Kesi ya EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya EPA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mizambwa, Feb 16, 2012.

 1. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Wadau naomba kuelimishwa kuhusu kesi za ubadhirifu wa mapesa ambazo watuhumiwa walifikishwa mahakamani. lakini kwa sasa mambo yamekuwa kimya sijui ni mimi tu sipati muendelezo wa habari kuhusu hizi kesi mfano EPA, RICHMOND, IPTL na zinginezo.

  Au vyombo vya habari wamechoka kuandika kuhusu hizi kesi kwani haieleweki kama wale ni bado watuhumiwa au washitakiwa.

  naomba mwenye kuelewa mnijuze.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huto yasikia siunajua maji yakiwa ya moto hata kutia kidole unaogopa,yakisha poa unatia mguu mzima ndio mambo ya EPA na mwengineyo,wakitaka kupitiasha mambo yao wanaanza na jambo kubwa ili balaa lilopita mlisahau.
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  tumewasamehen ila wasirudie tena.
   
 4. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Cha ajabu hata Wabunge ambao ndio waliyavumbua mambo yale, nao wapo kimya kabisa. Tuliambiwa kuwa watuhumiwa wanarudisha zile pesa za EPA, baadaye KIMYAAAAAAAAAAAAAA

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wabunge wetu ni wasanii tu, wapo mjengoni kuvimbisha matumbo yao na kusinzia tu!! Zitto alianzisha hoja dhidi ya Mustapha Mkullo kuhusu shirika la Consolidated holdings na jinsi waziri wa fedha alivyofanya hujuma ya kiwanja cha serikali, lakini Zitto huyo huyo inspite ya kuzungumza bungeni mpaka povu likamtoka mpaka leo hajafuatilia hoja ile ili kujua hatima yake. Inaelekea wanapiga kelele bungeni ili wapate publicity kupitia luninga na magazeti basi ndio mwisho wao.
   
 6. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Au inawezekana kuwa wanazibwa midomo kwa kumwagiwa mchele mifukoni mwao, Serikali ikishaona hoja ni nzito inawajaza mchele wananyamaza kimya.

  Huku mitaani tunawasifu kuwa wanapambana na ubadhirifu kumbe ni kutafuta umaarufu na kujazwa mchele tu.

  Tuliambiwa watuhumiwa wanarudisha pesa lakini haieleweki nani karudisha na nani bado. Leo wote wapo mitaani wanakula raha wanatupita na VX V8 sisi tunaning'inia kwenye daladala zetu.

  ACHENI NISEME, ATA WAKINUNA ACHENI NISEME, HATA WAKINIMWAGIA MAJI WASHA ACHENI NISEME, HATA WAKINIPIGA MABOMU ACHENI NISEME......!!!!!!!!!!!!!!

  MWENZENU NINA WASIWASI NA WABUNGE WETU HASA WANAOPIGA KELELE BUNGENI KUNA KITU WANAPATA HAWA TUWACHUNGUZE.

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
Loading...