Kesi ya huyu mrembo imefikia wapi?

excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
22,460
Reaction score
17,950
Suala lake la umri wa kichina limekuwa gumzo sana ndani ya muda mfupi!

Nimeona taarifa yake bbc swahili nako wanamzungumzia juu ya sakata lake!

Hii nchi yetu karibu kila kitu kinaendeshwa kimagumashi magumashi tu!



This face at 18yrs! is this possible??
 
Sitti at 18!
 
Muulize ben saanane ndiye anahangaika sana na haya mambo ya mamisi wengine utawaonea tu.
 
Muulize ben saanane ndiye anahangaika sana na haya mambo ya mamisi wengine utawaonea tu.

hahahaa! mkuu Ben Saanane kaacha siasa kaingia kwenye ulimbwende?? au ndiye hassanali??

Lino international wanadai kulishughulikia leo, jumanne!

kama kawaida tungoje only in Tanzania!
 
Last edited by a moderator:
hii issue inafaa kutifuliwa mzizi. Hii mambo ya fix fix, fake fake, inanyima uweledi nafasi yake kila kona nchini. nchi inaendeshwa na watu fake kuanzia wanasiasa, madaktari hadi warembo. Watanzania tuwache hii mambo ya 'funika kombe mwanaharamu apite' Uongo wa kijinga tunakubali, tukiambiwa mafala tunatuna.
 
Tutegemee fix,kamba na justification za kikuda mpaka tukae chini!
 
Kwani sheria inasemaje?akizidi miaka18 haruhusiwi kushiriki?
 
huyu yuko related na watawala hivyo huenda maamuzi yake yakawa kama yale ya kura za akidi ya bunge la katiba.
Mfano ni kijana aliyejinunulia kamtumba kake lakini wajeda wakamuogesha matope na ilivyotokea 'marafiki wa watawala' wakapanda nayo jukwaani ikatolewa taarifa ya onyo!
 

mkuu hii ni case sensitive kabisa!

Mi nadhani wananchi sisi ndiyo maboya kabisa!

Hatuna solidarity hata kama elimu tumekosa!

Kwani hawa viongozi akina kikwete na 'wapigwe tu' imeshindikana nini kutifuliwa hadharani?

Mtanzania kusema ukweli anajihisi anakandamiza kumbe ndivyo anajikandamiza yeye!
 
Wanasema this is the minor and petty issue eti!Eti tumekalia umbea na wivu!!Ni upepo utapita...wakubwa washamaliza mtoto wao hawezi aibika
 
Kwani sheria inasemaje?akizidi miaka18 haruhusiwi kushiriki?

sheria inaruhusu from 18.. the issue is, umri umedanganywa na vivid evidences zipo wazi kabisa!

cheti cha kuzaliwa imeonesha umri tofauti na huu,

driving license na yenyewe ina umri tofauti na 1996 (18 years)

real evidence iliyoletwa ni hii hapa ambayo inakinzana wazi wazi na umri tajwa atia shindano

 
mambwiga tu hao,wanajidanganya wenyewe

maamuzi ni leo jumanne tarehe 21.

tungoje maamuzi kama yatakuwa ya kijuha basi hii nchi tujue ishauzwa waziwazi kila mtu achukue hatua kumi kumi!
 
My beautiful country tanzania kama kawaida atakuja Babu lundenga atasema ule upepo mchafu tuu utatulia.hahaha kweli ONLY IN TANZANIA.

Nasikia JK au baba Ridhi 1 yupo safarini.............?sijui atapitia pia Siera Lione kutoa pole?
 

Haki kabisa mkuu hii inaonekana wazi kabisa wakuu wamemshika mkono wazi wazi kabisa!

Nina wasiwasi sana na waliovujisha vyeti vya huyu mlimbwende kama watakuwa salama!
 
My beautiful country tanzania kama kawaida atakuja Babu lundenga atasema ule upepo mchafu tuu utatulia.hahaha kweli ONLY IN TANZANIA.

Nasikia JK au baba Ridhi 1 yupo safarini.............?sijui atapitia pia Siera Lione kutoa pole?

hiyo haiwezeani aisee!! hahahaa! mkuu wa nchi anapenda kuzurura lakini hapa hatoenda kamwe!
 
Wakati wa kuandikisha vitambulisho vya uraia tuliambiwa zaidi ya askari 300 waligushi vyeti. Sasa ikiwa wachunga sheria ndio hivyo sasa vipi kwa warembo?

Hii nchi imejaa danganya toto kwa asilimia 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…