Kesi ya Abdul Nondo itawavua nguo Serikali na Jeshi la Polisi mchana kweupe

Tukwazane Taratibu

Senior Member
Dec 20, 2012
195
537
Mimi ni mpenzi wa Mwanafizikia wa zamani Albert Einsten (Baba wa mabomu ya nyukilia/atomiki duniani), zamani kidogo baada ya msomi huyu wa Kiyahudi kuikimbia Ujerumani na kutimkia Marekani alikumbana na vikwazo mbalimbali alipokuwa katika harakati zake za ugunduzi wa urutibishaji wa atomiki, katika harakati zake hizo za kuvikwepa vikwazo alisema “We can not solve our problems with the same level of thinking that created them” akiwa na maana ya kwamba hatuwezi kuyatatua matatizo yetu kwa fikra zile zile zilizoyatengeneza.

Ili uweze kuyatatua matatizo yanyokukabili yakupasa kufikiri kwa akili tofauti na ile uliyoitumia kuyasababisha matatizo hayo, kwa wale waliopata kuisoma Fizikia/Hesabu wanajua ukiitumia njia kulikabiri swali na ukakosa yakubidi kubadili njia ili ulipate jibu sahihi. Vivyo hivyo matatizo yanyoikabili jamii zetu yapaswa kutatuliwa kwa akili tofauti na ile iliyoyaleta.

Tarehe 13 ya mwezi huu niliandika humu na kuituhumu serikali juu ya mwenendo wake kwa sakata la Abdul Nondo, nilionya juu ya walakini ulioonyeshwa na jeshi la polisi na wawakilishi wa serikali kwa kijana huyu mdogo.

Hadi kufikia jana polisi walikuwa wamekaa nae kwa takribani siku 13 bila ya kumpandisha mahakamani kitendo ambacho ni kinyume na sheria, sheria inawataka polisi kukaa na mtuhumiwa masaa 24 tu kisha kumpandisha mbele ya mahakama. Cha kushangaza ni kwamba Polisi hawajali wala hawazingatii sheria hii, wameonyesha ya kwamba wao wako juu ya sheria za nchi.

Baada ya wanaharakati na vyombo mbalimbali vya utetezi wa sheria kuibuka mahakamani kuwashitaki IGP, DCI na AG mahakamani tarehe 19/03/2018 Polisi kwa aibu kubwa wakamkimbiza Abdul usiku usiku kumpeleka mkoani Iringa ili akafunguliwe mashitaka huko huku wakijua kwamba kesi dhidi yao imefunguliwa masijala ya Mahakama kuu Dar es Salaam dhidi yao kwa kitendo cha kumnyima dhamana na kutompeleka mahakamani kwa siku 13.

Kitendo cha polisi kukaa na mtuhumiwa/mwathirika kwa siku zote hizo bila ya kumpandisha mahakamani wala kumpa dhamana na bila kuruhusu ndugu zake au mawakili wake kumuona kina portray mambo kadhaa.

1. Kwamba Polisi wako juu ya sheria na kwao sheria haina makali, kama jeshi la polisi lingekuwa linatii sheria bila shuruti kama wanavyohubiri laiti wasingojea hadi waitwe mahakamani kwa oda ya "habeas corpus". Suala hili la kukaa na Nondo kwa siku zote hizi limeonyesha jinsi polisi walivyo viburi mbele ya sheria, haya yanaweza kutokea kwa nchi ambayo haitii sheria na inaongozwa kwa njia zisizo za kidemokrasia. Vinginevyo walipaswa kumlipa fidia na kisha kumuachia Nondo kwa kumpotezea mda.

2. Polisi hawajali juu ya matumizi mabaya ya raslimali na pesa za Watanzania.
Jeshi la Polisi likiwa linatambu ya kwamba Nondo alitekewa Dar es Salaam na alitolea taaarifa juu ya yaliyomkuta akiwa Dar es Salaam, wao bila kujali juu ya uhabirifu wa mafuta, pesa na vipuri vya magari/ndege wamemsafirisha hadi Iringa akafunguliwe mashitaka huko, huku kwenye hati zao za mashitaka walizoziwalisha mbele ya hakimu zikionyesha kwamba kosa wanalomtuhumu nalo lilitendekea Dar.

