KESI YA KITILYA: Mahakama Kuu yatupilia mbali rufaa ya DPP

Hizi 'technicalities' za sheria na taratibu za mahakama zimesababisha watu wengi kupoteza haki zao huko mahakamani. Na wanasheria wengi wamesaidia kushinda kesi nyingi kwa technicalities badala ya hukumu ya haki kwa kesi husika.
===========================================================================
Nashauri tutafute takwimu za wanasheria wameshinda kesi ngapi kwa kutumia technicalities na ngapi za kuhakikisha kesi imehukumiwa kwa haki.

...hii wanadai husababishwa na mawakili wengi kuwa na kesi nyingi mahakamani,hivyo wanachofanya, ni kutega tu kwenye kosa moja dogo pale kesi ikiendelea hapo hapo wanamaliza mchezo!
 
Ndio tatizo la kuajiri vilaza serikalini huku wakiacha vichwa wanaajiriwa na sekta binafsi. Hii ipo tofauti na nchi nyingi zilizoendelea duniani ambapo 'vichwa' huchukuliwa na serikali kwanza. Nchii hii utaratibu wa vilaza kuwa mpaka kiongozi mkuu ndio uliotupelekea huku
Nasikia mishahara serikalini inashuka, smart brain wa kujitolea utawapata wapi
 
Sio elimu mkuu ni uadilifu na kutanguliza maslahi ya taifa wengi wanafanya mambo kulinda matumbo yao posipohitaji kutumia taaluma zao chenge mwenyewe kagonga kitu cha havard lakin ona anachofanya.
Radika,
Ukimpeleka wakili mwadilifu sana lakini kilaza, atashinda kesi hii na kuwatia hatiani Kitillya na wenzake...??!

Kilaza = ambae alipita tuu shule ya sheria kumfurahisha baba yake...
 
Wanashinda kesi za wezi wa kuku wasio kuwa na uwezo wakuwalipa mawakili.Wakikutana na mtu mwenye uwezo wakupata mawakili chali.Hawana hasara yeyote wakishindwa kesi serikali italipa.Mshahara mnono na posho wanapewa.Kodi yetu ndio inatumika kulipa fidia.Hii nchi raha Sana.
 
Ndio tatizo la kuajiri vilaza serikalini huku wakiacha vichwa wanaajiriwa na sekta binafsi. Hii ipo tofauti na nchi nyingi zilizoendelea duniani ambapo 'vichwa' huchukuliwa na serikali kwanza. Nchii hii utaratibu wa vilaza kuwa mpaka kiongozi mkuu ndio uliotupelekea huku
Nakubaliana na wewe!
 
...hapo ndio ujue kazi aliyonayo ngosha kushughulika na mafisadi......naona wamesahau kuwa ufisadi nchi hii wameulea wao hadi ukatamalaki hadi kwenye vyombo vyetu vya sharia....kama wanapinga...waulize nani kwenye kesi ya escrow amefunguliwa mashtaka?....naisubiri hiyo mahakama ya mafisadi nishangae zaidi....JPM ANA KAZI KWELI KWELI...
 
Leo Mahakama Kuu Dar imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashataka(DPP)dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri kurudi Kisutu kufanya marekebisho ya shtaka hilo.

Jumanne wiki hii Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisema kuwa jalada la kesi inayowakabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Msamire Kitilya na wenzake kimsingi bado lipo Mahakama Kuu na kwamba washtakiwa hao walitakiwa kwenda mbele ya Jaji Mfawidhi kwa maelekezo mengine.

Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru pale kesi ya washtakiwa hao ilipokuja kwa ajili ya kutajwa baada ya mawakili wa pande zote mbili kusema ya kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kupata maelekezo kutoka Mahakama Kuu kama ilivyoamuliwa mara ya mwisho.
tutaona na kusikia mengi. kesi ya vigogo siijui kama wataweza kununua haki kama kawaida kwenye ile awamu iliyopita? inaelekea maduka ya kuuza haki bado yako wazi.
 
Mheshimiwa magufuli peleka mswada wa kuondoa kinga ya rais ndio mambo yatakaa sawa

Ingependeza sana mkuu. Lakini sote tunajua drama hizo hawezi kumletea kikwete. Yule baba huwa anajua drama haswaa.
Pili,itakuwa na sawa kujipiga bisbisi kwenye makalio mkuu.
 
Mawakili wa serikali(wanasheria) wanaungana na mawakili wa washtakiwa kuhujumu Jamhuri...

Tunaweza kuliondoa hili kwa wanasheria kuwa POLISI isiwe kama sasa polisi wanakusanya ushahidi na kisha jalada kulipeleka kwa wanasheria(ambao imegundulika wengi wanahujumu)...

Wanasheria wangekuwa MAPOLISI wangejua ni ugumu kiasi gani kupata taarifa za wahalifu.. Kuliko sasa hawana uchungu wowote.
Kesi nyingine ni mashinikizo ya Kisiasa kwa malengo fulani. Hizo kesi hata umpe malaika apambane na mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Sheria,huyo malaika atashindwa tu. Hakuna cha Lawyers wa Serikali kushirikiana na wa kujitegemea kuihujumu serikali, Ukweli utabaki kuwa Ukweli, HII KESI INA WALAKINI TANGU MWANZO, Serikali inapoteza Muda na Fedha kwa kutaka Sifa!
 
Na hata hivyo bado DPP anamamlaka ya kuiondoa hiyo kesi na kuwasilisha hati mpya ya mashtaka akilijumuisha na hilo la kutakatisha fedha baada ya kulifanyia marekebisho yalompa upenyo hakimu kulifuta, wanaachiwa na kukamatwa tena.

Au pia anamamlaka ya kuzuia hiyo dhamana so wala hakuna cha kufurahia maana mchezo ndo kwanza umeanza na hauhitaji hasira unless otherwise DPP awe compromised.
Uwezo wa kuzuia dhamana Hana, Mahakama ndiyo yenye last say linapokuja suala la haki.
Ku enter Nolle ProSeQue na kufanya amendment ya Charge Sheet ili kurudisha Money Laundering haiwezekani tena. Remedy aliyonayo ni Appeal to the Higher Court ili kosa hilo lirejeshwe kwani limeshatolewa Uamuzi, na Uamuzi wa Kisutu haukusema warekebishe Charge Sheet, bali hilo kosa halipaswi kuwepo kwa mazingira mazima ya Kesi ya hawa jamaa!
 
Jamani naomba mnisaindie kama kuna kesi serikali imeshashinda naona zote serikali inashindwa ukiacha hile yakina yonna na mramba naona zote chali naanza kuona na hii kesi itaishia serikali kushindwa na kutakiwa kulipa garama za kuendeshea kesi na mabilion yaliopaswa kupewa vijana kama mtaji zinaenda kwa lowassa lakin indirect way namanisha pamela kama hamjanielewa namanisha nn, yy si ndo mke wa yule sijui nani? mtuhumiwa, lakini kwa sababu baba mkwe ayupo kwenye system lazima tumfungee
 
Sheria zetu uta shangaa zinavyo chagua watu nakumbuka yule bwana mkubwa aliye toa bastola akakoki na kumuua dereva wa dala dala lakini ili mradi tu asi wekwe mahabusu kwa kosa la mauaji ika semwa ameua bila ya kukusudia haikuwa haki ila Mungu akaliona akaingilia kati kaenda kuhukumu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom