Kesi ya kina Muro upelelezi kuendelea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya kina Muro upelelezi kuendelea

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro  [FONT=ArialMT, sans-serif]Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imekubali ombi la upande wa mashitaka la kuongeza muda wa kuendelea na upelelezi katika kesi inayomkabili Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro na wenzake wawili.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika kesi hiyo, Muro, Edmund Kapama maarufu kama Dokta na Deogratias Mgasa ama Musa, wanadaiwa kula njama, kuomba rushwa ya Sh milioni 10 na kujifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Amri hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkuu Mkazi, Gabriel Mirumbe, anayesikiliza kesi hiyo, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Awali, Wakili wa Serikali, Theophil Mutakyawa, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, lakini aliomba mahakama kuwasilisha hati kutoka ofisi ya Mpelelezi Mkuu wa Kanda ya Dar es Salaam (ZCO), akitaka kuongezwa muda wa kufanya uchunguzi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akijibu hoja hiyo, Hakimu Mirumbe, alisema maombi ya upande wa mashitaka yana msingi na kwamba mahakama inatoa mwezi mmoja wa kuendelea na upelelezi hadi Mei 31, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika kesi hiyo, inadai kuwa Januari, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote na wengine ambao hawapo mahakamani kwa pamoja wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la kuomba rushwa .[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katika shitaka la pili, inadaiwa kuwa Januari 29, mwaka huu, katika hoteli ya Sea Cliff, jijini Dar es Salaam, watuhumiwa hao walitenda kosa la kuomba rushwa ya Sh. 10,000,000 kutoka kwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Inadaiwa kuwa washtakiwa waliomba rushwa hiyo baada ya kumtishia Wage kwamba habari zake za ubadhirifu wa fedha za umma kama Mhasibu wa halmashauri zitatangazwa kwenye luninga.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aidha inadaiwa katika shitaka la tatu, kuwa Januari 29, mwaka huu, katika hoteli ya Sea Cliff, mshtakiwa wa pili na wa tatu wakiwa na nia ovu walijitambulisha kwa Wage kwamba ni waajiriwa na maofisa wa Takukuru huku wakijua sio kweli.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Washtakiwa wote kwa nyakati tofauti walikana mashitaka yao na wako nje kwa dhamana.[/FONT]  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...