Kesi ya Lema ngoma nzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Lema ngoma nzito

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mdau wetu, Oct 18, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  UMATI mkubwa wa wananchi wanaojitokeza kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, umemfanya Jaji Aloyce Mujulisi kuamuru isikilizwe katika chumba kikubwa cha mahakama na kufungwa kwa vipaza sauti.

  Uamuzi huo umefikiwa jana na Jaji Aloyce Mujulizi wakati akiahirisha kesi hiyo mpaka Oktoba 25 , mwaka huu, baada ya wapiga chapa wa mahakama hiyo kushindwa kuwapatia mawakili wa wadaiwa nakala ya maamuzi madogo na ya mwenendo wa usikilizaji wa pingamizi la awali kama ilivyokuwa imeamriwa na vikao vya mahakama ya rufaa vinavyoendelea.

  Alisema kuwa kutokana na wananchi wengi kuwa na shauku ya kufuatilia kesi hiyo alimtaka msajili wa mahakama hiyo awapangie ukumbi mwingine ambao ni mkubwa kuliko walioutumia na wafunge vipaza sauti ili wale watakaokosa nafasi ndani wasikilize wakiwa nje.
  Awali jaji huyo waliwaomba wananchi waliofurika ndani ya mahakama hiyo kupungua ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa kukosa hewa lakini walikataa wakimwambia watavumilia hali hiyo.

  Aidha jaji huyo alimtaka msajili wa mahakama kuhakikisha anaweka matangazo kuonyesha siku na mahali kesi hiyo itakapofanyika pamoja na kuandika barua wizarani kuomba kuongezewa muda wa usikilizaji hasa baada ya kuonekana kuwa muda wa mwaka mmoja wa usikilizaji shauri hilo kisheria hautatosha.

  Katika tukio la kushangaza mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa hijabu, aliyejitambulisha kwa jina la Amina Ally na mfuasi wa CCM aliibuka na madai kuwa aliitwa mchawi na baadhi ya watu kwa kuwa alivaa vazi hilo.

  Mwanamke huyo ambaye alikuwa amekaa mbele kabisa kwenye chumba cha mahakama alisema kuwa aliona watu wakimnyooshea vidole ndani ya mahakama kuwa yeye ni mchawi na kuwa kijana mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Rashid alimfuata mara baada ya kesi kuahirishwa na kumwambia kuwa yeye ni mchawi na wangemvua hijabu yake.

  Hata hivyo katika hatua nyingine katibu wa Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) mkoani hapa, Abdulkarim Jonjo, aliyeongozana na mwanamke huyo wakati akiongea na waaandishi wa habari alisema kuwa yeye hakuona mwanamke huyo akinyooshewa kidole ila alisikia tuhuma za kuwepo kwa wachawi.

  Baada ya waandishi kumbana mwanamke huyo kwa maswali lilitokea kundi la wafuasi wa CCM wakawachukua pamoja na katibu huyo wa Bakwata na kuondoka kwa gari la katibu wa mkoa wa chama hicho aina ya Land Criizer VX lenye namba za usajili, T 436 ARX .

  Kwa upande wake mbunge wa Arusha Lema alipoulizwa juu ya suala hilo alisema kuwa yeye hakumnyooshea mtu yeyote kidole ndani ya mahakama hiyo huku akidai kuwa kama kuna anayejihisi kudaiwa mchawi basi ana tatizo.

  Hata hivyo alisema kuwa vijana wa CHADEMA walifanikiwa kumpiga picha mwanamke huyo akifanya vitendo visivyo vya kawaida ndani ya mahakama hiyo vinavyodhaniwa kuwa ni vya kishirikina.

  "Kwenye picha hizo mwanamke huyo anaonekana akijipaka vitu vya ajabu kwenye kucha na akitoa vitu vingine na kuvikandamiza kwenye mikono wakati kesi ikiendelea, mkanda huu tutaupeleka kwa masheikh na wachungaji watuambie kama vitendo hivyo vinakubalika kwenye dini zetu; CCM iache kuchanganya siasa na dini," alisema mbunge huyo.

  Shauri hilo la madai namba 13 ya mwaka 2010 lililofunguliwa na wapiga kura watatu wa jimbo hilo, Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo, wanaowakilishwa na mawakili Modest Akida na Alute Mughwai, mdaiwa wa kwanza, Lema anatetewa na wakili, Method Kimomogoro, na mwanasheria mkuu wa serikali akitetewa na mawakili wa serikali, Juma Masanja na Timon Vitalis.

  Katika matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba, mwaka jana, Lema alimshinda kwa kura nyingi aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Burian, ambaye alikuwa mshindani wake wa karibu kwa tofauti ya kura 56,196 huku Burian akiambulia kura 37460.
   
 2. M

  Maengo JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  2ko pamoja lema!
   
 3. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kesi hii itatushangaza uamuzi wake!
  Tusubiri
   
 4. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  arusha mjini ni chadema tuu hata iweje, miji yote mikubwa imefunguka akili isipokuwa dar tu, maana dar wapiga kura ni wachina na makabachori...
   
 5. m

  massai JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  MWENYEZI MUNGU atatulinda wanachadema na maovu yote,kwani tupo katika kusimamia ukweli na haki na usawa
   
 6. Beautiful Lady

  Beautiful Lady Senior Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uchawi mahakamani.... ! ccm kweli imechoka.
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,819
  Likes Received: 36,912
  Trophy Points: 280

  Salaleee!!! Kwa iyo aliyepigwa picha akifanya mambo ya ajabu yasiyoeleweka hapo mahakani aliambatana na msafara wa CCM na BAR-KWATA.
   
 8. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakerwa sana issue inapokuwa ngumu kwa wenzetu kutumia dini za watu kama ukuta."watanzania hawagawanyiki kwa dini wala kabila! poleni sana
   
 9. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Halafu mchawi mwenyewe was a beautiful lady alijipodoa kucha, vidole uso nk
   
 10. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kwish nehi ccm..
   
 11. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Dini haitakaa itugawanye milele, sisi ni wamoja, watanzania wamoja.

  Waambie watafute njia nyingine
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwanini hawa BAR KWATA wasisimamishe mgombea wao! ? ifikie wakati wajisajili kama chama cha siasa
   
 13. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Baba Katika Jina la Yesu Uzima wa Milele utakuwa nisi CDM Amen
   
 14. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm jamani tazameni mambo haya.
   
 15. K

  Konya JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  siasa za tz ka movie
   
Loading...