KESI YA KITILYA: Mahakama Kuu yatupilia mbali rufaa ya DPP


...hii wanadai husababishwa na mawakili wengi kuwa na kesi nyingi mahakamani,hivyo wanachofanya, ni kutega tu kwenye kosa moja dogo pale kesi ikiendelea hapo hapo wanamaliza mchezo!
 
Nasikia mishahara serikalini inashuka, smart brain wa kujitolea utawapata wapi
 
Sio elimu mkuu ni uadilifu na kutanguliza maslahi ya taifa wengi wanafanya mambo kulinda matumbo yao posipohitaji kutumia taaluma zao chenge mwenyewe kagonga kitu cha havard lakin ona anachofanya.
Radika,
Ukimpeleka wakili mwadilifu sana lakini kilaza, atashinda kesi hii na kuwatia hatiani Kitillya na wenzake...??!

Kilaza = ambae alipita tuu shule ya sheria kumfurahisha baba yake...
 
Wanashinda kesi za wezi wa kuku wasio kuwa na uwezo wakuwalipa mawakili.Wakikutana na mtu mwenye uwezo wakupata mawakili chali.Hawana hasara yeyote wakishindwa kesi serikali italipa.Mshahara mnono na posho wanapewa.Kodi yetu ndio inatumika kulipa fidia.Hii nchi raha Sana.
 
Nakubaliana na wewe!
 
...hapo ndio ujue kazi aliyonayo ngosha kushughulika na mafisadi......naona wamesahau kuwa ufisadi nchi hii wameulea wao hadi ukatamalaki hadi kwenye vyombo vyetu vya sharia....kama wanapinga...waulize nani kwenye kesi ya escrow amefunguliwa mashtaka?....naisubiri hiyo mahakama ya mafisadi nishangae zaidi....JPM ANA KAZI KWELI KWELI...
 
tutaona na kusikia mengi. kesi ya vigogo siijui kama wataweza kununua haki kama kawaida kwenye ile awamu iliyopita? inaelekea maduka ya kuuza haki bado yako wazi.
 
Mheshimiwa magufuli peleka mswada wa kuondoa kinga ya rais ndio mambo yatakaa sawa

Ingependeza sana mkuu. Lakini sote tunajua drama hizo hawezi kumletea kikwete. Yule baba huwa anajua drama haswaa.
Pili,itakuwa na sawa kujipiga bisbisi kwenye makalio mkuu.
 
Kesi nyingine ni mashinikizo ya Kisiasa kwa malengo fulani. Hizo kesi hata umpe malaika apambane na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria,huyo malaika atashindwa tu. Hakuna cha Lawyers wa Serikali kushirikiana na wa kujitegemea kuihujumu serikali, Ukweli utabaki kuwa Ukweli, HII KESI INA WALAKINI TANGU MWANZO, Serikali inapoteza Muda na Fedha kwa kutaka Sifa!
 
Uwezo wa kuzuia dhamana Hana, Mahakama ndiyo yenye last say linapokuja suala la haki.
Ku enter Nolle ProSeQue na kufanya amendment ya Charge Sheet ili kurudisha Money Laundering haiwezekani tena. Remedy aliyonayo ni Appeal to the Higher Court ili kosa hilo lirejeshwe kwani limeshatolewa Uamuzi, na Uamuzi wa Kisutu haukusema warekebishe Charge Sheet, bali hilo kosa halipaswi kuwepo kwa mazingira mazima ya Kesi ya hawa jamaa!
 
Jamani naomba mnisaindie kama kuna kesi serikali imeshashinda naona zote serikali inashindwa ukiacha hile yakina yonna na mramba naona zote chali naanza kuona na hii kesi itaishia serikali kushindwa na kutakiwa kulipa garama za kuendeshea kesi na mabilion yaliopaswa kupewa vijana kama mtaji zinaenda kwa lowassa lakin indirect way namanisha pamela kama hamjanielewa namanisha nn, yy si ndo mke wa yule sijui nani? mtuhumiwa, lakini kwa sababu baba mkwe ayupo kwenye system lazima tumfungee
 
Sheria zetu uta shangaa zinavyo chagua watu nakumbuka yule bwana mkubwa aliye toa bastola akakoki na kumuua dereva wa dala dala lakini ili mradi tu asi wekwe mahabusu kwa kosa la mauaji ika semwa ameua bila ya kukusudia haikuwa haki ila Mungu akaliona akaingilia kati kaenda kuhukumu mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…