KESI YA KITILYA: Mahakama Kuu yatupilia mbali rufaa ya DPP

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Leo Mahakama Kuu Dar imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashataka(DPP)dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri kurudi Kisutu kufanya marekebisho ya shtaka hilo.

Jumanne wiki hii Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisema kuwa jalada la kesi inayowakabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Msamire Kitilya na wenzake kimsingi bado lipo Mahakama Kuu na kwamba washtakiwa hao walitakiwa kwenda mbele ya Jaji Mfawidhi kwa maelekezo mengine.

Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru pale kesi ya washtakiwa hao ilipokuja kwa ajili ya kutajwa baada ya mawakili wa pande zote mbili kusema ya kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kupata maelekezo kutoka Mahakama Kuu kama ilivyoamuliwa mara ya mwisho.
 
KESI YA KITILYA: Mahakama Kuu Dar yatupilia mbali rufaa ya DPP dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri kurudi Kisutu kufanya marekebisho ya shtaka hilo.

Ndio tatizo la kuajiri vilaza serikalini huku wakiacha vichwa wanaajiriwa na sekta binafsi. Hii ipo tofauti na nchi nyingi zilizoendelea duniani ambapo 'vichwa' huchukuliwa na serikali kwanza. Nchii hii utaratibu wa vilaza kuwa mpaka kiongozi mkuu ndio uliotupelekea huku
 
Leo Mahakama Kuu Dar imetupilia mbali rufaa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashataka(DPP)dhidi ya Kitilya na wenzake, yaishauri Jamhuri kurudi Kisutu kufanya marekebisho ya shtaka hilo.

Jumanne wiki hii Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisema kuwa jalada la kesi inayowakabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mwenyekiti wa Enterprise Growth Market Advisors Ltd (EGMA), Harry Msamire Kitilya na wenzake kimsingi bado lipo Mahakama Kuu na kwamba washtakiwa hao walitakiwa kwenda mbele ya Jaji Mfawidhi kwa maelekezo mengine.

Hayo yalisemwa na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru pale kesi ya washtakiwa hao ilipokuja kwa ajili ya kutajwa baada ya mawakili wa pande zote mbili kusema ya kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kupata maelekezo kutoka Mahakama Kuu kama ilivyoamuliwa mara ya mwisho.
Tutapata hukumu yake? We can not comment mpaka tuone hukumu inasemaje!
 
Ndio tatizo la kuajiri vilaza serikalini huku wakiacha vichwa wanaajiriwa na sekta binafsi. Hii ipo tofauti na nchi nyingi zilizoendelea duniani ambapo 'vichwa' huchukuliwa na serikali kwanza. Nchii hii utaratibu wa vilaza kuwa mpaka kiongozi mkuu ndio uliotupelekea huku

Tatizo la kuajili watu kwa vimemo. wengi tu wengine wamepewa hadi nafasi za kua majaji kwa vimemo. Vichwa wanapambana mtaani na hao ndo wanaofanya vizuri
 
Back
Top Bottom