Kesi ya akina Slaa kusikilizwa Januari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya akina Slaa kusikilizwa Januari

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 22, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Kesi ya akina Slaa kusikilizwa Januari

  Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 21st December 2011 @ 12:00 Imesomwa na watu: 54; Jumla ya maoni: 0

  [​IMG]
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="align: right"]
  [TR]

  [/TR]
  [TR]

  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Marquee"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  USHAHIDI wa kesi inayomkabili Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbroad Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na wafuasi 26 wa chama hicho walioshitakiwa kwa ajili ya mkusanyiko usio halali na kutoa lugha ya uchochezi, umekamilika na kesi hiyo itaanza kusikilizwa Januari 23, mwakani.

  Wanadaiwa kutenda kosa hilo katika Jiji la Arusha katika Viwanja vya NMC Novemba 7 na 8, mwaka huu.

  Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, mbele ya Hakimu Devotha Kamuzora, Wakili wa Serikali, Ellen Rwijage alidai upande wa mashitaka uchunguzi umekamilika na kuomba kupangwa kwa usikilizwaji wa awali.

  Pia wakili huyo aliomba Mahakama hiyo itoe amri ya kumtaka Lissu, kuja na vielelezo vya kuonesha kama alikuwa mgonjwa na kiasi cha kushindwa kuhudhuria mahakamani jana.

  “Mheshimiwa pamoja mdhamini wake Calistus Lazaro, amekuja hapa kusema amepigiwa simu, lakini bado tunaomba Mahakama yako imwagize huyu mshitakiwa aje na kithibitisho siku ya kesi itakapopangwa ya kuonesha alikuwa mgonjwa Desemba 21 mwaka huu,” alisema Rwijage.

  Akijibu ombi hilo, Hakimu Kamuzora, alisema mshitakiwa siku ya kesi afike na kielelezo cha kuonesha ni mgonjwa na pia itaanza usikilizwaji wa awali Januari 23, mwakani.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  badala ya kulijenga taifa tunahangaika na migogoro uchwara.......
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  serikali iliyopoteza muelekeo ndo dalili zake hizo.huwa siku zote wana deal kwa nguvu zote na mambo yasiyo na tija kama haya
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Lissu hakufika, Slaa alifika?
   
Loading...