Bad enough walijua kwamba kesi imefunguliwa masijala ya Dar, kulikuwa na ulazima gani kumsafirisha hadi Iringa? Kama siyo uharibifu wa fedha za walipa kodi? Sote tunajua nia ambayo imekuwa ikinadiwa na serikali ya awamu ya 5 juu ya matumizi makubwa ya fedha, ni kwa nini polisi watumie kiasi hicho cha pesa bila ulazima wowote? Kama watasema ya kwamba alistahili kushitakiwa Iringa tutawauliza kulikuwa na ulazima gani wa kumleta kwa mahojiano Dar ? kwani Iringa hakuna wapelelezi?

3. Mashitaka waliyomfungulia Abdul Nondo yanatia kinyaa.
Nimeisoma hati ya mashitaka iliyowasilishwa na wakili wa serikali kwa mahakama ya wilaya ya Iringa juu ya kesi ya Abdul Nondo hakika nimebakia mdomo wazi. Wamemfungulia kesi 2

I: Ya kwamba Abdul alipotosha umma kwa kutumia simu yake kumtumia rafiki yake ujumbe mfupi (meseji) kwa njia ya Whatsapp kwamba yuko katika hatari. Ukilitazama shitaka hili kwa njia ya sheria utaona ni kwa kiasi gani litapanguliwa kirahisi sana mbele ya mahakama.

Swali la kujiuliza ni je, ujumbe huo ulitumiwa umma upi ambao Jeshi la polisi linataka kuwaaminisha Watanzania kwamba ulikuwa wa upotoshaji? Kwa sababu aliyetumiwa ujumbe ni rafiki yake na si umma wa Watanzania kama polisi na serikali wanavyotaka tuamini. Dai hili linawavua nguo waedesha mashitaka, mawakili wa serikali na jeshi la polisi kwa ujumla.

II: Shitaka lao la pili linasema eti Abdul alimdanganya mfanyakazi wa umma ambae ni Kopro Salim (E2328) wa kituo cha polisi cha Mafinga ya kwamba alitekwa jijini Dar es Salaam. Na kwamba uongo huo ulimfanya Kopro Salim kuendesha uchunguzi juu ya tukio hilo kitu ambacho asingefanya kama asingedanganywa na Nondo.

Mashitaka haya yote mawili ukiyasoma na kuyatathimini kwa akili ya tofauti unaona yalivyokosa ubunifu, uelewa na akili ya tofauti sawa na ile iliyoyatunga.
Kwa nini nasema hivi? Kwa sababu zifuatazo.

1. Jeshi la Polisi na viongozi wa serikali akiwemo Paul Makonda na Mwigulu Nchemba walikwisha toa hitimisho ya kwamba Abdul hajatekwa bali alijiteka mwenyewe na hata hati ya mashitaka walioifungua inasema hivyo. Huo ndio msimamo wao lakini kitu cha kushangaza zaidi baada ya mjadala kuendeshwa makamani wakili wa serikali alisimama na kumuomba hakimu amnyime dhamana Abdul Nondo dhamana kwa sababu ya kwamba yuko hatarini na kama angeruhusiwa kwa dhamana watekaji wangepata nafasi ya kumteka tena hivyo kuwa katika hatari zaidi ya maisha yake.

Hapa ndio unaona sasa maana ya ule msemo wa Albert Einstein nilioutoa mwanzoni kabisa mwa makala hii. Polisi na serikali hawajulikani wanataka nini kwa Nondo, hawaeleweki wanaamini nini juu ya sakata hili maana maelezo na utetezi wao unakinzana tokea siku za mwanzo kabisa za tukio hili, na hili limethirika mbele ya mahakama.

NINI KITATOKEA BAADA YA KESI HII?
Jeshi la polisi litaonyesha rangi yake halisi. Kuanzia mwanzo wa sakata hili jeshi la polisi limeonyesha ni namna gani linavyoendesha shuguli zake kwa kukanyaga sheria (kama nilivyoonyesha hapo mwanzo).

Kama jeshi lingekuwa linatii sheria na kuheshimu utu wa watu linaowalinda lisingethubutu hata kidogo kukaa na Abdul kwa siku 13 na kumhukumu kana kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kisheria ya kuthibitisha yaliyomkuta Abdul Nondo. Kwa siku nyingi jeshi la polisi limekuwa likituhumiwa kwa kuendesha mambo yake kwa "UONEVU" na kutofuata misingi ya haki na sheria, hakika sakata hili limezidi kuthibitisha hivyo.

