Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Ndugu wanaJF
Ile kesi inayo wakabili aliyekuwa kamishna mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya sambamba na Waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, ndugu Sioi Sumari na Bi.Shose Sanare
Leo imepangwa kutajwa June 2 2016 na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande kusubiri kesi hiyo itakaposomwa tena.
Ikumbukwe kabla ya leo: Washitakiwa hao wanaokabiriwa na mastaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza keshi yao, na hapo siku za nyuma washitakiwa hawa walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.
Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande.