Kesi ya huyu mrembo imefikia wapi?


labda ataikana hii siyo passport yake!?
 
labda ataikana hii siyo passport yake!?

Hivi kwanza mkuu, miss TZ iko chini ya wizara gani?? utamaduni na michezo ama??

waziri husika mpaka sasa hajasema chochote?



au huyu mama fenella mukangara anaona hayamuhusu sana haya mambo?
 
Aibu hii ni ya Taifa zima mkuu wala siyo lundenga ama mtemvu!

Na ikifika miss world tu, tuna disqualify kushiriki mara moja! halitokuwa na mjadala hilo hata kidogo!
 
Aibu hii ni ya Taifa zima mkuu wala siyo lundenga ama mtemvu!

Na ikifika miss world tu, tuna disqualify kushiriki mara moja! halitokuwa na mjadala hilo hata kidogo!

nadhan wao wanajua fika vigezo na mashart ya mashindano hayo na wanajua wazi mshindi atashiriki mashindano ya dunia sasa iwete waseme uongo au wampitishe asiefikia vigezo? watajijua bwana.
 
nahisi miss world watatupiga ban la kushiriki miss dunia na mashindayo yote ya kimataifa kama miaka 5 hivi ndio heshima itarudi
 
Hivi kwanza mkuu, miss TZ iko chini ya wizara gani?? utamaduni na michezo ama??

waziri husika mpaka sasa hajasema chochote?



au huyu mama fenella mukangara anaona hayamuhusu sana haya mambo?

huyu ni mwanaccm na kuchakachua ccm ni order of the day!!
 
waka 2005 kulikua na ushindani kidogo, mwaka 2006 kulikua na ushindani wa Wema na Jokate na upinzani huu umeendelea kuwepo kwenye mashindano yetu lakini ya mwaka huu imezidi mno, kumekua na matusi… kashfa na hata naona wamevuka mpaka na kuingiza mambo ya kisiasa ambayo sisi hatuyapendi, huu ni mchezo kama mchezo mwingine wowote… yani taji la mwaka mmoja limefunika mpaka katiba na Simba na Yanga? Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.
Yafuatayo ni mambo waliyoyasema Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.
‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti' – Lundenga
‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemvu…. jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa' – Lundenga
‘Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo' - Lundenga
‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda' – Lundenga
‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga

‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original' – Lundenga
‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu' – Lundenga
Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara' -Sitti
Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji' – Sitti
Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli'
Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao'
Hayo ndio maelezo yaliyotolewa leo kwenye mkutano na Waandishi wa habari…. kama una comment yoyote iandike hapa chini na itatufikia.
 
kuna kitabu kile "mafisadi wa elimu" kimeelezea bayana jinsi wabunge na mawaziri wetu walivyofoji vyeti. Kina makongoro, kina mary nagu, masaburi, bwana mengi, na wengineo. Cha kushangaza wabongo badala ya kushupalia hawa wanao-influence maamuzi ya nchi, wanakomalia miss tz isiyokuwa na chochote!
Je kipi kina athari: miss Tanzania aliyedanganya umri au waziri/mbunge aliyedanganya elimu yake?
 
Muangalie mikono yake kama serena wiliam (sijui nimekosea spelling yule hodari wa teniss) halafu ndo ana miaka 18 lol
 


point tupu 100%
 
Yani anasema taarifa za lešení ya udereva na passport ni mambo binafsi!
 
mimi sikukumbuka tarehe yangunya kuzaliwa siku nakata cheti

nikaandika tarehe nyingine

so kila mtu anaweza akaandika chochote katika cheti cha kuzaliwa
 

hivi sura hii walishindwa kujua kuwa huyu ni mama mtu mzima?
Kwa faida ya wengi umri huonekana kati ya pua,mashavu mkabala na mdomo kuna mifereji kadiri unavyozidi kuelekea utu uzima mifereji hukomaa.
Kwa umri aliodanganya hakupaswa kuwa na mifereji hiyo.
 
hivi kwanza mkuu, miss tz iko chini ya wizara gani?? Utamaduni na michezo ama??

Waziri husika mpaka sasa hajasema chochote?



au huyu mama fenella mukangara anaona hayamuhusu sana haya mambo?

samahani wadau hiyo beji ya bendera ya taifa huwa zinauzwa/patikana wapi? Mie nzalendo bana nataka vaa.msaada pls.
 
Wallah hata kama mtu hujui soma hata knyago washindwa kuelewa,
Huyu anachezea 25 or 24 just guessing due to her out appearance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…