Kwa sasa Watanzania waamini kwamba Jeshi la polisi siyo chombo chao cha kuwalinda, chombo hiki kimekuwa kikituhumiwa kwa kugubikwa na rushwa sana katika utendaji wake wa kazi miaka kwa miaka (kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za ndani ya nchi), ni wazi kwamba sakata hili la Abdul Nondo limeingiliwa na viongozi wa serikalini ambao ndio maboss wa moja kwa moja wa jeshi hili (kwa mujibu wa statements zao), hivyo hii inawafanya Watanzania watambue ya kwamba ukiwa dagaa utatendewa sawa na Abdul Nondo ila ukiwa chengu utafikishwa mahakamani mara moja na haki yako utapatiwa.
Abdul Nondo atashinda kesi yake mchana kweupe hata bila ya wakili , maana makosa aliyoshitakiwa nayo ni dhaifu na yaliyokosa nguvu ya kisheria na kimantiki.

NINI KIFANYIKE ILI JESHI LA POLISI NA SERIKALI WASIJIVUE NGUO TENA HUKO MBELENI?

Kwanza kabisa mfumo wa uendeshaji wa jehi unatakiwa kubadilishwa na kuwatoa kutoka kwenye dhahania ya kwamba wao ndio walinda amani wa wananchi hadi kuwa watumishi wa wananchi. Amani ya nchi inaanza na mtu mmoja mmoja, amani ya nchi inaanza na jamii, serikali inao wajibu wa kuwekeza kwenye jamii na kuifanya jamii kutambua ya kwamba amani ya kweli inaanza kwenye nafsi zao.

Jeshi la polisi liwepo kama huduma kwa jamii pale inapohitajika kutoa huduma kama uokozi, ulinzi katika sehemu za umma (viwanja n.k), kuendelea kuwafanya polisi kama ndio waliosimamia amani ya nchi katu hakutaweza kutatua matatizo ya nchi hii, bali kutaendelea kuwafanya kuwa wanyanyasaji na waonezi wa watu. Kutaendelea kuwafanya kuipuuza sheria (kama walivopuuza kumpandisha Nondo mahakamani kwa wakati kama sheria inavyotaka).

Mtafiti mmoja alipata kusema ya kwamba ili kulifanya Jeshi la Polisi kuwa la kisasa na la kuthaminika zaidi kwa wananchi basi linapaswa kubadilika kwa kupitia hatua zifuatazo.
A. Engage citizens
B. Empower police officers
C. Optimize ways of working
D. Predict and improve services through analytics.
E. Enhance collaboration
F. Pro actively manage change.

Kwa hatua hizo 6 hapo juu kutalifanya jeshi kuweza kuhudumu kwa mda mrefu na kwa kizazi kijacho bila ya tuhuma wala matatizo yoyote sawa na haya tunayoyashuhudia kutoka kwao kwa sasa.
 
wanaotoa maoni mazuri kama haya,hivi ni kwa nini wanachukiwa na hawa watu?hivi watanzania tumelogwa na nani?yaani miaka yote hii ya uhuru bado tunashindwa kujitambua utu wetu?haya maajabu sijui yataisha lini,hivi kweli kama tunashindwa kuelewa haya tutaweza kweli kuwa na kiwanda chetu wenyewe, mimi nadhani tujikite kwenye kuendeleza uchawi kuliko kuangaika na viwanda
 
Ndugu mimi naona unawaonea tu hawa walinda amani na utulivu wa nchi. Kama mahakama imekubaliana na waendesha mashtaka kuwa ni vyema na haki huyo dogo aendelee kubaki mahabusu kwa usalama wake ina maana polisi walikuwa sahihi kukaa naye. Ni mtazamo tu ndugu.
 
Kuna watu wengi wa taasisi ya kipolishi watapata hasara,tena hasara kubwa sana huko mbeleni.
Ombeni Mungu asiingie mtawala mwingine mwenye mtaizamo wa kutenda haki,mwenye mtizamo wa kitawala kwa mujibu wa sheria,mwenye mtizamo wa KUNYOOSHA NCHI IPASAVYO watalia na kusaga meno.
 
Back
Top Bottom