtu wa darasa la saba inatakiwa awe na uwezo wa kupambanua mambo kuliko ilivyo sasa graduate ana ubongo wa mjusi!!

Mkuu ni kweli elimu ni muhimu kutizamwa upya. Lakini ukweli tatizo ni kubwa kuliko tunavyodhani. Mfumo mzima wa maisha ya watnzania umebadilishwa. Wigo wa mahitaji muhimu ya mtu umeongezwa au umeachwa uongezeke sambamba na matamanio yake kwa kasi inayozidi maendeleo ya mtu binafsi na ya taifa pia. Mfano simu, umeme, tv, usafiri, nk sasa zilizokuwa 'wants' sasa ni 'needs'. Mbaya zaidi, mifumo ya kumwongoza mtu kutimiza mahitaji yake imeharibiwa. Njia za mikato, haram na zisizoendana na tamaduni stahiki, maadili na mipango ya nchi ndizo zinazotumika. Elfu 5 au elfu 50 au laki 5 yaweza kutosha kutimiza usaliti
 
Judiciary ya tz ndo ilivyo. Haiko independent na always kuna commands kutoka mahala flani. Ni kawaida pia kwa dpp kusema hakuna kesi na polisi kugangamala na upelelezi.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Judiciary ya tz ndo ilivyo. Haiko independent na always kuna commands kutoka mahala flani. Ni kawaida pia kwa dpp kusema hakuna kesi na polisi kugangamala na upelelezi.

Kinachoonekana hapa ni dhahiri kuwa kuna msukumo wa kisiasa kulazimisha Lwakatare ashitakiwe kwa makosa ya ugaidi wakati ushahidi uliopo ni mdogo sana kushadia makosa ya ugaidi.

Inaonekana DPP hajaridhika na ushahidi uliopo na polisi wanafanya kila wawezalo kutafuta na kutengeneza ushahidi wa kumshawishi DPP.

Lakini kwa hali inavyoendelea tutarajie lolote kutoka kwa DPP, jeshi la polisi au mahakama kuu manake hapa kuna nguvu kubwa sana ya kisiasa inayoizunguka kesi hii kuliko uhalisia na sheria yenyewe.
 
Sisi tuna Mungu, Wao wana fedha.... Sisi tunaongozwa na hekima, wao wanaongozwa na jeuri ya fedha. Mungu akiwa upande wetu, ni nani tena awezaye kututisha? Kwa kuwa Mungu ni mwenye haki, haki siku zote itashinda na udhalimu utapotelea kuzimu!
 
Back
Top Bottom