Kesi mbili za Kikatiba kuhusu kudai demokrasia kuanza kusikilizwa Ijumaa Machi 9, 2018 Mahakama Kuu Kanda ya Dar

Kijana wa Chacha Wangwe ambaye ni mlalamikanji katika mojawapo ya hizo kesi simwelewielewi. Hivi ni yule aliyekuwa diwani, akajiuzulu then akaonekana kwenye "pipa" akipelekwa SA? Au ni mwingine?
 
Kwa kweli tuwaombee sana maana hili suala ni zito mno. Kwa hali iliyopo ni kuweka maisha rehani.
 
Kijana wa Chacha Wangwe ambaye ni mlalamikanji katika mojawapo ya hizo kesi simwelewielewi. Hivi ni yule aliyekuwa diwani, akajiuzulu then akaonekana kwenye "pipa" akipelekwa SA? Au ni mwingine?
Mlalamikaji anaitwa Bob chacha wangw sio Yule aliejiuzulu
 
Hali ilivyo sidhani Kama litakubalika maana mtashindwa kufanya kazi
Ni aibu mwanasheria mkuu na timu yake watakavyokuwa wanasasambuliwa hadharani. Kuficha aibu ni lazima kila aina ya ubabe utumike.
 
Kijana wa Chacha Wangwe ambaye ni mlalamikanji katika mojawapo ya hizo kesi simwelewielewi. Hivi ni yule aliyekuwa diwani, akajiuzulu then akaonekana kwenye "pipa" akipelekwa SA? Au ni mwingine?
Sio yy
 
Mashauri mawili ya kikatiba yaliyofunguliwa na umoja wa wanaharakati wa kudai demokrasia Tanzania yataanza kusikilizwa Ijumaa Machi 9, 2018 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mashauri hayo ya kikatiba yalifunguliwa katika mahakama hiyo na umoja huo kwa kushirikiana na wanasheria kupinga namna demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa kujieleza na kukusanyika unavyokiukwa hapa nchini.

Pia mashauri hayo yalilenga kuhoji namna utendaji wa vyombo vilivyoundwa kwa mamlaka ya kikatiba vinavyoikiuka katiba hiyo.

Mratibu wa Umoja huo Dk Makongoro Mahanga amesema kesi hizo zitatajwa Ijumaa mahakamani hapo, kuanzia saa tatu asubuhi.

Amesema shauri namba 6/218 lililofunguliwa na Bob Chacha Wangwe, akisimamiwa na Wakili Fatuma Karume kuhusu Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi litatajwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu.

Dk Mahanga amewataja majaji hao kuwa ni Jaji Wambali JK, Jaji Mwandambo J na Jaji Teemba J.

Amesema shauri namba 4/2018 lililofunguliwa na Francis Garatwa, Baraka Mwango na Allan Bujo ambao wanatetewa na Wakili Jebra Kambole kuhusu Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya vyama vya siasa litatajwa mbele ya jopo la majaji watatu ambao ni Jaji Wambali JK, Jaji Sameji R na Jaji Teemba J.

“Wananchi wapenda demokrasia ya kweli ni vema na busara kuhudhuria na kufuatilia mashauri haya yatakayokuwa yakiendelea kunguruma Mahakama Kuu, ”amesema Dk Mahanga.

Chanzo: Mwananchi
UKOMBOZI - TANZANIA UNAKARIBIA... ILA KWANZA WATANZANIA WAJITAMBUE WAANZE KUDAI HAKI ZAO.
 
Kama JK yupo, hapo tutegemee kesi kuishia kwenye LEGAL TECHNICALITIES (ufundi/sarakasi za kisheria) itachukua muda kusikilizwa kwenye hoja za msingi (MERITS). Maana nimeona posts nyingi huko nyuma zikimtuhumu -ve E.g Kesi ya Kafulila.
 
Dar es Salaam. Mashauri mawili ya kikatiba yaliyofunguliwa na umoja wa wanaharakati wa kudai demokrasia Tanzania yataanza kusikilizwa Ijumaa Machi 9, 2018 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mashauri hayo ya kikatiba yalifunguliwa katika mahakama hiyo na umoja huo kwa kushirikiana na wanasheria kupinga namna demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa kujieleza na kukusanyika unavyokiukwa hapa nchini.

Pia mashauri hayo yalilenga kuhoji namna utendaji wa vyombo vilivyoundwa kwa mamlaka ya kikatiba vinavyoikiuka katiba hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Mratibu wa Umoja huo Dk Makongoro Mahanga amesema kesi hizo zitatajwa Ijumaa mahakamani hapo, kuanzia saa tatu asubuhi.

Amesema shauri namba 6/218 lililofunguliwa na Bob Chacha Wangwe, akisimamiwa na Wakili Fatuma Karume kuhusu Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi litatajwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu.

Dk Mahanga amewataja majaji hao kuwa ni Jaji Wambali JK, Jaji Mwandambo J na Jaji Teemba J.

Amesema shauri namba 4/2018 lililofunguliwa na Francis Garatwa, Baraka Mwango na Allan Bujo ambao wanatetewa na Wakili Jebra Kambole kuhusu Sheria ya Jeshi la Polisi na Sheria ya vyama vya siasa litatajwa mbele ya jopo la majaji watatu ambao ni Jaji Wambali JK, Jaji Sameji R na Jaji Teemba J.

“Wananchi wapenda demokrasia ya kweli ni vema na busara kuhudhuria na kufuatilia mashauri haya yatakayokuwa yakiendelea kunguruma Mahakama Kuu, ”amesema Dk Mahanga.
 
Ee Mwenyenzi Mungu uwalinde hao wote waliofungua hayo mashauri ya kupata tafsri za hizo kesi. Amen
 
Back
Top Bottom